Posted On: October 21st 2026, 08:56 pm
🤍 HII NI KWA AJILI YA MUNGU (GOD & ALLAH) 🤲🏽
Kila tunachokifanya, kila maisha tunayogusa, na kila tendo la upendo tunalolifanya, tunalifanya kwa ajili ya Mungu (God/Allah). Tumeumbwa kuwa sababu ya furaha kwa wengine, kuwasaidia wenye uhitaji, kuwapa matumaini waliokata tamaa, na kuonyesha upendo kwa wanadamu wote bila kujali dini, kabila au hali zao za maisha.
Kwetu sisi, kusaidia wenye uhitaji si tendo la kibinadamu pekee, bali pia ni namna ya kuonyesha upendo wetu kwa Muumba wetu. Tunatamani kila tunachokifanya kipate baraka na kibali kutoka kwa Mungu.
Tunachofanya si kwa ajili ya sifa za wanadamu, bali kwa ajili ya Mungu (Allah), ambaye ndiye anayejua nia za mioyo yetu. ❤️🙏🏽
📖 Suratul-Baqarah 2:272
“Na kheri yoyote mnayoitoa, basi ni kwa ajili ya nafsi zenu, wala hamtoi ila kwa kutaka radhi ya Allah.”
📖 Wakolosai 3:23
“Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.”
🦅 THE VISION OF EAGLE FOUNDATION
ONE LOVE ONE HEART TOGETHER WE CAN HELP SOMEONE