Instagram story viewer> @iringa_rs> Posts
2.4K
followers
24
following
RC | @comradekheri
Ukurasa Rasmi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa IRINGA
#IringaimaraTutaijengakwaUmojanaUwajibikaji
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
📍IRINGA. 

RC KHERI JAMES ARIDHISHWA NA KASI YA UKARABATI WA BARABARA YA IPOGOLO. 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Komred Kheri James, amefanya ziara fupi ya kutembelea mradi wa ukarabati wa Barabara ya Ipogolo yenye lengo la kuimarisha njia za maji za Barabara hiyo ili kuipa uwezo Barabara hiyo kuhimili athari za mvua ambazo zimekua ni changamoto ya muda mrefu katika eneo hilo. 

Akizungumza katika ziara hiyo Komred Kheri James ameeleza kuwa dhamira ya Serikali ni kulinda Usalama wa Wananchi na kuweka uhakika wa kusafiri na kusafirisha Bidhaa kupitia barabara hiyo ambayo ni kiungo cha kijamii na kiuchumi kitaifa na kimataifa. 

Pamoja na mambo mengine Komred Kheri James ameipongeza TANROAD pamoja na mkandarasi kwa kasi na ubora wa utekelezaji wa mradi huo na amewasihi Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi cha utekekelezaji wa mradi na kuwasisitiza wazingatie maelekezo ya TANROAD pamoja na Jeshi la Polisi ili kumpa mkandarasi mazingira mazuri ya kutekeleza mradi huo bila changamoto. 

#IringaimaraTutaijengaKwaUmojanaUwajibikaji 

@comradekheri | @owm_tz | | @tanroadshq 

.

| | @ikulu_mawasiliano | @ccmtanzania | @wizara_elimutanzania | @urtmof | @bunge.tanzania | @ofisi_ya_makamu_wa_rais | @mafinga_town_council | | @ortamisemi | @msemajimkuuwaserikali | @maelezonews | @iringa_dc | taken in Ipogolo-Iringa by @iringa_rs
1
a month ago
Download
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan alipowasili katika Uwanja wa Ndege Mkoani Iringa ambapo atashiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yatakayofanyika mkoani Njombe Leo Mei 1, 2026.

Fuatilia mitandao yetu ya kijamii 
Instagram: @mamakajatz
Twitter @mamakajatz
Facebook: Mamakajatz
YouTube: Mama kaja tz 

#Mamakaja #kazinaututunasongambele taken in Iringa, Tanzania by @iringa_rs
0
5 months ago
Download
TAARIFA YA ZIARA YA MHESHIMIWA WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. MWIGULU NCHEMBA (MB) MKOANI IRINGA. taken in Iringa, Tanzania by @iringa_rs
0
5 months ago
Download
📍IRINGA.

RC IRINGA AHIMIZA UWAJIBIKAJI NA UBUNIFU KWA BODI
MPYA YA IRUWASA.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Komred Kheri James, amewataka wajumbe wa Bodi Mpya ya mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Iringa Iruwasa kuwajibika kikamilifu ili
kuongeza ufanisi na ubora wa huduma kwa umma.

Komred Kheri James ametoa maelekezo hayo mapema leo katika zoezi fupi la uzinduzi wa bodi ya 10 ya Iruwasa, zoezi lililokwenda sambamba na utoaji wa vitendea kazi kwa wajumbe wapya wa Bodi hiyo.

Pamoja na mambo mengine ameipongeza Bodi iliomaliza muda
wake, ameipongeza Bodi mpya na kuwahimiza kusimamia miradi, ubora wa huduma, matumizi ya teknolojia na utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.

#IringaimaraTutaijengaKwaUmojanaUwajibikaji 

@comradekheri | @owm_tz | | @tamisemi 

.

 | @ruaha_national_park | @ikulu_mawasiliano |  @ccmtanzania | @wizara_elimutanzania | @urtmof | @bunge.tanzania | @ofisi_ya_makamu_wa_rais | @mafinga_town_council | | @ortamisemi | @msemajimkuuwaserikali | @maelezonews | @iringa_dc | Comrade Kheri James taken in Iringa, Tanzania by @iringa_rs
2
5 months ago
Download
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James, ameagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Kilolo kuhakikisha wanasambaza miche ya miti ya matunda katika shule mbalimbali kwa lengo la kuboresha lishe ya wanafunzi, badala ya kuendelea kupanda miti ya vivuli pekee huku akiwataka wakuu wa shule kuhakikisha kila mwanafunzi anapatiwa mche na kuusimamia

Mapema leo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amefanya ziara katika Shule ya Sekondari Irole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, kwa lengo la kujionea hali na maendeleo ya shule hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha na kuwatia moyo walimu kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi pamoja na kuimarisha malezi yao.

Akiwa shuleni hapo, Kheri James amesisitiza umuhimu wa mpango wa lishe kwa wanafunzi, huku akitoa agizo kwa uongozi wa TFS katika halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha wanapeleka miche ya miti ya matunda kwa wingi shuleni kwaajili ya chakula cha wanafunzi.

#2Digital 
#TBC2Updates 
#TBC2Yakijanjazaidi by @iringa_rs
4
6 months ago
Download
taken in Idodi, Iringa, Tanzania by @iringa_rs
2
6 months ago
Download
taken in Iringa, Tanzania by @iringa_rs
2
6 months ago
Download
KILOLO. 

SERIKALI YAWAHIKIKISHIA WANANCHI HUDUMA BORA YA MAJI MKOANI IRINGA. 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Komred Kheri James amewahakishishia Wananchi mkoani humo juu ya dhamira ya dhati ya Serikali ya kuwafikishia huduma bora ya maji safi na salama wananchi wote mkoani humo. 

Komred Kheri James ametoa uhakika huo mapema leo katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Boma la ng’ombe wilayani Kilolo,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji. taken in Kilolo, Iringa, Tanzania by @iringa_rs
3
6 months ago
Download
📍IRINGA

MKOA WA IRINGA WAWAHAKIKISHIA WANAHABARI MAZINGIRA RAFIKI YA KUTENDA MAJUKUMU YAO

Mkuu wa mkoa wa Iringa Komred Kheri James amewaeleza kwamba na kuwapa uhakika waandishi na wahariri wa vyombo vya Habari mkoani humo, kuwa Serikali mkoani humo itaendelea kutoa ushirikiano na kutengeza mazingira rafiki kwa waandishi kufanya majukumu yao ili kuchochea maendeleo na uwajibikaji mkoani humo.

Komred Kheri James alitoa maelezo hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Jumuiya ya vyombo vya habari vya kusini mwa Afrika uliofanyika kwa siku mbili mkoani Iringa.

#IringaimaraTutaijengaKwaUmojanaUwajibikaji 

@comradekheri | @owm_tz | | @ortamisemi

.

 | @ruaha_national_park | @ikulu_mawasiliano |  @ccmtanzania | @wizara_elimutanzania | @urtmof | @bunge.tanzania | @ofisi_ya_makamu_wa_rais | @mafinga_town_council | | @ortamisemi | @msemajimkuuwaserikali | @maelezonews | @iringa_dc | taken in Iringa, Tanzania by @iringa_rs
0
6 months ago
Download
📍IRINGA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Komred Kheri James, mapema leo amempokea Waziri wa Katiba, Sheria na Jinsia wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Alfred Ahingejeje, ambaye amewasili mkoani Iringa kwa ziara ya siku mbili ya mafunzo katika sekta ya Kilimo na Uwezeshaji wa wananchi Kiuchumi.

#IringaimaraTutaijengaKwaUmojanaUwajibikaji 

@comradekheri | @owm_tz | | @ortamisemi

.

 | @ruaha_national_park | @ikulu_mawasiliano |  @ccmtanzania | @wizara_elimutanzania | @urtmof | @bunge.tanzania | @ofisi_ya_makamu_wa_rais | @mafinga_town_council | | @ortamisemi | @msemajimkuuwaserikali | @maelezonews | @iringa_dc | taken in Iringa, Tanzania by @iringa_rs
0
7 months ago
Download
📍IRINGA.

BILIONI 59 ZAONGEZA CHACHU YA HUDUMA NA UKUAJI WA
UTALII MKOANI IRINGA.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Komred Kheri James amewaongoza
viongozi na watumishi kutembelea na kukagua miradi ya
kimkakati inayo tekelezwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa
lengo la kuimarisha miondombinu na Huduma katika hifadhi hiyo.

Akizungumza katika ziara hiyo Komred Kheri James ameeleza
kuwa miradi yote iliopangwa kutekelezwa katika hifadhi hiyo
imekamilika na hivyo kuiwezesha Hifadhi kupata uwanja mpya
wa ndege, vyuma vya kulala, kumbi ndogo za vikao, Kituo cha
Taarifa na kituo cha utafiti.

Komred Kheri James ameeleza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kutimiza maono ya Serikali ya kuimarisha sekta ya utalii na kuongeza idadi ya Watalii nchini.

#IringaimaraTutaijengaKwaUmojanaUwajibikaji 

@comradekheri | @owm_tz | | @ortamisemi

.

 | @ruaha_national_park | @ikulu_mawasiliano |  @ccmtanzania | @wizara_elimutanzania | @urtmof | @bunge.tanzania | @ofisi_ya_makamu_wa_rais | @mafinga_town_council | | @ortamisemi | @msemajimkuuwaserikali | @maelezonews | @iringa_dc | Kheri James taken in Ruaha National Park by @iringa_rs
0
8 months ago
Download
 by @iringa_rs
1
8 months ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up