Posted On: July 6th 2026, 04:46 am
THOMAS TUCHEL
Unazungumzia mwalimu ambaye anajua sana kuusoma mchezo ukiwa unaendelea na kuja na jibu ambalo litakuwa tiba kwa timu yake hususani kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji (substitutions)
Mechi mbili mfululizo amefanya sub ambazo zinaenda kumpa kile kitu anachokihitaji na kuifanya timu yake kusogea hatua inayofuata
Game ya Mexico imekuwa ngumu na ukizingatia wamepata kadi nyekundu kuanzia dakika ya 53 hivyo ilibidi kulishikilia tu bomba mbungi iishe 🙌 Mexico walikuwa hatari sana
Rasmi chama letu linaenda robo fainali na mpinzani wa sasa ni Norway ya Haaland
MASTER TOM TUCHEL KATUPELEKA ROBO FAINALI 🤝 HII NI MPAKA FAINALI 📌
#england #fifa #worldcup #footbal #mexico