Wananchi Mkoani Songwe wametakiwa kuwa mabalozi wa kutoa elimu ya kupinga na kukemea uvumi wa unaoenea ambao umeleta madhara ya kuwa mwanaume akiguswa nyeti zinapotea jambo lililosababisha mauaji ya aliyekuwa mlinzi wa Zelezeta viwandani Aron Mgogo mkazi wa Mlowo eneo la Tazara Wilayani Mbozi ambae aliuwawa kwa kupigwa na wananchi.
Majonzi haya ni matokeo ya wananchi kuendelea kujichukulia sheria mkononi na tabia hii imekuwa ikiendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali Mkoani hapa mpaka sasa idadi ya waliofariki ni watu 6 akiwemo Aron Mgogo aliuwawa na wananchi kwa kupigwa baada ya tuhuma ya kudai kumgusa mtu na sehemu zake za siri kupotea jambo limeacha kovu na maumivu katika familia hii.
#CloudsDigitalUpdates.
#HABARI Abiria zaidi ya 80 waliotoka Mlowo wilaya ya Mbozi kuelekea Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe, wamekwama kuendelea na Safari katika eneo la Mnkonko wilayani Momba kwa sababu za ubovu wa barabara.
Gari tatu zimekwama katika eneo hilo kwasababu barabara katika eneo hilo haina kifusi hali inayosababisha gari kuteleza na kutitia chini.
Aina ya gari zilizokwama ni Bus lenye namba za usajiri T 612 DFU kampuni ya KP express, T 792 AZR kampuni ya Mpare classic na Fuso fighter lenye namba za Usajiri T 601 DVS lilitotokea kamsamba kuelekea Mbozi.#EastAfricaTV
Vwawa Mlowo inavyotekeleza malengo ya serikali, huduma ya maji Kwa jamii.
ABIRIA WAKWAMA KUENDELEA NA SAFARI KISA UBOVU WA BARABARA MLOWO-KAMSAMBA.
abiria zaidi ya 80 waliotoka Mlowo wilaya ya Mbozi kuelekea Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe wamekwama kuendelea na Safari katika eneo la Mnkonko wilayani Momba kwa sababu za ubovu wa barabara.
gari tatu zimekwama katika eneo hili kwasababu barabara katika eneo hili ni haina kifusi na inateleza hivyo kusababisha gari kutitia chini.
📌📌MAKONDA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MLOWO WILAYANI MBOZI - SONGWE
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda akizungumza na Wananchi wa Mlowo katika Wilaya ya Mbozi.
Makonda akiwa hapo, amesikiliza kero, changamoto na malalamiko mbalimbali ya Wananchi wa Mlowo na kuzitolea mwanga na njia sahihi ya utatuzi wa hapo kwa hapo katika kuhakikisha CCM inawasimamia Viongozi na Watumishi wa Serikali kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia utu na misingi ya haki.
📍Mbozi - Songwe
🗓️ 7 Februari, 2024
#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imekamilisha matengenezo ya barabara ya Mlowo-Mpito-Isansa yenye urefu wa Km 13.4 kwa kiwango cha changarawe wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Katika hali ya ujasiri, kijana mmoja amejitokeza kupitia video fupi akimuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuangazia hali mbaya ya barabara kuanzia Igawo, Mlowo hadi Tunduma.
Kijana huyo ameeleza kuwa ubovu wa barabara hiyo wenye mashimo mengi na ufinyu, umekuwa chanzo kikubwa cha ajali ambazo mara nyingi hukimbiliwa kuitwa "uzembe wa dereva" wakati changamoto halisi ni miundombinu.
Ametoa wito kwa Waziri Mkuu na Waziri wa Uchukuzi kuhakikisha mwaka huu haupiti bila marekebisho kufanyika ili kuokoa maisha ya Watanzania na mali zao zinazopita katika ukanda huo muhimu wa kibiashara.
Usisahau ku follow ukurasa wetu wa @Bahama_media kwa habari na uchambuzi zaidi wa matukio ya kijamii.
#BahamaMedia #SautiYako
WATOTO WAWILI WA MIAKA 3 WAKUTWA MTONI WAKIWA WAMEFARIKI
Watoto wawili wenye Umri wa Miaka 3 Desi Mwasenga na Mariam Lyala wote wakiwa jinsia kike wamekufa maji baada ya kusombwa wakiwa wanaogelea katika Mto Mlowo ambao upo kata ya Mahenje Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe .
Jeshi la Polisi Kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamshina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watoto hao walipotea Januari 31 Majira ya Saa nane Mchana.
Wasafimedia imezungumza na mmoja wa wazazi wa watoto walifariki pamoja na wananchi wameeleza kusikitishwa kwao kutokana na tukio hilo ambapo aligundua mtoto wake kutokuwepo mazingira ya nyumbani Januari31 muda wa Saa nane Mchana baada ya yeye kutoka shambani ndipo alipochukua hatua ya kuwajulisha majirani na kuanza kuwatafuta bila mafanikio.
@iamhaika1
#WasafiDigital
"WANAKWAYA INASIKITISHA MANATUIMBIA TUKAKOMUNIKE, HALAFU NYIE HAMKOMUNIKI"
-Video ni Mhashamu Godfrey Jackson Mwasekaga, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu Dominika ya 21 ya Mwaka wa C wa Kanisa katika Kigango cha Mtakatifu Monica, Parokia ya Mtakatifu Peter Clavery - Mlowo, Jimboni humo.
.
.
www.radiomaria.co.tz
#gusamoyo2025
Serikali imeanza rasmi utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Tunduma, Vwawa na Mlowo kutoka Mto Momba, unaotarajiwa kumaliza kabisa tatizo la maji katika maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Elias Mwandobo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabir Makame, amewakabidhi wakandarasi kazi ya ujenzi wa mradi huo unaosimamiwa na TUNUMAMWASSA.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mwandobo amesema wakandarasi wameanza kazi mara moja katika maeneo mbalimbali kwa wakati mmoja ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya miezi 18 iliyopangwa.
Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 119 tayari umeanza kwa kulipwa kiasi cha awali cha shilingi bilioni 4 kati ya bilioni 14 za malipo ya kuanzia.
Kwa sasa upatikanaji wa maji Tunduma ni asilimia 45 pekee, lakini kukamilika kwa mradi huu kunatarajiwa kufikisha huduma ya maji kwa asilimia 100 na kumaliza kabisa kero ya maji kwa wananchi.
@simkondalaudence
#2Digital
#TBC2UPDATES
#TBC2YAKIJANJAZAIDI
“SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA YA MLOWO – KAMSAMBA MKOANI SONGWE’’
Hayo yameelezwa hivi karibuni na Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mha. Suleiman Bishanga alipozungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa.
#mlowo
Namna ya kuishi na mama mkwe wako