Posted On: September 26th 2026, 07:00 pm
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusisitiza kuhusu wajibu wa watu waliopata fursa ya elimu kwa kusema:
“Wengine wapatao upendeleo huu wa kipekee, wana wajibu wa kulipa fadhila kutokana na wengine kujitoa mhanga kwa ajili yao. Wao ni kama mtu ambaye amepewa chakula chote kilichopo ili aweze kuwa na nguvu za kuleta vyakula vingi zaidi. Iwapo atachukua chakula hiki na kushindwa kutoa msaada kwa ndugu zake, basi atakuwa msaliti. Vivyo hivyo, endapo vijana wa kiume na wa kike watapata elimu na watu wa Jamhuri hii na kujiona bora zaidi, au wakashindwa kutumia maarifa waliyopata kusaidia maendeleo ya nchi hii, basi watakuwa wasaliti wa umoja wetu.”