Posted On: November 2nd 2026, 03:30 pm
Yesu wangu, hakuna kama wewe ❤️🙌 Kila ninapokumbuka wema wako, moyo wangu unajaa furaha na kinywa changu kinakosa maneno ya kukushukuru. Umenivusha mengi, umenilinda na umekuwa nami hata pale nilipohisi niko peke yangu. Wewe ni Mungu wa ajabu, mwenye upendo usio na mwisho. Sina cha kujivunia zaidi ya neema yako maishani mwangu. Nitaendelea kukusifu, kukuabudu na kulitangaza jina lako, maana wewe ndiye mwanzo na mwisho wa tumaini langu. Utukufu wote ni wako Yesu wangu, leo na milele. 🙏❤️🔥
.
.
.
#sisindowaletunaosaidiwanabwana
#jesusismylife #love