Posted On: October 20th 2026, 05:10 am
Unapitia changamoto ya ndoa? Haupati matunzo ya mtoto? Kuna mgogoro wa mirathi katika familia yako? Au una kesi inayohusu haki za mtoto na hujui pa kuanzia?
Usibaki na changamoto hizi peke yako!
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kupitia timu yake ya wanasheria, kinaendelea kutoa msaada wa kisheria katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, kwa wananchi wenye changamoto za kifamilia, mirathi na haki za watoto na mashauri mengineyo.
Katika wiki hii ambayo kituo hicho, kinaadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake, tunakukumbusha kuwa, LHRC ipo hapa kila siku za huduma, si kwa ajili ya maadhimisho pekee.
Share ujumbe huu kwa ndugu, rafiki au jirani anayepitia changamoto hizi ili nae apate kusaidika.
#LHRC #MsaadaWaKisheria #humanrights #HakiZaWatoto #legalaid