Posted On: July 21st 2026, 02:14 pm
Kuna chapisho nililisoma kupitia kwa mchambuzi na mwandishi wa habari za michezo na tetesi za usajili Hans Rafael Mwombeki kuwa Simba SC kupitia coach wao Steve Barker wanapush deal la kumpata Peter Shalulile na kama ikishindikana basi watarejea msimu mpya wakimtumia Mpanzu kama false 9 kama msimu uliomalizika akisaidiana na Sele Gomez Mwalimu
Hii imenifanya kufikiria kwa kina zaidi kwa namna gani striker wenye quality ya juu jinsi ilivyo ngumu kuwapata kwasasa sokoni tofauti na maeneo mengine ya kiuchezaji uwanjani
Na ndiyo maana pia tangu Mayele atuache ni misimu kadhaa sasa hatujapata Striker wa level ya juu kama ya Mayele mwenyewe, Bocco, Kagere, hivi karibuni ni kama Jonathan Sowah alitaka kutuaminisha kitu lakini bahati mbaya mambo ya nje ya uwanja yamekuwa mengi kuliko
Sasa Shalulile amemaliza mkataba wake na Mamelod hivyo yupo huru, tetesi pia zinasema anazo offer kadhaa pale pale South Africa ikiwemo ya Orlando Pirates lakini pia za nchini Libya ambako yeye binasi anadhaniwa kuwa ndipo anapafikiria zaidi
So, licha ya ofa hizo zote kubwa still coach wa Simba anaonekana kuwa huyu ndiye option yake pekee sokoni ni kama inatisha hivi kuiwazia hii🤔
Lakini yote kwa yote kama Simba wakimpata Peter Shalulile nadhani itakuwa ni deal bora sana kwao kwasababu ya ubora aliokuwa nao na uzoefu wake wa muda mrefu wa kucheza mpira wa ngazi ya juu kabisa ya Afrika na kuwa mshindi wa kila kitu kuanzia timu mpaka mafanikio binafsi
Umri wa miaka 32 siyo jioni sana ukizingatia intensity ya ligi yetu na uhalisia wa wachezaji tuliyokuwa nao so far, so kwangu mimi binafsi ni addition bora sana kuiendea ✅️
Ligi yetu kupitia vilabu vyetu vikubwa imeendelea kufungua milango taratibu ya hatua za ukuaji hususani kwenye recruitments ukilinganisha na tulipotoka ilikuwa siyo rahisi kuwaendea wachezaji wanaowika kwenye ligi bora kama South lakini miaka miwili hii uanaona uthubutu wa mpaka kujaribu kuwavunjia mikataba wachezaji wa ligi hizo so we still moving up 🤝
MAFANIKIO HAYAJI KWA KUJIKATIA TAMAA 🙏
#simbasc #ligikuu #afrika #tanzania #football