Posted On: November 3rd 2026, 07:32 am
Nimefurahi sana kupata fursa ya kukutana na Balozi
@liberata_mulamula , mshauri wetu katika maswala ya Ushirki wa wanawake katika ujenzi wa Amani
@global_impact_transformation na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika kuhusu Wanawake, Amani na Usalama (AU Special Envoy on Women, Peace and Security).
Ni heshima kubwa kuendelea kujifunza na kubadilishana mawazo na kiongozi mwenye uzoefu mkubwa katika diplomasia na ujenzi wa amani barani Afrika. Uongozi wake katika kusukuma mbele ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama ni chachu muhimu katika kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuzuia migogoro, michakato ya upatanishi na kufanya maamuzi yanayohusu amani na usalama.
Amani ya kweli na endelevu inahitaji wanawake kuwa sehemu ya maamuzi, si sehemu ya mijadala pekee. π
#gitimpact #WPC2026 πΉπΏ
Load More