MWAKA ULIPOANZA NA WEWE ULISEMA HUU NI MWAKA WAKO? Na aje mpaka sasa ni mwaka wako tu? Ngoja nikufundishe jambo kuhusu MALENGO au mipangilio. MALENGO yoyote yanakuwa yana rekodiwa ndivyo akili zetu zilivyo usiporekodi hutojua kama nayakaribia au Bado yako mbali au Niko nia sahihi
Step 1
ANDIKA MALENGO YOTE UNAYOTAKA KUYAFIKIA
Step 2
ANDIKA KUANZIA MADOGO KWENDA MAKUBWA
Hapa wengi tunafeli kwenye kuandika MALENGO kwakuwa huwezi Andika nataka nyumba Ya milioni Mia wakati tofali la elfu 2 au 1500/ huwezi fikia, hivyo Andika MALENGO kwa ufanisi inakuwa Kama unajipima
A) je naweza kuwa na uthabiti? (Consistency?)
B) je Nina nidhamu na MALENGO yangu?
C) je ninapojiwekea MALENGO namanisha?
D) je ni MALENGO sahihi au nimekurupuka?
Step 3
HAKUNA MELENGO YANAYOTIMIA USIKU MMOJA HIVYO INAWEZA CHUKUAMIEZI SITA, MWAKA, MIAKA MIWILI NA KUENDELEA KUTIMIA Hapa epuka ile kauli ya "mwaka ujao naanza upya, badala yake Sema mwaka ujao naendelea kwenye 2.4.6... Acha kuanza kila mwaka "kata hiyo roho"
Step 4
WEKA VIASHIRIA KUWA HII SASA NI DALILI NAYAKARIBIA MALENGO YANGU, mfano Ukianza kukutana na connection za watu wa hardware wakati unataka kujenga nyumba unajua kabisa kuwa ohoooo sio mbaya sio mbaya
Step 5
ACHA KUPELEKWA MBIO NA MAMBO YA MJINI
Maana mwaka huu watakuja na trend za magari, mwezi haujaisha utashangaa trend ni nyumba mwaka haujaisha utashangaa trend ni Dubai mwaka haujaisha utashangaa trend ni simu, hivyo STAY ON YOUR LANE!✅
Step 6
KUBALI KUCHELEWA ILA SIO KUACHA, ukiona mambo yanakuwa mazito unafeli unakwamishwa Shikwa na hasira, Ingia chumbani kwako piga keleleeeeee kisha lamba sukari😄 Rudi kwenye MALENGO yako! Afe Beki afe simba
Step 7
TAFUTA WATAALAMU WA MAMBO - Ingia gharama kujifunza mambo zaidi, Acha ubahili kwenye ndoto yako. Ukitaka kuwa tajiri utaambiwa mambo Ya share , hisa, bond , real estate, sasa huwezi ukatoka tu kuamka na matongotongo yako ukaanza kuyafanya, TAFUTA WATAALAMU WAKUSHIKE MKONO ACHA UBAHILI.
Anyway swali langu lilikuwa ni je huu Bado ni mwaka wako???
@almas_microfinance_ltd#viral #reels #instagram #entrepreneur #discipline