Instagram story viewer> @dizzimfm> Posts
21967
posts
68.9K
followers
2
following
Official Instagram for Dizzim FM | Twitter & FB @dizzimfm | Frequency 93.1 Morogoro | For Enquiries and Submissions - [email protected]
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Sasa ni rasmi, tarehe 21/12/2024, tutamuaga rasmi mwanafamilia wetu katika hafla itakayofanyika Dizzim FM Mtawala HQ.

Ni kweli kwamba kuachana si jambo rahisi, lakini tutakukumbuka daima kwa mchango wako mkubwa na upendo usio na kifani ulioonyesha kwa familia ya Dizzim FM.

Hii si kwaheri ya milele, bali ni ishara ya kuthamini muda uliokuwa nasi. Hakika utaendelea kuwa sehemu muhimu ya historia yetu, na tutakuenzi siku zote!

#KwaheriTutakukumbuka👋🏽👋🏽
#DizzimFm #UlipoTumekufikia by @dizzimfm
6
2 years ago
Download
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, amemtembelea mdau wa muziki na mlezi wa vipaji, Mkubwa Fella, nyumbani kwake na kumkabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya matibabu.

Katika ziara hiyo, Majaliwa pia alifanya mazoezi mepesi ya viungo pamoja na Mkubwa Fella na kupata nafasi ya kuzungumza naye kuhusu mchango wake mkubwa katika kukuza vipaji vya wasanii na maendeleo ya tasnia ya muziki nchini.

Aidha, Majaliwa ameahidi kuendelea kumtembelea Mkubwa Fella mara kwa mara ili kufuatilia maendeleo ya afya yake na kumpa faraja katika kipindi anachoendelea na matibabu. by @dizzimfm
0
7 hours ago
Download
Serikali imeendelea na juhudi za kuimarisha elimu jumuishi nchini kwa kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalumu wanapata haki ya elimu bila malipo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora na yenye usawa.

Hatua hiyo imeelezwa wakati wa mkutano wa tano wa Chama cha Wanawake Wamiliki wa Shule na Vyuo Tanzania (TAWOSCO) uliofanyika mjini Morogoro, ukiwaleta pamoja wamiliki wa shule za msingi, sekondari na vyuo binafsi kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kujadili maendeleo ya sekta ya elimu na mchango wa taasisi binafsi.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Ameir, amesema Serikali imeendelea kujizatiti kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora na bure, wakiwemo watoto wenye mahitaji maalumu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amelipongeza TAWOSCO kwa mchango wake katika kuendeleza sekta ya elimu na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa elimu bora yenye ushindani nchini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, amewapongeza TAWOSCO kwa kuwaunganisha wadau wa elimu na taasisi mbalimbali katika kujadili changamoto na maendeleo ya sekta hiyo.

Kwa upande wake, Katibu wa TAWOSCO, Aysha Shamte, amesema mazingira rafiki yanayotolewa na Serikali yamechangia taasisi binafsi kupiga hatua katika utekelezaji wa malengo yao, huku akieleza kuwa wamechukua hatua kuongeza uwezo wa kupokea wanafunzi wengi zaidi na kupunguza changamoto zilizokuwa zikijitokeza awali. by @dizzimfm
0
a day ago
Download
Watanzania wametakiwa kuendelea kuonyesha dhamira na kuongeza juhudi katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, huku ikielezwa kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ina nia ya kuendeleza ajenda hiyo.

Akizungumza leo Julai 24, 2026 akiwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Dkt. Nchimbi amesema mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai pamoja na Tume ya Jaji Chande yameonesha umuhimu wa kuendelea na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya kwa lengo la kuimarisha utawala bora na demokrasia.

Amesema Watanzania hawapaswi kulegeza juhudi katika kudai Katiba Mpya, akisisitiza kuwa kuendelea kuipa kipaumbele ajenda hiyo kutasaidia kuhakikisha mchakato huo unakamilika chini ya uongozi wenye utayari wa kuutekeleza. by @dizzimfm
3
a day ago
Download
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia Julai 24, 2026 katika eneo la Mafiga, Manispaa ya Morogoro, kwenye barabara ya Morogoro–Iringa.

Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 738 DQD, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), pamoja na lori lililokuwa limebeba mchanga likitokea Lugono kuelekea Chalinze.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mtu mmoja amepoteza maisha huku wengine wawili wakipata majeraha.

Kwa mujibu wa Kamanda Kantimbo, uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori aina ya FAW, ambaye aliacha njia yake na kuingia upande wa kulia wa barabara, na kusababisha kugongana na lori lingine.

Baada ya ajali hiyo, lori lililosababisha tukio liliteketea kwa moto, huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo. by @dizzimfm
0
a day ago
Download
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Benki ya Azania imezindua rasmi mradi wa utoaji wa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo kwa ajili ya ujenzi na uendeshaji wa vituo vidogo vya kuuza mafuta ya petroli na dizeli katika maeneo ya vijijini.

Mradi huo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za mafuta vijijini, kupunguza gharama za wananchi pamoja na kukomesha biashara hatarishi ya kuuza mafuta kwenye chupa za plastiki na vyombo visivyokidhi viwango vya usalama.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba kwa wanufaika nane wa kwanza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Mafuta na Gesi), Dkt. James Mataragio, amesema Serikali imeamua kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi ili kupunguza changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata mafuta.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema mpango huo unafungua ukurasa mpya wa kusambaza huduma za mafuta katika maeneo ya vijijini, huku ukichangia kupunguza gharama za uzalishaji, usafirishaji na hatari za moto zinazotokana na uuzaji holela wa mafuta.

Aidha, REA imeeleza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 12 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo nchini, huku wanufaika nane wa kwanza wakipatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1, na dirisha la maombi likiendelea kuwa wazi kwa wajasiriamali wengine. by @dizzimfm
0
2 days ago
Download
Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) inaendelea kuimarisha uzalishaji na biashara ya zao la vitunguu kwa kukamilisha miongozo ya usimamizi wa zao hilo pamoja na kuendeleza miundombinu ya masoko, hatua zinazolenga kuongeza ushindani wa vitunguu vya Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Akizungumza akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Karatu, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, ameielekeza COPRA kukamilisha miongozo ya zao la vitunguu ndani ya miezi mitatu na kuanza mchakato wa kupanua Soko la Vitunguu la Endashangwet ili kuongeza fursa za masoko kwa wakulima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Irene Mlola, amesema miongozo hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilishwa na itaweka mfumo rasmi wa biashara ya vitunguu kupitia matumizi ya vipimo sahihi, vifungashio sanifu na usimamizi bora wa masoko.

Katika mwaka wa 2025/2026, Tanzania ilisafirisha kilogramu 33,295,659 za vitunguu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.9, huku Serikali ikilenga kuongeza thamani ya zao hilo, kupanua masoko ya kimataifa na kuinua kipato cha wakulima. by @dizzimfm
0
2 days ago
Download
Rangi mpya inaweza kubadilisha kabisa mwonekano wa nyumba. Lakini swali ni...

Wewe ungechagua rangi ipi kwa kuta za nyumba yako?

Andika rangi unayoipenda kwenye maoni! 👇

 #InteriorDesign #ColourPalette #plascontanzania🇹🇿#nizaidiyarangi #ThePaintThatBuildsAfrica by @dizzimfm
0
2 days ago
Download
Kupitia #DizzimCourt Leo @mooh_savage na @dinnynasorotz wameletewa file la Jaiva na Kisha kulijadili kwa upana ili pia kutoa ushauri na namna ambavyo inatakiwa kuwa 

Full story ipo kwenye YouTube channel yetu ya DizzimOnline 

Powered by @plascontanzania 

Shot and edited by @jacksoni_mrema 

#DizzimCourt #WeGotYouCovered by @dizzimfm
2
2 days ago
Download
Kuta zako huleta hisia za nyumba yako.

Splashing Pond huongeza mvuto na upekee.
Plaster huleta mwonekano safi na utulivu.
Ukizichanganya? Unapata uwiano mzuri wa rangi.

Ni ipi inayoendana zaidi na mtindo wako?

#PaintInspiration #ColourChoice #plascontanzania🇹🇿 #nizaidiyarangi #ThePaintThatBuildsAfrica by @dizzimfm
1
3 days ago
Download
Leo kwenye #DizzimCourt file la #Harmonize limefika mezani kwa @mooh_savage na @dinnynasorotz kujadiliwa na kinachoonekana ni kwamba file no gumu sana kulishikilia tu 

Full story ipo kwenye YouTube channel yetu ya DizzimOnline 

Powered by @plascontanzania 

Shot and edited by @jacksoni_mrema 

#DizzimCourt #WeGotYouCovered by @dizzimfm
21
3 days ago
Download
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema rasmi kuwa Uwanja wa Uhuru utakuwa tayari kutumika kwa ajili ya matukio ya Simba Day na Yanga Day, baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya uwanja huo, Msigwa amesema Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 19 katika kazi za ukarabati ili kuhakikisha unakidhi viwango vinavyohitajika kwa matumizi ya michezo na matukio makubwa.

Ameeleza kuwa kukamilika kwa ukarabati huo kutatoa fursa kwa mashabiki wa soka kushuhudia matukio hayo mawili makubwa katika mazingira bora na salama. by @dizzimfm
0
3 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up