Instagram story viewer> @aloycesagara_> Posts
3K
followers
3946
following
Philippians. 4:13 II Journalist II BA in Mass Communication (SAUT-CLASS OF 2024) II Founder @alomediatz
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
It does not matter how slowly you go, as long as you do not stop.

Slide 2.

#wekeepgrinding by @aloycesagara_
0
a year ago
Download
MEMORIES by @aloycesagara_
0
a year ago
Download
Happy SIMBA DAY Mr.Sagara

Nakumbuka enzi hizo kukiwa na Matangazo ya Mpira Radio Tanzania ulikuwa unanunua Battery Mpya kabisa maalum kwa ajili ya kusikiliza Mpira hapo Juma Nkamia na Charles Hilary.

Nimeanza kuupenda mpira kwa kuvutiwa na picha za Wachezaji MagazetiniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ. Umehusika kwa asilimia kubwa mno kufanya nizame zaidi kwenye dimbwi la Soka.

It's SIMBA DAY Daddy 🦁 by @aloycesagara_
7
a year ago
Download
"𝐓𝐔𝐓𝐀𝐖𝐀𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 π˜π€ππ†π€"

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Ismail Mgunda ameweka wazi kuwa kutokana na kile kinachoendelea mazoezini ana asilimia 100% kuwa watapata ushindi kwenye mchezo wao wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga.

"Mechi za Dabi nimekuwa nikiziangalia tu. Kwa hiyo hii itakuwa ni mara ya kwanza kuwepo kwenye mchezo au kuwepo kwenye Dabi. Naamini kwa ninachokiona na tunachokifanya mazoezini, encouragement jinsi ilivyo na timu ilivyo, mchezo huo tutashinda.Mimi nina asilimia 100% tunashinda."

-Ismail Mgunda (Kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga Oktoba 10,2026).

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
14 hours ago
Download
πŒπ„π’π’πˆ π€πŠπ€π‘πˆππˆπ€ πŠπ”π•π”ππ‰π€ π‘π„πŠπŽπƒπˆ π‡πˆπˆ....

Nyota wa klabu ya Inter Miami Lionel Messi anakaribia kuvunja rekodi ya Marceilnho Carloca ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ya "Free Kick".

Messi hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao (76) kwa njia ya "Free Kick" huku akibakiza mabao mawili pekee ili kufikia rekodi inayoshikiliwa na Marceilnho mwenye mabao (78).

NB: Je Messi atafanikiwa kuvunja rekodi hiyo na kuweka rekodi mpya?

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
14 hours ago
Download
π“π€π€π‘πˆπ…π€ πŒππ€π˜π€ πŠπ–π€ π˜π€ππ†π€, π˜π€ππ€π“π€ πŒπ’πˆππ€ πŒπ™πˆπ“πŽ....

Shabiki maarufu wa Klabu ya Yanga, Mzee Mpili, amefariki dunia usiku huu huko Ikwiriri, Rufiji.

Mzee Mpili alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na matatizo ya mgongo, kiuno na magonjwa ya uzee.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Klabu ya Yanga SC imeeleza kuwa mwanachama wake, Haji Omari Ramadhani Mpili, amefariki dunia usiku wa Septemba 27, 2026, katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho, majira ya saa 10:00 jioni, katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
17 hours ago
Download
"ππˆπ‹π€ 𝐇𝐀𝐍𝐒 π…π‹πˆπ‚πŠ ππˆπ’πˆππ†π„πŠπ”π–π€ ππ€π‘π‚π„π‹πŽππ€"

Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona, Raphinha, amefunguka ukweli wa mambo yaliyomfanya asiondoke klabuni hapo huku akimtaja kocha Hansi Flick kama mtu aliyebadilisha maisha yake.

Raphinha amefichua kuwa mnamo mwaka 2024, alikuwa ameshakata tamaa na maisha ya Camp Nou na alikuwa tayari kufunganya virago vyake kuondoka, lakini ujio wa Flick ulibadilisha kila kitu ndani ya dakika chache tu.

"Bila Hansi Flick, nisingekuwa Barcelona tena. Alibadilisha mtazamo wangu (mentality), ki-klabu na kama binadamu pia. Kila siku nitasema hivi: Hansi Flick ndiye kocha aliyebadilisha maisha yangu."

-Raphinha (Mchezaji wa klabu ya Barcelona akielezea vile Kocha Hans Flick alimsaidia).

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
4 days ago
Download
𝐉𝐄 𝐍𝐈 πŒπ‚π‡π„π™π€π‰πˆ π†π€ππˆ π‡π”π˜πŽ?

Kwenye historia ya Soka la Tanzania kuna nyota mbalimbali wakigeni ambao wamecheza nchini Tanzania na kufanya mambo makubwa na hadi leo bado majina yao yanaimbwa kwa ukubwa.

Tangu enzi za kina Nonda Shaban, Haruna Niyonzima, Kipre Tchetche, Emmanuel Okwi,Fiston Mayele na hadi sasa Clatous Chama JR bado anatamba.

Je ni mchezaji gani wakigeni ambaye unadhani ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kucheza kwenye Ligi yetu?

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
1
4 days ago
Download
𝐍𝐈 π€π‘π€π‰πˆπ†π€ 𝐓𝐄𝐍𝐀 π€π…π‘πˆπŠπ€, π€π€πŒπˆππˆπ–π€ 𝐍𝐀 𝐂𝐀𝐅 

Mwamuzi wa kati (Referee) kutokea nchini Tanzania Ahmed Ally Arajiga amechaguliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuchezesha mchezo wa Kundi (H) kati ya Tunisia na Botswana kuwania nafasi ya kufuzu michuano ya AFCON 2027.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 29.

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
6 days ago
Download
π‘π”π’π‡πˆππ„ 𝐃𝐄 π‘π„π”π‚πŠ π€π“πŽπ€ ππ„ππŽ πŠπ”π‡π”π’π” π’πˆπŒππ€...

Beki wa klabu ya Simba raia wa Afrika Kusini Rushine De Reuck, kupitia Podcast ya @fatemagdewji amefunguka kuwa alikuja Tanzania akiwa na hofu kubwa baada ya kukosa nafasi ya kucheza kwa muda mrefu nchini Afrika Kusini kiasi cha kuanza kujishuku kama bado anaweza kucheza mpira wa kulipwa.

Rushine amesema mtu pekee aliyemjua kabla ya kuja alikuwa Kocha Fadlu Davids, lakini licha ya hofu hiyo, amesema Tanzania imempa kitu alichokuwa amekipoteza, mapenzi na furaha ya kucheza mpira tena.

Nyota huyo amesema mazingira mazuri ya Simba na kumwamini kwa kocha wake ndio vimefanya arudishe kujiamini kwake na kuwa na furaha kama binadamu tena.

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
6 days ago
Download
π–π€π’π‡πˆππƒπˆ 𝐖𝐀 ππ€π‹π‹πŽπ 𝐃'πŽπ‘ πŠπ”π“πŽπŠπ€ 𝐁𝐀𝐑𝐂𝐀 𝐍𝐀 πŒπ€πƒπ‘πˆπƒ

Hadi sasa vilabu vya FC Barcelona na Real Madrid vimelingana kwa idadi ya kutoa wachezaji walioshinda Tuzo ya Ballon D'or mara nyingi kila timu ikiwa imetwaa tuzo hiyo mara (12).

Kwa upande wa FC Barcelona kinara ni Lionel Messi mwenye Tuzo (6) akifuatiwa na Johan Cruyff mwenye tuzo (2) huku upande wa Real Madrid kinara ni Cristiano Ronaldo mwenye tuzo (4) akifuatiwa na Alfredo Di Stefano mwenye tuzo (2).

Hii hapa orodha kamili ya wachezaji wa Barcelona na Real Madrid walioshinda Tuzo ya Ballon D'or:-

(Barcelona)
Lionel Messi - Mara (6)
Johan Cruyff - Mara (2)
Ronaldinho - Mara (1)
Hristo Stoichkov - Mara (1)
Luis Suárez - Mara (1)
Rivaldo - Mara (1)

(Real Madrid)
Cristiano Ronaldo - Mara (4)
Alfredo Di Stefano - Mara (2)
Karim Benzema - Mara (1)
Fabio Cannavaro - Mara (1)
Ronaldo Nazario - Mara (1)
Luis Figo - Mara (1)
Raymond Kopa - Mara (1)
Luka Modric - Mara (1)

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
7 days ago
Download
π‚π„πƒπ‘πˆπ‚ πŠπ€π™π„ π€π“π€πŒππ”π‹πˆπ’π‡π–π€ πŠπ€π†π„π‘π€ 𝐒𝐔𝐆𝐀𝐑 

Klabu ya Kagera Sugar imemtambulisha raia wa Burundi, Cedric Kaze, kuwa Kocha Mkuu mpya wa kikosi hicho, akichukua nafasi ya Juma Kaseja aliyeachana na klabu hiyo baada ya mwenendo wa matokeo kutoridhisha katika michezo sita ya mwanzo ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27.

Kaze anarejea katika soka la Tanzania akiwa na uzoefu wa kuifundisha Yanga SC, ambapo aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo kabla ya kuendelea na safari yake ya ukocha nje ya Tanzania.

Cc: @aloycesagara_ by @aloycesagara_
0
7 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up