Instagram story viewer> @dodomafmradio> Posts
39.2K
followers
23
following
Official page Dodoma Fm Radio
[email protected]
π‘»π’–π’”π’Šπ’Œπ’Šπ’π’Šπ’›π’† π‘³π’Šπ’—π’† π‘²π’–π’‘π’Šπ’•π’Šπ’‚ π‘³π’Šπ’π’Œ πŸ‘‡
0715244705
POSTS STORIES REELS TAGGED
Taasisi binafsi zinazojihusisha na uhifadhi wa mazingira zimetakiwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan katika nguzo ya hifadhi na usimamizi wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za LEAD Foundation jijini Dodoma, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, Timotheo Mande, Bwana Miti kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, amesema taasisi hizo zina nafasi kubwa katika kusaidia Serikali kufikia malengo yaliyowekwa kupitia dira hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi wa LEAD Foundation, Njamasi Chiwanga, amesema taasisi hiyo imekuwa ikihamasisha jamii kuhusu uhifadhi wa mazingira kupitia kampeni ya Kisiki Hai, ambayo sasa imeingia awamu ya pili kwa lengo la kuongeza kasi ya urejeshaji wa ardhi iliyoharibika.

Naye Meneja wa Justdiggit Tanzania, Mary Sengelela, amesema wameendelea kushirikiana na halmashauri husika kufikisha elimu na kuendeleza shughuli za urejeshaji wa mazingira katika vijiji mbalimbali vyenye uhitaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya programu ya Kisiki Hai, zaidi ya miti milioni 32 imerejeshwa katika hekta 500,000 za mashamba, ikihusisha zaidi ya kaya 200,000 za wakulima katika vijiji zaidi ya 650 vya mikoa ya Dodoma na Singida. Kupitia awamu ya pili, LEAD Foundation na Justdiggit wanalenga kuongeza eneo hilo hadi hekta milioni moja na kufikia angalau vijiji 1,000 ifikapo mwaka 2030.

Baadhi ya wananchi wamesema ushiriki wa taasisi binafsi katika uhifadhi wa mazingira, hususan katika shughuli za kilimo, ni muhimu kwa kuwa unasaidia kulinda ardhi na kuimarisha uzalishaji, huku ukiunga mkono juhudi za Serikali kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. by @dodomafmradio
0
35 minutes ago
Download
Ngoma zinabondwa na dj dapher micharazoni
#MicharazoTime by @dodomafmradio
3
an hour ago
Download
Ukitaka kumpa zawadi 'Mwali wako' wewe mpelekee Puma Gas 

@pumaenergy_tanzania 

#dodomafm2026 by @dodomafmradio
0
an hour ago
Download
Nani atamjibu Mic Planet kwenye Micharazo karaoke
@micplanet_
#micharqzokaraoke
#MicharazoTime2026 by @dodomafmradio
1
3 hours ago
Download
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewataka viongozi wa dini nchini kuwa sehemu ya suluhisho katika kukabiliana na changamoto ya viongozi wasiozingatia maadili na uadilifu katika utumishi wa umma. Amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kutumia nafasi zao kuhubiri ukweli, haki, uwajibikaji na uadilifu ili kusaidia kujenga jamii inayozingatia misingi ya maadili mema.

Aidha, ameeleza kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuelimisha jamii na kukemea vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili, ikiwemo rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Wito huo unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za dini na jamii katika kuhamasisha uwajibikaji na kuhakikisha viongozi wa umma wanatekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kwa maslahi ya wananchi. by @dodomafmradio
0
4 hours ago
Download
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 15 kupitia TARURA katika mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za maingilio na mchepuko mkoani Songwe, ili kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 6 zitaelekezwa Wilaya ya Momba, ambapo bilioni 3 ni kwa Tunduma na bilioni 3 kwa maeneo mengine ya wilaya hiyo, huku bilioni 9 zikielekezwa Mbozi, Ileje na Songwe.

Prof. Shemdoe ameyasema hayo Oktoba 15, 2026, wakati akijibu kero zilizowasilishwa na wananchi wa Tunduma katika mkutano wa hadhara uliofanyika wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, mkoani Songwe. Amesema ujenzi huo utasaidia kupunguza msongamano katika barabara ya Tunduma–Mpaka wa Zambia, barabara kuu ya TANZAM inayounganisha Igawa, Songwe na Tunduma, pamoja na barabara ya Mpemba–Tunduma, hususan eneo la mizani ya Mpemba.

Katika sekta ya afya na elimu, Prof. Shemdoe amesema Serikali imetenga shilingi milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ivuna, inaendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduma, pamoja na kukamilisha shule ya saba ya ghorofa, huku shule sita zikiwa zimekamilika. 

Hatua hizo zinalenga kuboresha huduma za afya na kukabiliana na ongezeko la wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza mwaka 2028 kupitia mfumo wa double cohort, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha miundombinu na huduma za kijamii mkoani Songwe. by @dodomafmradio
0
5 hours ago
Download
Timu ya Azam FC leo inatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na Zed FC katika mchezo wa raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF TotalEnergies Confederation Cup), hatua ya kwanza (First Leg). Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikihitaji kupata matokeo mazuri yatakayoipa nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano. Wakati maandalizi ya mchezo huo yakiendelea, mashabiki wa Azam FC waliopo nchini Misri wamewaomba mashabiki wengine kutoka Tanzania kujitokeza kwa wingi kuipa nguvu timu hiyo.

Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Cairo International nchini Misri kuanzia saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Mashabiki hao wameeleza umuhimu wa mshikamano na sapoti kwa Azam FC inapoiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo ya kimataifa, huku wakitarajia kuona timu hiyo ikipambana kupata matokeo mazuri ugenini na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo. by @dodomafmradio
2
6 hours ago
Download
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo Oktoba 16, 2026, amekagua ujenzi wa miundombinu ya Mradi wa Maji wa Forest Mpya jijini Mbeya, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo. Mradi huo unaotumia maji kutoka Mto Kiwira unahusisha ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni tano za maji, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi.

Akizungumza na viongozi pamoja na wananchi, Mhe. Ndejembi amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka kipaumbele katika kuboresha huduma muhimu za kijamii, ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, ili kuinua hali ya maisha ya Watanzania. Amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo kwa uhakika na kwa wakati.

Aidha, Mhe. Ndejembi ameeleza kuwa Mkoa wa Mbeya una nafasi muhimu katika uchumi wa Taifa, hivyo upatikanaji wa maji ya uhakika ni nguzo muhimu katika kuchochea uzalishaji, biashara na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na maeneo ya jirani, hivyo kupunguza changamoto ya huduma hiyo kwa wananchi. by @dodomafmradio
0
6 hours ago
Download
Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Masanja Kadogosa, amemuondoa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe, Mhandisi Fredrick Mande, kutokana na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Forodha–OSBP–Tunduma wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha miradi ya miundombinu inatekelezwa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.

Uamuzi huo unakuja wakati Serikali ikiendelea kusisitiza uwajibikaji kwa watendaji wanaosimamia miradi ya maendeleo, hususan katika sekta ya ujenzi. Kuondolewa kwa kiongozi huyo kunatoa ujumbe kuhusu umuhimu wa kusimamia kikamilifu miradi ya barabara ili kukamilika kwa wakati na kutoa huduma inayotarajiwa kwa wananchi na watumiaji wa miundombinu hiyo. by @dodomafmradio
0
7 hours ago
Download
Kimeumana πŸ˜‚

#dodomafm2026 #funnyclips by @dodomafmradio
11
8 hours ago
Download
Mwanamume aliyejaribu kushinda kipimo cha dawa za kulevya mahali pa kazi alijikuta akijiweka wazi kwa njia tofauti kabisa baada ya sampuli ya mkojo aliyowasilisha kurudi na matokeo ambayo hakuna aliyetarajia

Mwanamume huyo alikuwa na wasiwasi kwamba sampuli yake mwenyewe ingepimwa na kuwa na virusi, kwa hivyo alichukua mkojo wa mtu mwingine kwa siri na kuuwasilisha kwa jina lake.

Kwa muda, mpango huo ulionekana kufanya kazi.

Sampuli haikusababisha matokeo ambayo alikuwa akijaribu kuepuka.

Badala yake, wafanyakazi wa maabara waligundua kitu cha ajabu sana.

Mkojo ulikuwa na homoni za ujauzito.

Mwanamume huyo alipoulizwa kuhusu jinsi hilo lilivyowezekana, hadithi yake ilianza kuharibika haraka.

Hatimaye alikiri kwamba sampuli haikuwa yake na ilitoka kwa mwanamke - akibadilisha kile kilichodhaniwa kuwa njia ya busara ya kupima dawa za kulevya kuwa kitu halisi kilichomfunua.

Alijaribu kuficha matokeo moja chanya na kwa namna fulani akarudi akiwa mjamzito badala yake.

#dodomafm2026 by @dodomafmradio
7
8 hours ago
Download
"Rushwa ni sababu ya umasikini kwa vijana,  na kupitia rushwa na ndoto za vijana wengi zinashindwa kutumia" by @dodomafmradio
1
10 hours ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up