Instagram story viewer> @crdbbankfoundation> Posts
34.6K
followers
13
following
Dira yetu ni kuboresha maisha ya watu wetu na kukuza uchumi.
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Every entrepreneur has a story. Every opportunity creates impact. 

Through the INCLU-CITIES SASA Project, funded by @euintanzania and implemented by ENABEL and CRDB Bank Foundation, women and youth entrepreneurs are building stronger businesses and transforming their communities. 

This week, meet the Faces of Impact behind these inspiring stories. 

#FacesOfImpact #INCLUCITIESSASA by @crdbbankfoundation
8
21 days ago
Download
International R&B superstar Trey Songz takes the stage, bringing his signature sound and incredible live performance to Tanzania. 🎤✨

From the lights and the crowd to every beat and every moment, tonight is all about celebrating great music and creating memories that will last long after the final song. 🥂🔥

#crdbfoundation #imbejusautimoja #crdbmarathon #kasiisambazayotabasamu #concertforacause taken in Dar es Salaam, Tanzania by @crdbbankfoundation
43
2 months ago
Download
This is what 2026 looked like. 🏃🏾‍♂️🔥

The streets came alive. The energy was unmatched. And thousands moved together with one purpose.

CRDB Bank International Marathon 2026🏅✨

#crdbmarathon2026 #CRDBMarathon #kasiisambazayotabasamu #daressalaa #hugodomingoevents taken in Dar es Salaam, Tanzania by @crdbbankfoundation
34
2 months ago
Download
Leo Benki yetu inashiriki Kongamano la Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Forum 2026) linalofanyika jijini London, Uingereza, kwa kushirikiana na Invest Africa.

Ushiriki wetu unaendelea kudhihirisha dhamira ya kuwa mshirika wa kimkakati wa kifedha katika kuvutia mitaji, kufungua fursa za uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

#CRDBBank #CRDBBankFoundation 
#TanzaniaInvestmentForum2026 taken in London, United Kingdom by @crdbbankfoundation
12
4 days ago
Download
Mkurugenzi wa @crdbbankfoundation @tully_esther_mwambapa katika wiki ya wateja ameishukuru CMG kwa kuwa pamoja kwa miaka yote na kwenye project nyingi za kufungulia Dunia. by @crdbbankfoundation
11
7 days ago
Download
CRDB Bank Foundation yashiriki juhudi za kimataifa za kuongeza upatikanaji wa mitaji vijijini.

CRDB Bank Foundation imeshiriki mkutano unaojaili Ufadhili Mseto wa Miradi yaani  Blended Finance Working Group (BFWG) ulioandaliwa na FAO jijini Rome, Italia, ukilenga kujadili namna ya kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa wakulima, wajasiriamali na biashara za vijijini.

Kupitia mkutano huo, Foundation imeshirikisha uzoefu wa Tanzania na kusisitiza umuhimu wa blended finance, ushirikiano wa kimkakati na mifumo bunifu ya ufadhili katika kuziba pengo la upatikanaji wa fedha kwa jamii ambazo hazijahudumiwa ipasavyo na mifumo rasmi ya kifedha.

Kupitia programu kama iMBEJU Kilimo na iMBEJU Nuru, Foundation inaendelea kuunganisha rasilimali, mitaji na fursa ili kuchochea ujasiriamali, ajira, uhakika wa chakula na ukuaji wa uchumi jumuishi na endelevu vijijini. by @crdbbankfoundation
7
8 days ago
Download
MAKAMU WA RAIS AZINDUA USHIRIKIANO WA BENKI YA CRDB NA TANESCO UUNGANISHAJI UMEME NAFUU KWA WANANCHI

Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amezindua rasmi ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unaolenga kuongeza fursa kwa wananchi kuunganishiwa umeme na kunufaika zaidi na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya nishati.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Ndejembi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuhakikisha huduma za msingi zinawafikia wananchi na kuchochea shughuli za kiuchumi hususan kwa kaya na wajasiriamali wanaohitaji umeme.

Kupitia ushirikiano huu, CRDB Bank Foundation itasimamia utekelezaji wake chini ya iMbeju Nuru, mpango unaolenga kuwawezesha wananchi kulipia gharama za awali kwa ruzuku au mkopo nafuu kutoka Benki ya CRDB hivyo kuwawezesha wananchi kutumia huduma hiyo kama kichocheo cha fursa na maendeleo ya kiuchumi.

Uzinduzi huu unaweka msingi wa hatua mpya katika safari ya kuhakikisha umeme unafika ndani ya kaya, kwenye biashara na shughuli za uzalishaji za wananchi.

Kutoka kwenye miundombinu hadi kwenye fursa. Kutoka kwenye mwanga hadi kwenye maendeleo. Hii ndiyo iMbeju Nuru.

#CRDBBank
#CRDBBankFoundation
#iMbejuNuru
#TANESCO by @crdbbankfoundation
6
10 days ago
Download
Mgeni Rasmi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuwawezesha wananchi kuunganishiwa umeme kwa gharama nafuu kupitia Programu ya iMbeju Nuru inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation, amesema ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi utaharakisha maendeleo ya wananchi na taifa.

Makubaliano hayo yalisainiwa na Mkurugenzi wetu Mtendaji, Dkt Abdulmajid Mussa Nsekela  na  Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange umeweka msingi wa ushirikiano wa kimkakati katika utekelezaji wa mpango kusambaza kuunganisha umeme kwa zaidi ya kaya 500,000 mpaka ifikapo mwaka 2030.

Kupitia ushirikiano huu, CRDB Bank Foundation itasimamia utekelezaji unaolenga kuondoa vikwazo vya gharama za awali za uunganishaji umeme na kuongeza fursa za wananchi kutumia nishati hiyo katika shughuli za kiuchumi.

#CRDBBank
#CRDBBankFoundation
#iMbejuNuru
#TANESCO by @crdbbankfoundation
4
10 days ago
Download
Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Juma Zuberi Homera amepongeza ushirikiano wa Benki yetu ya CRDB kupitia CRDB Bank Foundation na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akieleza kuwa ni sehemu ya juhudi muhimu za kuendeleza upatikanaji wa nishati na kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na miundombinu iliyowekezwa na Serikali.

Mheshimiwa Homera amepongeza ubunifu unaofanywa na Benki yetu ya CRDB katika kuibua suluhisho la kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi katika jitihada za kawaunganishia umeme, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kuleta matokeo yenye manufaa kwa Watanzania.

Utekelezaji wa mkataba huu kupitia iMbeju Nuru – programu inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation inaonyesha hatua muhimu iliyofikiwa katika kuunganisha uwekezaji wa Serikali kwenye miundombinu ya umeme ili kukidhi mahitaji ya wananchi hususan katika kuwafikishia umeme majumbani mwao pamoja na kwenye shughuli zao za kiuchumi.

#CRDBBank
#CRDBBankFoundation
#iMbejuNuru
#TANESCO by @crdbbankfoundation
0
10 days ago
Download
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Profesa Neema Munisi Mori, amesema wataendelea kuiwezesha menejimenti kushiriki utekelezaji wa miradi inayowagusa wananchi ili kuhakikisha Benki inaendelea kutimiza dhamira yake ya kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.

Amesema hayo alipozungumza katika hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Benki ya CRDB na TANESCO, akisisitiza kuwa Bodi inaendelea kusimamia utekelezaji wa mkakati wa Benki unaolenga kutumia uwezo wa taasisi kushirikiana na Serikali na wadau wengine kutatua changamoto za wananchi.

Ushirikiano huu unaotekelezwa na Benki ya CRDB kupitia CRDB Bank Foundation chini ya mpango wa iMbeju Nuru, amesema ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha dhamira ya Benki ya kuchochea maendeleo inafika moja kwa moja kwa jamii.

#CRDBBank
#CRDBBankFoundation
#iMbejuNuru
#TANESCO by @crdbbankfoundation
8
10 days ago
Download
Akitoa salamu za Benki ya CRDB katika tukio la utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Benki ya CRDB na TANESCO, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela, amesema ushirikiano huo ni hatua muhimu ya kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanywa katika miundombinu ya umeme unatafsiriwa kuwa huduma halisi kwa wananchi.

Amesema utekelezaji wa makubaliano hayo utasimamiwa na CRDB Bank Foundation kupitia programu maalum ya iMbeju Nuru, inayolenga kuwawezesha wananchi kupata huduma ya kuunganishiwa umeme na kutumia nishati hiyo kama kichocheo cha shughuli za kiuchumi na maendeleo ya kaya.

Kupitia iMbeju Nuru, CRDB Bank Foundation itashirikiana na TANESCO katika kuifikia jamii, kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha na kutoa elimu ya fedha na ujasiriamali, ili mwananchi asiishie kupata umeme pekee, bali aweze kuugeuza kuwa fursa ya kuongeza kipato na uzalishaji.

Hii ndiyo iMbeju Nuru mbegu ya mwangaza inayolenga kuleta fursa, kuchochea uzalishaji na kuboresha maisha ya Watanzania.

#CRDBBank
#CRDBBankFoundation
#iMbejuNuru
#TANESCO by @crdbbankfoundation
6
10 days ago
Download
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert John Chalamila ametoa salamu za Mkoa katika tukio hili muhimu, akipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa na kuendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

Ameipongeza Benki ya CRDB kupitia CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na TANESCO katika mradi mpya unaolenga kurahisisha uwezo wa wananchi kupata huduma ya umeme jambo litakalo boresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya Taifa.

#CRDBBank
#CRDBBankFoundation
#TANESCO by @crdbbankfoundation
4
10 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up