#HABARI: Serikali imesisitiza kuwa huduma za afya kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano zinaendelea kutolewa bure kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007, na kwamba vitendo vya kutoza gharama kwa makundi hayo haviruhusiwi.
Hayo yameelezwa leo Februari 3, 2026 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, wakati akijibu swali la Mhe. Bakari Bakari Shingo (Ukonga), aliyeuliza iwapo Serikali ina mpango wa kukemea vitendo vya kutoza gharama za matibabu kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Akijibu swali hilo, Dkt. Samizi amesema Sera ya Afya ya mwaka 2007 inaelekeza wazi utoaji wa huduma za matibabu bure kwa makundi maalum yakiwemo akina mama wajawazito, watoto chini ya umri wa miaka mitano pamoja na wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wasiokuwa na uwezo.
Ameongeza kuwa Serikali imeshatangaza rasmi kuanza utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote (UHI) awamu ya kwanza, itakayohusisha makundi maalum ya wananchi yakiwemo watoto, wajawazito, watu wenye ulemavu na wazee wasio na uwezo, ambapo gharama za bima kwa makundi hayo zitagharamiwa na Serikali.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
Serikali imesisitiza kuwa maboresho ya mifumo katika sekta ya afya hayaishii kwenye kuandika sera na taratibu pekee, bali huanza kuonekana mapema katika uhalisia wa utoaji huduma kwa wananchi. Waziri wa Afya, Mchengerwa, amesema dalili za kwanza za ubadhirifu hujitokeza vituoni kwenye madai, foleni, risiti pamoja na malalamiko ya wananchi, akibainisha kuwa hapo ndipo uandishi wa habari za kiuchunguzi unapokuwa nguzo muhimu ya kulinda mfumo wa afya.
Akizungumzia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Waziri Mchengerwa amesema hatakubali kwa namna yoyote mfuko huo kuchezewa chini ya uongozi wake. Amesisitiza kuwa yuko tayari kukosolewa au kuchukiwa ilimradi alinde uadilifu wa NHIF, akionya kuwa vitendo vya ulaghai, wizi na utapeli vikiruhusiwa vinaweza kusababisha mfumo mzima wa afya kuyumba.
Waziri huyo ameeleza kuwa NHIF ikipoteza uaminifu wa wananchi, athari zake haziishii kwenye mfuko huo pekee bali huathiri uimara wa mifumo ya taifa kwa ujumla. Amesisitiza kuwa hayuko tayari kuona mifumo ya afya ikiyumba wakati yeye akiwa msimamizi mkuu wa sekta hiyo, akisisitiza kuwa kuchezea uaminifu wa NHIF ni kuchezea uthabiti wa huduma za afya kwa Watanzania.
Katika hatua nyingine, Waziri Mchengerwa amewataka waandishi wa habari, hususan wa habari za kiuchunguzi katika sekta ya afya, kushirikiana na serikali kwa kubainisha mapema vitendo viovu. Amesema serikali imeazimia kuboresha sekta ya afya bila sababu yoyote ya kushindwa, huku ikiahidi kujenga ulinzi madhubuti wa mifumo na kuwalinda wote watakaofichua uoovu, akisisitiza kuwa wizara itasimama kwenye nguzo tatu zitakazotumika kama mwongozo wa utekelezaji na uwajibikaji.
#gmnet_tz Tunakuletea habari kwa uwazi na usahihi kwa manufaa ya jamii.
SERIKALI YAPANUA HUDUMA ZA CHANJO, TIBA NA ELIMU YA HOMA YA INI
Na WAF, Dodoma
Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Ini kupitia utoaji wa chanjo bure kwa watoto pamoja na chanjo kwa watu wazima, ikiwa ni hatua ya kuzuia maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Naomy Dungan Mwaipopo (Viti Maalum) leo Januari 29, 2026 Bungeni jijini Dodoma, aliyeuliza mkakati wa serikali wa kuhakikisha ugonjwa wa homa ya ini unatokomezwa.
Aidha, Dkt. Samizi amesema Serikali imeanzisha huduma za tiba ya magonjwa ya ini, ambapo kuanzia Desemba 2025 hospitali zote za mikoa, kanda na taifa zimeanza kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa Homa ya Ini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo karibu na maeneo yao.
Katika hatua nyingine, amesema Serikali imeeleza kuwa itaongeza juhudi za usimamizi shirikishi katika mikoa inayoongoza kitaifa kwa viwango vya maambukizi ya ugonjwa wa Homa ya Ini, kwa lengo la kudhibiti na hatimaye kutokomeza ugonjwa huo katika mikoa iliyoathirika zaidi.
Pia, Dkt. Samizi ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupima ugonjwa wa Homa ya Ini mapema ili kuchukua tahadhari stahiki, kujikinga dhidi ya maambukizi, pamoja na kupata matibabu kwa wakati.
Aidha, huduma hizo jumuishi zimeendelea kuboreshwa kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Zinaa na Homa ya Ini (NASHCoP), ambapo wahudumu wa afya wamepatiwa miongozo na maelekezo ya kitaalamu ili kuwawezesha kutoa huduma bora na salama kwa wananchi.
BIMA YA AFYA KWA WOTE YALENGA MAKUNDI MAALUM YA KIMKAKATI
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema mpango wa Bima ya Afya kwa Wote umejikita kuyafikia makundi maalum ya kimkakati ikiwemo wafugaji, wakulima, wasanii, waendesha bodaboda na wachimbaji wadogo.
Waziri Mchengerwa ameyasema jana Februari 2, 2026, wakati akizungumza katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Waziri Mchengerwa amesema dhamira kuu ya Serikali ni kumfuata mwananchi popote alipo kwa kutumia lugha na njia zinazoeleweka kwa kundi husika, ili kuongeza uelewa kuhusu Bima ya Afya kwa Wote na kuhamasisha usajili wa wananchi wengi zaidi.
Kwa upande mwingine, amesema mpango huo pia utazingatia makundi yasiyo na uwezo, yakiwemo wazee, wajawazito na watu wenye ulemavu, ambao wataendelea kupatiwa huduma za matibabu bila malipo kwa mujibu wa utaratibu wa Serikali.
Aidha, ameeleza kuwa katika kuhakikisha taarifa za Bima ya Afya kwa Wote zinamfikia kila mwananchi, Serikali itaingiza ajenda ya bima katika shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi, pamoja na kutumia sanaa, wasanii na teknolojia ya habari katika kampeni za uhamasishaji.
Wizara ya Afya Tanzania National Health Insurance Fund
Ndimi Muhidini Dua Alaiyka 0783 54 54 30
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewataka viongozi katika ngazi ya vitongoji na vijiji mkoani humo kutumia vizuri majukwaa ya mikutano ya hadhara kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kuchangamkia zoezi la kujiandikisha na kujiunga na Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, akisisitiza kuwa mpango huo utasaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa gharama za matibabu wakati wote wanapohitaji huduma za afya.
Ametoa maagizo hayo wakati akikagua miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa.
Kheri James amesema Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ni nguzo muhimu ya ustawi wa jamii kwani unalenga kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za afya kwa wakati, kwa gharama nafuu na bila vikwazo, hivyo kuchangia kupunguza vifo vinavyotokana na kuchelewa kupata matibabu.
@canalmathias
#WazoHuruMedia #KwaMawazoEndelevu
NAIBU WAZIRI KIHENZILE AZINDUA KITUO CHA AFYA MAKUNGU MUFINDI
Naibu Waziri wa Uchukuzi (MB), @david_kihenzile amezindua Kituo cha Afya Makungu kilichopo Kata ya Makungu, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambacho kinatarajiwa kuhudumia wananchi wa kata hiyo pamoja na kata za jirani zikiwemo za mkoa wa Njombe huku kikigharimu zaidi ya shilingi milioni 500.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kihenzile ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, amesema kukamilika na kuanza kwa utoaji huduma katika kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Amesema serikali imeendelea kuimarisha miundombinu ya afya ili kupunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu, huku akisisitiza kuwa kituo hicho kitasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za mama na mtoto, matibabu ya dharura na huduma nyingine muhimu za afya.
Wananchi wa Makungu na maeneo ya jirani wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo wakisema itarahisisha upatikanaji wa matibabu na kupunguza gharama za usafiri waliokuwa wakitumia kufuata huduma katika vituo vya mbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Ndugu Juma Hokororo, amewataka madiwani wa kata zote wilayani humo kuhakikisha wanawafikishia wananchi taarifa sahihi kuhusu huduma ya Bima ya Afya kwa Wote inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani, Hokororo amesema kuwa bima hiyo ni fursa muhimu kwa wananchi kupata huduma bora za afya kwa gharama nafuu, hivyo ni wajibu wa madiwani kushirikiana na viongozi wa ngazi za chini kuwahamasisha wananchi kujiunga na mpango huo.
Ameeleza kuwa Bima ya Afya kwa Wote inapatikana kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini (150,000) kwa mwaka, ambapo inahudumia familia yenye jumla ya watu sita wakiwemo baba, mama na wategemezi wanne ambao ni ndugu wa damu.
“Hii ni bima rafiki na yenye manufaa makubwa kwa wananchi wetu, hivyo madiwani mna jukumu la kuhakikisha taarifa hii inawafikia wananchi ili waweze kujiunga na kupata huduma za afya bila changamoto,” amesema Hokororo.
Kwa upande wake, baadhi ya madiwani wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya na kuahidi kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza uelewa na ushiriki wao katika mpango huo wa bima ya afya kwa wote.
#fariemedia
#tupositekukuhabarisha
#26tabasamulakishua
HAKUNA MAITI INAYOZUILIWA KATIKA VITUO VYA AFYA, HOSPITALI
Na WAF - Dar es Salaam
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ameweka wazi, kupitia Serikali hii chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa hakuna maiti inayozuiliwa katika vituo vyote vya afya pamoja na hospitali.
Waziri Mchengerwa amesema hayo leo Februari 02, 2026 kwenye kikao kazi na Wahariri wa Vyombo vya Habari pamoja na Waandishi wa Habari wa Redio pamoja na mitandao ya kijamii wa nchi nzima.
"Nichukue fursa hii kusema kwamba, tunapoelekea kuhitimisha siku 100 za Daktari Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani, hakuna kituo wala Hospitali wanaozui maiti," amesisitiza Waziri Mchengerwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amehoji upungufu wa dawa katika hospitali za mkoani Manyara, akiuliza kwa nini dawa zinakosekana katika vituo vya umma huku zikipatikana katika maduka binafsi ya dawa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Manyara, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa dawa katika hospitali za Serikali unaimarishwa kwa manufaa ya wananchi.
Endelea kuwa karibu na mitandao yetu
Zaidi ya wananchi 7,000 kutoka makundi maalumu wakiwemo wazee, watu wenye ulemavu na kaya zisizojiweza katika Tarafa ya Isimani, Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, wamenufaika katika awamu ya kwanza ya mpango wa Serikali wa Bima ya Afya kwa Wote baada ya kupatiwa kadi za bima ya afya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa kadi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Afisa Tarafa wa Isimani, Bw. Benito Kayugwa, amesema Serikali imeanzisha mpango wa Bima ya Afya kwa Wote kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote, hususan wa makundi maalumu, wanapata huduma za matibabu bila kukumbwa na vikwazo vya kifedha.
Baadhi ya wanufaika wa mpango huo wamesema kabla ya kuingizwa kwenye utaratibu huo walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa za kiafya, ikiwemo kushindwa kumudu gharama za matibabu, jambo lililosababisha kuchelewa au kukosa kabisa huduma muhimu walipokuwa wanaugua.
Naibu Waziri David Kihenzile Azindua Kituo cha Afya Makungu chenye Thamani ya Shilingi Milioni 500
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amezindua Kituo cha Afya cha Kata ya Makungu kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, mradi uliogharimu shilingi milioni 500.
Uzinduzi wa kituo hicho unatajwa kuwa suluhisho la kudumu kwa zaidi ya wananchi 17,000 wa Kata ya Makungu na maeneo ya jirani ambao hapo awali walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya, hususan huduma za mama na mtoto. Kupatikana kwa huduma hizo karibu kutapunguza gharama na hatari zilizokuwa zikiwakabili wananchi, hasa wajawazito.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kihenzile alisema kukamilika kwa kituo hicho ni hatua muhimu katika kuboresha sekta ya afya katika Wilaya ya Mufindi. Uzinduzi huo umefanyika katika ziara yake ya siku nne jimboni kwake, yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Kuhusu maboresho yaliyotekelezwa, amesema changamoto ya mochwari iliyokuwa ikiwasumbua wananchi imepatiwa ufumbuzi baada ya ujenzi wake kukamilika kwa asilimia 100. Kukamilika huko kutawaondolea wananchi adha ya kusafirisha miili umbali mrefu pamoja na gharama za usafiri, kwani sasa miili ya wapendwa wao itahifadhiwa kwa heshima katika eneo lao.
Aidha, alibainisha kuwa bado kuna maeneo yanayohitaji kukamilishwa, ikiwemo jengo la maabara na upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba. Amesema vifaa vilivyopokelewa vitafungwa na kuanza kutumika mara moja. Pia, suala la upatikanaji wa gari la wagonjwa (ambulance) limewasilishwa serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Kukamilika kwa Kituo cha Afya cha Kata ya Makungu ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya afya na kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi.