Instagram story viewer> @kcmc1971> Post
18 hours ago
Photo by KCMC on November 04, 2026. May be a Twitter screenshot of one or more people, poster and text.
Photo by KCMC on November 04, 2026. May be a Twitter screenshot of one or more people, poster and text.
6
Posted On: November 4th 2026, 12:11 pm
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC, Prof. Gileard Masenga, amewasilisha taarifa kuhusu mafanikio ya Dkt. Happiness Rabiel, aliyeshinda tuzo ya Daktari Bora wa Mwaka 2026 katika Mkutano wa 13 wa Tanzania Health Summit (THS), wakati wa kikao cha Bodi ya Utawala - GSF kilichofanyika leo, Novemba 4, 2026.

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa wajumbe wa Bodi, Prof. Masenga ameeleza kuwa tuzo hiyo ni utambuzi muhimu wa ubora wa kitaaluma, weledi, kujituma na mchango mkubwa wa Dkt. Rabiel katika sekta ya afya nchini.

Dkt. Happiness Rabiel ni daktari bingwa bobezi wa upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu katika KCMC. Alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo katika mkutano wa Tanzania Health Summit uliofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 7 Oktoba 2026, katika Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, tarehe 5 Oktoba 2026, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alimkabidhi Dkt. Rabiel cheti cha utambuzi pamoja na zawadi ya fedha taslimu Shilingi milioni moja baada ya kutangazwa mshindi.

Dkt. Rabiel alipata ushindi huo katika ushindani uliohusisha pia madaktari kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Upigaji kura ulifanyika kupitia tovuti ya tuzo za Tanzania Health Summit, huku juhudi za uongozi wa KCMC kuhamasisha watumishi na wananchi kumpigia kura kupitia mitandao ya kijamii zikichangia mafanikio hayo.

Katika taarifa yake, Prof. Masenga amesisitiza umuhimu wa mafanikio hayo kwa KCMC, Chuo Kikuu KCMC na Good Samaritan Foundation (GSF), akieleza kuwa tuzo hiyo inaonesha mchango wa wataalamu wa taasisi hizo katika utoaji wa huduma za afya za kibingwa na kibingwa bobezi, kuboresha ubora wa huduma na kuimarisha imani ya umma kwa taasisi hizo.

Dkt. Happiness Rabiel ni miongoni mwa madaktari bingwa bobezi wawili wa kwanza wa kike wa upasuaji wa ubongo nchini Tanzania. Kwa sasa, anahudumu kama Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Jumla na Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu katika KCMC na Chuo Kikuu KCMC.
Comments (6)
janemrosso2018 14 hours ago

janemrosso2018

Congratulations Dr. Rabiel.👏🏾👏🏾🔥🔥

akilichanya_tz 14 hours ago

akilichanya_tz

👏👏👏

jeimkulima 15 hours ago

jeimkulima

Let the fire burn ......Dr Rabiel🔥🙌

veronica_kessy_ 15 hours ago
nickymagarimoshi 17 hours ago

nickymagarimoshi

🔥🔥🔥🔥

More posts

back to up