Posted On: July 18th 2026, 05:04 am
Siku ya jana imekuwa ya umuhimu wa kipekee kwa mradi wetu. Familia ya
@lamgambotz ilikutana tena kuendelea na maandalizi, na kubwa zaidi ni kwamba wasanii wetu wote wamekabidhiwa rasmi uhusika wao kulingana na mswada wa onyesho 💯
Rasmi sasa, maneno yaliyopo kwenye maandishi yanaenda kupewa uhai, hisia, na pumzi jukwaani na timu hii ya kipekee.
Tunaandaa kitu kikubwa na cha tofauti sana kwa ajili yenu 🔥🔥🔥
Endelea kukaa karibu na ukurasa huu ili kuona jinsi wahusika hawa wanavyozaliwa siku hadi siku 🙌
Tuandikie neno moja la heri kwa wasanii wetu wanapoanza safari hii ya kuvaa uhusika wao tafadhali 💪🏾💯🔥
LA MGAMBO
Jukwaa Letu, Maadili Yetu
LA MGAMBO inafadhiliwa na mpango wa ruzuku wa Feel Free. Mfuko huu unatekelezwa na Nafasi Art Space, Kwa msaada wa ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania na ubalozi wa Norway - Dar es salaam.
#LaMgambo#FeelFreeGrant2026#SwissEmbassyTz#NorwayInTz#Edutainment