Posted On: November 3rd 2026, 02:38 pm
@dsetanzania Yashiriki Uzinduzi wa Tawi na ETF Mpya ya
@orbit_securities Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) imeshiriki katika ufunguzi wa tawi jipya la Orbit Securities katika Jiji la Arusha na uzinduzi wa bidhaa mpya ya uwekezaji ya Orbit Multi Asset ETF. Akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa DSE, Mkurugenzi wa kampuni tanzu ya
@csdr_tz , Ndugu Benitho Kyando, amesema ukuaji wa soko unaendelea kuchochewa na ongezeko la wawekezaji na thamani ya miamala, inayotarajiwa kufikia TZS trilioni 2 ifikapo mwisho wa mwaka 2026. Amesisitiza kuwa DSE iko tayari kuboresha mifumo ili kuhudumia wawekezaji wengi zaidi na bidhaa mbalimbali. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil.
Sasa, wawekezaji wanaweza kununua Orbit Multi Asset ETF kupitia Hisa Kiganjani.