Instagram story viewer> @greathopetz> Post
10 months ago
Co Creator: humphreyevarist
Photo by Great Hope Foundation on January 08, 2026.
Photo by Great Hope Foundation on January 08, 2026.
Photo by Great Hope Foundation on January 08, 2026.
Photo by Great Hope Foundation on January 08, 2026.
1
Posted On: January 8th 2026, 08:57 am
Tunapoendelea kuadhimisha miaka 10 ya PROGRAMU YA UWEZO, leo, tunaangazia mmoja wa wahitimu wetu wenye msukumo, @humphreyevarist.

"Naitwa @humphreyevarist. Nilianza kushiriki katika program ya UWEZO mwaka 2018 nikiwa mwanafunzi kiongozi wa @jitegemeesecschool. Katika ushiriki huo, niliwezesha shule yangu kushiriki kikamilifu na hatimaye kushinda tuzo ya fedha, tukiwa washindi wa 13, kupitia mradi wa utunzaji wa mazingira uliolenga kuhamasisha uwajibikaji wa vijana katika uhifadhi wa mazingira shuleni na kwenye jamii inayozunguka shule.

Baada ya kumaliza shule, nilivutiwa sana na uratibu mzuri na weledi wa mradi huu, jambo lililonichochea kuendelea kushiriki zaidi. Kupitia hilo, nilipata fursa ya kujitolea kama Mratibu wa Wilaya ya Ubungo, na baadaye mratibu wa Wilaya ya Kibaha. Katika nafasi hizi, nilihusika na uratibu wa shule, walimu, wanafunzi, pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha mchakato wa tuzo unatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.

Kupitia mradi huu niliweza kujifunza Uongozi na Uwajibikaji, jinsi ya kujenga uwezo wa kuongoza timu tofauti, kufanya maamuzi kwa haki, na kusimamia rasilimali kwa uwazi. Pia, uratibu wa Programu na Miradi imenifunza namna ya Kupanga, kutekeleza na kufuatilia shughuli kwa kuzingatia malengo, muda na matokeo yanayotarajiwa. Pamoja na Tathmini na Ubora (Assessment & Quality Assurance) imenifunza jinsi ya Kuimarisha uwezo wa kuchambua miradi, kutoa maoni ya kitaalamu, na kuhakiki ubora wa ubunifu na athari za kijamii.

Kwa kuzingatia uzoefu na uaminifu nilioujenga, baadaye nilipata nafasi ya kuwa miongoni mwa Majaji wa mradi wa #uwezoaward kwa awamu mbili, jukumu lililoniongezea maarifa ya kitaalamu katika tathmini ya miradi ya vijana na uamuzi wa haki.

Kwa sasa, mimi ni Mratibu wa Taasisi ya @global_impact_transformation (GIT), ambapo nimekuwa nikiratibu matukio na miradi mbalimbali ya vijana, nikiunganisha wadau, kuendeleza vipaji, na kuhakikisha miradi inaleta athari chanya na endelevu. Maarifa na uzoefu nilioupata kupitia mradi huu yamekuwa nguzo muhimu katika kazi yangu ya sasa hasa katika uongozi, uratibu wa programu, na tathmini ya miradi yenye athari kwa jamii.”
Comments (1)
omarism_1 10 months ago

omarism_1

Smart🔥

More posts

back to up