Instagram story viewer> @comrade_tizeba> Post
a year ago
0
Posted On: September 30th 2025, 08:09 am
Tagged Users:
Wana Nzengo wenzangu wa Kata ya Nzegandogo, tumekuwa na Safari nzuri ya Maedeleo kwa kipindi cha 2020-2025 kwa kugusa Sekta mbalimbali za Maendeleo kwenye Kata yetu kwa kuzingatia vipaumbele.

Kwa kipindi cha 2025-2030 nitahakikisha yafuatayo yanatekelezeka;

I. Kufikisha Maji kwenye Vitongoji vyote na kuweka utaratibu stahimilivu kwa Wananchi kulipia gharama ya Tsh. 30,000/= ya kuunganishiwa maji kwenye Kaya zao tofauti na gharama ya 150,000/= iliyopo sasa na ujenzi na ununuzi wa Pump ya maji ili kutumia maji ya Mgodi wa zamani wa Resolute kwaajili ya matumizi ya kibinadamu, kilimo na mifugo.

II. Ujenzi wa Zahanati za Iyuki na Ikulu na upatikanaji wa Mtaalamu wa Mionzi (x-ray) na ununuzi wa Gari ya kubeba wagonjwa (ambulance) kwa Kituo cha Afya cha Zogolo.

III. Ujenzi wa Barabara na Madaraja kutoka Kijengele hadi Bukingwa, Nzegandogo hadi Malilika, Iyuki hadi Kabale na Ikulu hadi Ipilyaza.

IV. Ujenzi wa Bweni la wasichana wa shule ya Sekondari Nzegandogo.

V. Kuhakikisha Umeme unafika kwenye Vitongoji vyote na wananchi wanaunganishiwa kwa gharama stahiki ya Tsh. 27,000/=.

VII. Uanzishwaji wa Stendi ya Malori Center ya Nzegandogo ili kuhamasisha na kukuza Biashara pamoja na kuinua Uchumi wa Mwananchi mmoja mmoja huku Serikali ya Kijiji cha Zogolo ikipata mapato pia.

Tujitokeze wote Oktoba 29, 2025 kufanya maamuzi sahihi kwaajili ya Safari yetu nyingine kwa kupiga KURA zote za Ndiyo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

#NzegaYetuKeshoYetu
#OktobaTukatiki

More posts

back to up