Instagram story viewer> @iringa_dc> Posts
4.3K
followers
331
following
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni Taasisi ya Serikali inayohudumia Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Mtihani Mwema darasa la nne 📍 

@rsiringa by @iringa_dc
0
an hour ago
Download
Miaka 💯 ya shule ya sekondari Tosamaganga Oktoba 10, 2026 Maadhimisho ya Jubilei 🔥🔥 

#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji 
@tamisemi @rsiringa @tosamaganga_sec_official by @iringa_dc
0
2 hours ago
Download
Miaka 💯 ya shule ya sekondari Tosamaganga 
Tukutane Msiwasi 📍

#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji 
@tamisemi @rsiringa @_tosamagangasecondary569 by @iringa_dc
1
19 hours ago
Download
TATHMINI YA TAHADHARI YA EL NINO YAFANYIKA IRINGA DC

Wananchi wahamasishwa kuchukua tahadhari kwa kuimarisha usafi wa mifereji ya maji na mazingira kwa ujumla

Uhifadhi wa chakula mahali salama wasisitizwa

Katibu tawala wa Wilaya ya Iringa Ndugu Benard Urassa ameongoza kamati ya usalama ya Wilaya na Timu ya kushughukikia maafa ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kutembelea maeneo yaliyobainishwa kuwa na uwezekano wa kukumbwa na athari za el nino kutoa elimu na kuwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari kwenye maeneo ya miundombinu, makazi na hifadhi ya chakula.

Ziara hiyo imefanyika katika vijiji vya kata za Migoli na Izazi Oktoba 01, 2026. Timu imeweza kukutana na viongozi wa vijiji na baadhi ya wananchi na kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na athari zinazotarajiwa kujitokeza wakati wa mvua.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo ndugu Urassa amewahimiza wananchi kuchukua hatua za mapema ikiwemo usafi wa nazingira kuepuka mlipuko wa magonjwa, uhifadhi bora wa chakula na watu walio kwenye mazingira hatarishi kuhamia maeneo salama jambo ambalo baadhi ya wananchi wameanza kulitekeleza.

Kwa upande wao viongozi wa taasisi za serikali kama TANESCO, TARURA, TANROADS, JESHI LA ZIMAMOTO, JESHI LA POLISI nao walieleza mikakati yao na kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuitikia hali yoyote ta dharura itakayojutokeza

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndugu George Magembe amefafanua lengo la ziara hiyo na kutoa wito kwa wananchi kuchukua hatua zilizo katika uwezo wao kama vile usafi wa mazingira, mifereji ya maji na uhifadhi wa chakula badala ya kusubiri hatua za Serikali pekee.

Timu hii imepita kwenye maeneo yaliyobainishwa kuwa na uwezekano wa kuathirika au kuleta athari na kushauri hatua za kuchukua kwa taasisi husika kwa kushirikiana na wananchi.

#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji
@tamisemi @rsiringa @owm_tz @owm.sbu by @iringa_dc
1
2 days ago
Download
Miaka 💯 ya shule ya sekondari Tosamaganga 📍 

#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji 
@tamisemi @rsiringa @_tosamagangasecondary569 @maelezonews @msemajimkuuwaserikali @tosamaganga_sec_official by @iringa_dc
2
2 days ago
Download
IRINGA YAJIPANGA JUBILEI YA MIAKA 100 YA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

RC Iringa awakaribisha wadau wote wa elimu wa ndani na nje ya Tanzania, azindua jezi maalumu ya 'funny run'

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James ametoa neno la ukaribisho kwa wananchi wote waliopo ndani na nje ya nchi kuja kushiriki tukio maalumu la maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 ya shule ya sekondari Tosamaganga.

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya maandalizi ya tukio hilo shuleni hapo Septemba 30, 2026 Mhe. James  amesema shule ya Sekondari Tosamaganga inabeba historia kubwa ya Mkoa wa Iringa hivyo maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 ni muhimu kwa heshima ya taaluma na  malezi nchini.

Sanjari na hayo Mhe. James amezindua jezi maalumu itakayotumika kwenye mbio kama maandalizi ya tukio ka Jubilei.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndg. Robert Masunya amesema maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 ya shule ya sekondari Tosamaganga yatafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 8 hadi 10 ambayo ndio kilele cha shughuli hiyo.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kutanguliwa na shughuli mbalimbali za kijamii tarehe 8 kisha mbio za hisani (funny run ) tarehe 9. Shule ya Sekondari Tosamaganga yenye usajili wa namba moja nchini inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake

@tamisemi @rsiringa by @iringa_dc
0
4 days ago
Download
"Uchomaji wa Moto Ovyo, Huleta Madhara Makubwa Katika Jamii" - RC Kheri James

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James ameendelea na ziara yake  kwa kuwatembelea wananchi.

Mhe. Kheri amefika Kata ya Ifunda Kijiji cha Udumuka Septemba 29, 2026,  na kuongea na wananchi, ikiwa ni kuwaonya juu ya uchomaji moto misitu na mashamba. 

Mhe. Kheri amesema, "uchomaji misitu na mashamba ovyo huleta madhara makubwa kwa jamii, hata kwa wanyama. Mtu anapotaka kuchoma shamba analazimika kutoa taarifa kwa Uongozi wa Kijiji, ili moto ukiwa mkubwa na ukamshinda kuzima anaweza kupata msaada kwa haraka. Pia unapotaka kuchoma shamba hakikisha unadhibiti moto usisambae kwa eneo kubwa na kusababisha madhara. Toa taarifa kabla ya kufanya jambo hilo, na ikitokea umechoma shamba au msitu bila kushirikisha watu wengine, basi tutachukulia umefanya makusudi na tutakuchukulia hatua".

Aidha, Mhe. Kheri amewaambia wananchi wa Kijiji hicho kuchukua tahadhari juu ya mvua kubwa za Elnino zinazotarajiwa kunyesha, na kuwaasa kuchukua tahadhari na kuhifadhi chakula kwa kipindi chote cha mvua hizo.

@owmtamisemi
@rsiringa by @iringa_dc
0
5 days ago
Download
Mwanafunzi Akipata Ujauzito, Wazazi Kuchukuliwa Hatua" - RC Kheri James

Zaidi ya Milioni 100 Zimetolewa na Serikali katika Shule ya Sekondari Lupembelwasenga Kata ya Lyamgungwe.

Hatua hiyo imepelekea Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James kuwaambia wazazi na wananchi wa Kata hiyo Septemba 29, 2026 baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Bweni la Shule hiyo.

"Mtoto akipata ujauzito na kukatisha ndoto zake, wazazi na Kijana aliyempa ujauzito watachukuliwa hatua kali za kisheia. Bweni limejengwa na leo nimeweka jiwe la msingi, baada ya kukamilika kwa jengo hilo kila mwanafunzi wa kike wa shule hiyo atalazimika kukaa bwenini. Serikali imejenga bweni hilo ili kuwapungizia watoto umbali mrefu kwa kwenda na kurudi shuleni, na kuepusha mimba za utotoni".

Mhe. Kheri pia amewaambia wananchi wa Kata hiyo kulima kwa tija, akiwa na maana kuwa walime mazao ya chakula na biashara ili kuinua kipato cha familia.

Aidha, Mhe. Kheri ametoa elimu juu ya kuchukua tahadhari katika mvua kubwa za Elnino zinazotarajiwa kunyesha na kusisitiza kuhifadhi chakula kipindi chote cha mvua hizo.

@owmtamisemi
@rsiringa by @iringa_dc
0
5 days ago
Download
World Vision Wakabidhi Jengo la Kukusanyia Maziwa kwa Serikali, Kiponzero

Kaimu Katibu Tawala akimuawakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndugu Elia Luvanda Seotemba 29, 2026, amekabidhiwa jengo la kukusanyia maziwa Tarafa ya Kiponzero Kata ya Maboga kwa naiba ya wananchi.

Jengo hilo ambalo limegharimu zaidi Milioni 250, ikiwa pamoja na genereta litakuwa msaada kwa wananchi na Wajasiriamali ambao watakuwa wanauza maziwa katika kituo hicho.

Akitoa taarifa ya mradi huo Word Vision wanafurahi kufanya kazi na Serikali kwa uhuru na uwazi na kwamba kuwasaidia wananchi ni jukumu lao kama Shirika.

Ndugu Luvanda amewaambia wananchi kuwa, wanaishukuru Wirld Visio kwa kujitoa kwao na kusaidia wananchi katika nyanja mbalimbali kama kilimo, ujasiriamali na elimu ya kujitegemea, hivyo wananchi watumie fursa hiyo kujifunza.

Pia Ndugu Luvanda ametoa elimu juu ya mvua za Elnino na kwamba wananchi wachukue tahadhari na kuhifadhi chakula

@owmtamisemi
@rsiringa 
@worldvisiontz by @iringa_dc
0
5 days ago
Download
Zaidi ya Milioni 400, zimejenga Wodi ya Mama na Mtoto Kiponzero - World Vision

World Vision ni Shirika la Dini lisilo la Kiserikali ambalo limejikita kusaidia wananchi wenye mazingira magumu, na kuwainua Wajasiriamal, i pia kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Kituo cha Afya Kiponzero Kata ya Maboga shiriki hilo limejenga wodi ya Mama na Mtoto na sehemu ya upasuaji kwa wajawazito.

Septemba 29, 2026 Shirika hilo limemualika Mkuu wa Mkoa kuzindua na kukabidhi jengo hilo ambapo tayari lina vifaa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma.

Akisoma ripoti ya ujenzi huo Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho amesema, anashukuru Shirika hilo kwani jengo la mama na mtoto la zamani lilikuwa linechakaa.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Kaimu Katibu Tawala Mkoa Ndugu Elia Luvanda, amepongeza kwa shirika hilo jinsi linavyosaidia Serikali na kuomba Wadau wengine waige mfano kutoka kwa World Vision.

Aidha, Ndugu Luvanda amewaasa Watumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wananchi na kutumia miundombinu hiyo kama fursa ha kufanya kazi kwa ufanisi.

Pia amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Watumishi wanaotoa huduma katika maeneo hayo ikiwa na kufanya usafi katika mazingira ya kutolea huduma.

Ndugu Luvanda pia amewakumbusha wananchi kwa kutoa elimu juu ya kuchukua tahadhari katika mvua kubwa za Elnino zinazotarajiwa kunyesha, ikiwa na kuhifadhi chakula kipindi chote cha mvua hizo.

@owmtamisemi
@wizarayaafya
@rsiringa
@worldvisiontz by @iringa_dc
0
5 days ago
Download
KM 9 ZA SAFARI ZAGEUKA HISTORIA, SERIKALI YAJENGA BWENI LA MILIONI 140

● LUPMBELWASENGA YAPATA BWENI, WANANCHI WAOMBA HUDUMA ZAIDI ZA MIUNDOMBINU

Wananchi wa Kata ya Lyamgungwe, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wameishukuru Serikali kwa kuwajengea bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 wa kike katika Shule ya Sekondari Lupembelwasenga, wakisema litasaidia kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni na kupunguza mimba za utotoni. Aidha, wameomba kujengwa kwa bweni la wavulana.

Wakizungumza Septemba 30, 2026, wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa ya kukagua miradi ya maendeleo, wananchi hao wamesema ujenzi wa bweni hilo ni hatua muhimu katika kuboresha mazingira ya elimu na usalama wa wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufika shuleni.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Lupembelwasenga, Mwl. Edda Kutika, amesema bweni hilo linalenga kupunguza safari ya takribani kilomita tisa kwa wanafunzi, pamoja na utoro na mimba za utotoni huku akisema kuwa mradi huo umegharimu Shilingi milioni 140 kutoka Serikali Kuu, huku wananchi wakichangia nguvu zao kwa kukusanya tripu 70 za mawe.

Nae Diwani wa Kata ya Lyamgungwe, Mhe. Alex Malangalila, ameishukuru Serikali kwa ujenzi huo huku akiomba kujengwa kwa maabara pamoja na kusogezwa kwa nguzo za umeme katika eneo la bweni. Pia amemshukuru mwananchi aliyetoa ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, ameagiza bweni hilo kukamilika ifikapo Oktoba 15, 2026, akisema fedha na vifaa vipo. Pia ameagiza TANESCO kuhakikisha nguzo za umeme zinafikishwa kwa wakati.

Aidha, Mhe. Kheri amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo, akisema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha mazingira ya elimu na kwamba ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kulinda na kunufaika na miradi ya maendeleo.
#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji 
@tamisemi @wizara_elimutanzania @iringa_dc by @iringa_dc
0
6 days ago
Download
IRINGA DC YATATHMINI MAANDALIZI YA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NINO NA EBOLA

Yahuisha kamati ya Mawasiliano na Ushirikishwaji wa jamii katika majanga (Risk Communication and community Engagement – RCCE)

Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya, na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wamefanya zoezi maalum la tathmini ya mfumo wa uratibu wa shughuli za afya kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuona utayari wa timu hiyo kwenye eneo la mwitikio wa majanga hususani kwenye kipindi hiki cha tishio la ugonjwa wa Ebola pamoja na taarifa za uwezekano wa uwepo wa mvua kubwa  za El Nino.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa zoezi hilo, Septemba 24, 2026 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Ndg. Robert Masunya, ametoa wito kwa wataalamu wote wanaohusika kuhakikisha wanajibu dodoso hilo kwa umakini, uadilifu na usahihi, kwa kuwa taarifa zitakazopatikana zitasaidia kubaini maeneo yanayohitaji kuimarishwa na hatimaye kuongeza ufanisi wa hatua za kinga na mwitikio.

Ndg. Masunya amesisitiza kuwa ushiriki wa wataalamu katika zoezi hilo si suala la kujaza dodoso pekee, bali ni sehemu ya maandalizi muhimu ya Halmashauri ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na wanapata elimu sahihi kwa wakati.

“Natoa wito kwa wataalamu wote kujibu dodoso hili kwa umakini na kutoa taarifa sahihi ili ziwe na manufaa katika kupanga na kuchukua hatua zinazolenga kuwalinda na kuwahudumia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa ufanisi zaidi” amesema Ndg. Masunya.

Zoezi hili ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya za kuimarisha utayari na mifumo ya uratibu wa afya katika ngazi za Halmashauri ili kuhakikisha mamlaka husika zinakuwa tayari kuchukua hatua za dharura na kukabiliana na changamoto za kiafya zinazoweza kujitokeza ambapo hatua inayofuata ni kuifikia jamii katika utoaji wa elimu.
@tamisemi @wizara_afyatz @rsiringa by @iringa_dc
0
10 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up