Posted On: October 3rd 2026, 05:54 pm
NGORONGORO: KUJIFUNZA, KUGUNDUA NA KUTHAMINI URITHI WA TANZANIA.
Tarehe 3 Oktoba 2026, Tanzania Heritage & Tourism Alliance (THTA) iliandaa safari ya utalii kwenda Hifadhi ya Ngorongoro, ikiwa na lengo la kuwaunganisha washiriki na utajiri wa urithi wa asili wa Tanzania.
Safari hii ilikuwa fursa ya kujionea kwa karibu mandhari ya kipekee, wanyamapori na bioanuwai inayopatikana katika eneo hili muhimu la urithi wa asili.
Kupitia programu za aina hii, THTA inaendelea kuhamasisha utalii wa ndani, kuongeza uelewa kuhusu vivutio vya Tanzania na kuimarisha dhamira ya jamii katika kuhifadhi rasilimali za taifa.
Tunaamini kuwa kuitambua na kuithamini Tanzania ni hatua muhimu katika kuilinda kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
THTA – KUHAMASISHA UTALII, KUTHAMINI URITHI NA KUENDELEZA UHIFADHI.
#THTATanzania #Ngorongoro #UtaliiWaNdani #UrithiWaTanzania #Chakwetukitunzwe