Posted On: July 27th 2026, 09:36 am
Nakumbuka 08/2022 mpaka 08/2025,hii miaka 3 nilijua Maana ya KUKATALIWA,KUKOSA,nilijua Maana ya kulala njaa,nilijua nani Rafiki,nani ndugu
Katika kipindi ambacho nilihisi ndio mwisho wangu,Kumbe Mungu alikuwa ananiandaa kwa HATMA iliyo njema,
Hata kama sivyo nilivyotarajia,Ila amenibariki zaidi ya nilivyotegemea
Naandika haya Leo kukupa Moyo Binti ambaye huenda Jana ulikataliwa,Jana ulilala njaa,na mpaka sasa hujui kama utapata riziki yoyote
USIKATE TAMAA, katikati ya dharau Kuna HESHIMA,katikati ya KUKOSA Kuna KIBALI KISICHOKUWA NA MIPAKA
MUNGU aliyenishindia na kuniinua tena,Atafanya zaidi na zaidi kwako
MUNGU ANAKUPENDA ANAKUWAZIA MEMA
HAJAKUSAHAU