Posted On: October 31st 2026, 08:05 am
Mwaka 2012 kwenye mahafali ya kumaliza kidato cha sita, shule ya sekondari Tambaza. Picha hii nilipiga na 'Geography department' baada ya kupokea zawadi ya bingwa wa Geography. Sio hapo tu, Dar es salaam huwa kuna mtihani unaitwa TAHOSSA, niliibuka mshindi pia wa somo la Geography kwa kanda hiyo. Nakumbuka nilipewa zawadi ya Dictionary ya Geography pamoja na cheti ambacho walikuja kukichukua wakakisain na sikukiona tena hadi leo.
Enzi hizo nilikua na ndoto za kuwa RUBANI/PILOT ndio maana nilisoma PGM. Nawashukuru wote waliowezesha safari yangu ya masomo, kwakweli Mwenyezi Mungu awabariki sana. Nilipo leo, mna mchango mkubwa sana!
Load More