Posted On: November 3rd 2026, 11:39 am
🕊️💔 TAARIFA YA HUZUNI: JESÚS DE MIGUEL AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 30.
Soka la Hispania limegubikwa na majonzi kufuatia kifo cha mshambuliaji wa CD Tenerife 🇪🇸, Jesús de Miguel, aliyefariki dunia Jumanne hii baada ya kupata ajali mbaya wakati wa mchezo dhidi ya FC Andorra.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika dakika za mwisho za mchezo, baada ya Jesús kugongana kwa nguvu na kipa wa timu pinzani, Jesús Owono 🇬🇶.
Baada ya tukio hilo, alipatiwa huduma ya kwanza ndani ya uwanja kabla ya kukimbizwa hospitalini kwa dharura kufuatia kupata tatizo la kusimama kwa moyo na kupumua. Kwa bahati mbaya, licha ya juhudi zote za madaktari na wahudumu wa afya, hakufanikiwa kunusurika.
Mchezo huo ukiwa katika matokeo ya sare ya mabao 2-2, ulisimamishwa kabisa kufuatia tukio hilo.
🙏 Mawazo na pole zetu za dhati ziende kwa familia yake, ndugu, jamaa, marafiki, wachezaji wenzake na familia nzima ya CD Tenerife katika kipindi hiki kigumu.
Pumzika kwa amani, Jesús de Miguel. 🕊️❤️
#kidosportsupdates#RIPJesusDeMiguel #FootballFamily