Posted On: September 27th 2026, 10:42 am
Siku ya Jumamosi, tarehe 26.09.2026,
@wizara_ya_malazi_daruso @darusomlimani, kupitia Waziri wake Mheshimiwa
@aphilidolini ametoa ufafanuzi kuhusu maandalizi ya hosteli kuelekea mapokezi ya wanafunzi wapya (Freshers) yanayotarajiwa kuanza kufanyika tarehe 17 Oktoba 2026.
Katika ufafanuzi huo, Waziri alisisitiza pia kuhusu mpango wa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza wanaotarajiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka wa masomo 2026/2027, ambapo chuo kimetenga utaratibu wa kuwapatia na kuwapangia vyumba vya hosteli wanafunzi hao kwa idadi yao kwa mwaka wa masomo.
Alieleza kuwa utaratibu huo unalenga kuhakikisha wanafunzi wapya wanapata sehemu za malazi kwa utaratibu unaoeleweka wanapoanza masomo yao katika chuo...
Aidha,Waziri alieleza mambo muhimu yanayohusu hali ya hosteli, maandalizi na taratibu zinazopaswa kuzingatiwa na wanafunzi wapya katika kipindi cha mapokezi.
maandalizi yanaendelea!kuhakikisha wanafunzi wapya wanapata mazingira rafiki na salama wanapoanza safari yao ya elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam...
@darusomlimani
@wizara_ya_maji_malazi_daruso @aphilidolini
@presenter_eysher#udsmofficial#darusomlimani#wizara_ya_maji_malazi_daruso