instagram story viewer > #HABARI

#HABARI

Posts
#Habari | Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti, baada ya kula kiapo cha Ubalozi na kusubiri kupangiwa kituo cha kazi, amepokea maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kuitumikia nafasi yake mpya. Kwa urefu zaidi, tembelea YouTube channel yetu ya EastAfricaTv #EastAfricaTv | #Habari
#HABARI Jinsi Mama mzazi wa James Temba, alivyoangua Kilio kwenye jeneza la mwanae mara baada ya kuwasili ndani ya Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania Dayosisi ya Mashariki ya Pwani usharika wa Tabata tayari kwa ibada. #EastAfricaTV
#HABARI Muigizaji maarufu nchini Tanzania @nicolejoyberry amewatoa hofu mashabiki zake kuwa yupo salama baada ya kupunguza nyama za chini ya kidevu. Unaongeleaje muonekano wake kwa sasa? ✍🏿 @mariamshabanitz #taimweusi🦅 #taimediatz #taimediatv #tanzania
— Mvutano wa chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini unachukua sura mpya na ya kuhuzunisha. Hivi karibuni, kumeibuka malalamiko kutoka kwa wanawake wazawa wa Afrika Kusini ambao wameolewa na raia wa Nigeria, wakidai kuwa sasa wanatengwa na kunyanyaswa ndani ya jamii zao wenyewe. Kwa mujibu wa ushuhuda uliotolewa, wanawake hawa wanatakiwa “kuwafuata waume zao Nigeria,” huku uadui ukiongezeka kutokana na hisia kali dhidi ya wahamiaji zinazoendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Hali hii inaibua maswali mazito kuhusu haki za kiraia, umoja wa Kiafrika, na usalama wa familia zinazounganisha mataifa mawili makubwa barani Afrika. Nini maoni yako kuhusu hali hii? Tumbukiza neno lako hapa chini. 👇 Usipitwe na habari na video mpya kila siku — Follow page yetu sasa @nasseraltaie.media 📢✨ #Habari #AfrikaKusini #Nigeria #Xenophobia #HabariZaKimataifa
#swahiliconnecttv #swahiliconnect #swahiliconnectupdates #habari #tanzania
Anko hana baya😁😁
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, tarehe 8 Machi 2026 amemtembelea na kumjulia hali Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Zahir Ally Zorro, nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es Salaam. Mhe. Mwinjuma amemkabidhi Mzee Zorro kiasi cha Shilingi milioni 10 taslimu kama salamu za pole na faraja kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimtakia apone haraka. Akizungumza baadaa ya kufika kumjulia hali, Mhe. Mwinjuma amesema Serikali inaendelea kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na wasanii wakongwe katika kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni wa Tanzania na kuwa wasanii hao ni hazina muhimu ya taifa, hivyo wanastahili kuenziwa na kupewa faraja wanapokumbwa na changamoto mbalimbali za kiafya au kijamii. Kwa upande wake, Mzee Zorro alitoa shukrani zake kwa Rais Samia pamoja na Serikali kwa upendo na kujali hali yake, akisema msaada huo ni faraja kubwa kwake na kwa familia yake katika kipindi hiki anachopitia. #Habari #SAT MediaUpdates
work and prayer🙏
Kwa mujibu wa @guinessworldrecord Kuku aitwaye Gertie ametajwa kuwa kuku mzee zaidi duniani! Akiwa na manyoya mazuri ya kahawia na meusi yenye madoadoa, Gertie ni kuku wa aina ya Golden Sebright ambaye licha ya umri wake mkubwa bado anaonekana mwenye afya na haiba ya kipekee. Kila asubuhi, mmiliki wake Frank Turek (USA) humtembelea na Gertie humsalimia kwa sauti ndogo kabla ya kuanza kula chakula chake kwa bidii. Ameishi na mmiliki wake tangu mwaka 2010. Inasemekana kuwa Gertie ni kipofu, lakini bado hupenda kupumzika pamoja na rafiki yake mbwa aina ya Great Dane na kutembea ndani ya banda lake. Mnamo Novemba mwaka jana, Gertie aliweka rekodi ya dunia akiwa na umri wa **miaka 15 na siku 100**, akimshinda aliyekuwa mshikiliaji wa rekodi hapo awali kwa zaidi ya miezi sita! Mmiliki wake anasema licha ya kuwa mdogo kuliko kuku wengine, Gertie alikuwa mrembo sana tangu akiwa mdogo na ndiye aliyekuwa “mpiga picha” bora zaidi kila wakati. Leo hii, Gertie anaendelea kuishi kama “malkia” wa banda, akiongoza kuku wengine kwa utulivu na heshima. 📌Hakika, hii ni historia ya kipekee kwa dunia ya wanyama!* #GuinnessWorldRecords #Habari #Kuku #RekodiYaDunia #Gertie
VIDEO: Arsenal imekuwa gumzo kubwa msimu huu baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika michuano ya UEFA Champions League. Timu hiyo kutoka London imefanikiwa kufika hatua ya fainali, jambo ambalo limewapa mashabiki wake matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa. Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka, Arsenal ina nafasi ya asilimia 85 ya kushinda kutokana na rekodi nzuri ya mechi zilizopita na uimara wa kikosi chao. Safari ya Arsenal kuelekea fainali haikuwa rahisi. Walikabiliana na timu kubwa barani Ulaya na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, mbinu bora za kiufundi, na mshikamano wa wachezaji. Ushindi wao dhidi ya wapinzani wakubwa ulionyesha kuwa kikosi hiki kimekomaa na kina uwezo wa kushindana na timu yoyote. Mtangazaji na mchambuzi wa michezo wa Uyui Fm Kimwaga Shaban @kimsports_ alitabiri mapema kuwa Arsenal ingeweza kufika fainali, na sasa utabiri huo umeonekana kuwa sahihi. Mashabiki wengi wamekuwa wakimpongeza kwa kuona mbali na kuamini katika uwezo wa kikosi cha kocha Mikel Arteta. Hii imeongeza hamasa na mjadala mkubwa miongoni mwa wapenzi wa soka. Hata hivyo, licha ya nafasi kubwa ya kushinda, bado kuna mashaka kidogo. Baadhi ya wachambuzi wanaamini kuwa presha ya fainali na uzoefu wa wapinzani inaweza kuwa changamoto kwa Arsenal. Timu pinzani mara nyingi hujipanga kwa ustadi mkubwa katika hatua ya mwisho, na makosa madogo yanaweza kugharimu ubingwa. Mashabiki wa Arsenal duniani kote wanasubiri kwa hamu siku ya fainali. Wengi wanaamini huu ndio msimu wa historia kwa klabu hiyo, kwani mara ya mwisho walifika fainali ya Champions League ilikuwa mwaka 2006, lakini walishindwa kutwaa taji. Safari ya sasa imewapa matumaini mapya ya kuandika ukurasa mpya wa mafanikio. Kwa ujumla, Arsenal imeonyesha kuwa ni timu yenye uwezo mkubwa na ari ya ushindi. Ikiwa wataendelea na nidhamu na umakini waliouonyesha katika hatua zilizopita, nafasi ya kutwaa ubingwa ni kubwa. Fainali hii itakuwa kipimo cha kweli cha nguvu zao na inaweza kubadilisha historia ya klabu hiyo kwa miaka mingi ijayo. @kimsports_ #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #Media
#Repost @itvtz #HABARI: Wananchi Mkoani Wilayani Babati Mkoani Manyara wameaswa kuacha tabia ya kujitibu nyumbani pindi wanapojihisi kuumwa na badala yake kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kwa ushauri na vipimo zaidi. Wito huo umetolewa Wilayani Babati Mkoani Manyara na Mfamasia Mwandamizi kutoka Baraza la Famasi Tanzania Bi. Anna Tema wakati akitoa Elimu ya Afya kuhusu matumizi sahihi ya dawa kwa Wananchi waliohudhuria kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Mji wa Babati ikiwa ni mwendelezo wa Baraza la Famasi wa utoaji wa Elimu ya Afya kwa jamii kwa kushirikiana na Sehemu ya Elimu ya Afya kwa umma. Kwa upande wake Erick Bokango kutoka Baraza hilo amesema ni muhimu kufuata maelekezo sahihi ya wataalamu wa afya katika kulinda afya bora. Simon Gadiye ni Mfamasia wa Halmashauri ya Mji wa Babati ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kununua holela dawa kwa maduka yasiyosajiliwa na Baraza la Famasi Tanzania
#Repost @itvtz #HABARI: Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Majanga, kutoka Wizara ya Afya, Dokta Erasto Silvanus, amesema taarifa ya ongezeko la visa vya UVIKO-19 kutoka mwezi Februari hadi Aprili ni ishara ya jamii kujua kuwa ugonjwa huo upo, ingawa si tishio kama mlipuko wa kwanza mwaka 2020 huku akisisitiza uhitaji wa jamii kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza maambukizi yake. Dkt.Silvanus amezungumza na #ITVDIGITAL baada ya tamko kwa umma lililotolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe, juu ya tahadhari ya magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa na magonjwa yanayoenezwa na mbu.
back to up