Posted On: September 5th 2026, 07:16 pm
Moja kati ya taarifa ambazo zinasambaa kwa kasi ni pamoja na taarifa inayomuhusu Influencer na mfanyabiashara Kutoka Uingereza mwenye asili ya Nigeria, Igho Ubiribo (43), amefariki nchini Thailand baada ya kuchomwa sindano za kuongeza ukubwa wa uume.
Baada ya kufanyiwa matibabu hayo, Ubiribo alianza kupata maumivu makali ya kifua na baadaye akazimia. Alikimbizwa hospitalini, lakini alifariki licha ya juhudi za madaktari kumuokoa.
Uchunguzi wa mwili wake baada ya kifo ulibaini kuwa kemikali ya hyaluronic acid iliyotumika kwenye sindano hizo iliingia kwenye mishipa ya damu na kufika kwenye mapafu. Hali hiyo ilisababisha kuziba kwa mishipa ya damu kwenye mapafu, tatizo linalojulikana kama pulmonary embolism, ambalo lilichangia kifo chake.
@mshuaramy_ Load More