Instagram story viewer> @japhethnyombe> Posts
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
โœ…๐Ÿ”ด๐Ÿ‘Š BOOOOM! Wana wa Nzambe wamekomesha Ronaldo! ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

โ–ช๏ธโšก DR Congo imefanikiwa kuondoka na pointi muhimu baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Portugal, matokeo yaliyowaongezea matumaini ya kufanya vizuri kwenye mashindano haya makubwa.

โ–ช๏ธโšก Mchezo umemalizika kwa sare ya bao 1-1, huku bao la Yoane Wissa likiwanyima ushindi Wareno na kuwaletea furaha kubwa mashabiki wa DR Congo.

โ–ช๏ธโšก Nahodha wa Portugal, Cristiano Ronaldo, alishindwa kuonyesha makali yake mbele ya safu imara ya ulinzi ya Wakongo, na kuondoka bila kufunga bao.

โ–ช๏ธโšก Sasa DR Congo itahitaji kupambana zaidi katika mechi zake mbili zilizobaki dhidi ya Colombia na Uzbekistan ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

โ–ช๏ธโšก Kwa sasa, DR Congo inapanda hadi nafasi ya pili katika Kundi K, ikisubiri matokeo ya mechi kati ya Colombia na Uzbekistan.

๐Ÿ‘๐Ÿ‘ Hongereni sana Wana wa Nzambe! Mmeonyesha moyo wa kupambana, umoja na uzalendo mkubwa. Sare hii ni ushindi wa heshima na ujumbe kuwa hakuna kisichowezekana kwenye soka! ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ’ชโšฝ๏ธ

#FIFAWorldCup2026 
#nyombejrsportnews 01net by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
MAREKANI: Nahodha wa Argentina, Lionel Messi ameendelea kuandika historia katika Kombe la Dunia baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick) katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Algeria na kufikisha jumla ya mabao 16 katika michuano hiyo.

Hat-trick hiyo imemwezesha Messi aliyecheza mechi 27 kufikia rekodi ya nguli wa Ujerumani, Miroslav Klose, ambaye amekuwa akishikilia rekodi ya mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kucheza michezo 24.

Nani atakuwa Mfalme wa Mabao wa Muda Wote wa Kombe la Dunia? ๐Ÿ‘‘

A. Lionel Messi mchawi wa mpira
B. Kylian Mbappe bado ana muda wa michuano ijayo
C. Cristiano Ronaldo anaweza kushangaza
Mjadala unaoendelea ???

#WorldCup2026
#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
๐Ÿฆ SIMBA WAMERUDI KILELENI! ๐Ÿ”ฅ

Ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City umeifanya Simba SC kufikisha pointi 64 na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa sasa. ๐Ÿ’ช๐Ÿ”ด

Wekundu wa Msimbazi wamefanya kazi yao uwanjani na sasa presha yote inahamia kwa Yanga ambao bado hawajacheza mechi yao. ๐Ÿ‘€

Je, Simba wataendelea kubaki kileleni au Yanga watarudisha nafasi yao? Mbio za ubingwa zimezidi kupamba moto! ๐Ÿ†๐Ÿ”ฅ

#SimbaSC #NguvuMoja #NBCPL #MbioZaUbingwa
#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
Content Creator @kiredio_ ambae pia ni Shabiki wa Argentina na Lionel Messi ameandika barua ya wazi kwa Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Paul Makonda 

Barua hiyo inaeleza haya

"BARUA YA WAZI KWA MH WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NCHINI TANZANIA

Mimi Kama Kijana Wa Kitanzania Kwa Unyenyekevu Mkubwa Sana Kiongozi Wangu Nlikua Naomba Kuja Na Maombi Machache Mbele Yako Kiongozi Wangu

1. Naomba Serikali Kupitia Wizara Yako Ihakikikishe Kila Mtanzania Analipa Kodi Kwa Ajili Tu Ya Kuwepo Hai Na Kuweza Kumshuhudia LIONEL MESSI "Hii Kodi litwe Messi Tax"

2. Naomba Jezi Ya Taifa La Tanzania Namba Kumi Isitumike Tena Na Badala Yake Tuiprint Jina Messi Na Tuihifadhi Vizuri Kwa Ajili Ya Utalii Duniani

3. Naomba Kuwepo Na Somo Jipya Mashuleni Linaloitwa Messi Vijana Wafundishwe Kuwa Mpira Sio Tu Kufunga Bali Ni Kujua Hesabu Kama Vile Angle, Radius, Height, Distance Na Timing, Hii Itasaidia Sana Kukuza Vipaji Vya Vijana Wetu Nchini

4. Naomba Mashabiki Wote Wa Ronaldo Wakamatwe Wahojiwe Kwa Kina, Kwani Hatuna Amani Sisi Kama Mashabiki Wa Messi Na Mda Wowote Wanaweza Kutufanyia Fujo

5. Mashabiki Wa Messi Tupewe Mapumziko Ya Siku Tatu Kuweza Kuangalia Haya Magoli Ya Messi Vizuri Kwani Ni Tiba Na Yanaongeza Ari Katika Ufanyaji Wa Kazi

6. Kuangalia Mechi Za Taifa La Argentina Kwa Wanaume Iwe Lazima Na Sio Ombi, Hii Itasaidia Sana Ndoa Nyingi Kwani Magoli Ya Messi Yanarudisha Mpaka Nguvu Za Kiume

7. Kutokana Na Usalama Wangu Kuwa Mdogo Naomba Serikali Kupitia Wizara Yako Iniite Na Kunipa Ulinzi Dodoma Hata Siku 2 Lakini Pia Nipate Picha Na Wewe Pamoja Na Sahihi Kwenye Mpira Ntakaonunua Kwa Niaba Ya Mashabiki Wote Wa Messi Nchini Tanzania

La Mwisho Japo Sio Muhimu, Leo Usiku Saa 2 Kamili Tanesco Wanaweza Kukata Umeme Na Kufanya Marekebisho Yoyote Ndani Ya Masaa Mawili Kuhakikisha Upatikanaji Bora Wa Nishati Hiyo Nchini

Nnaamini Maombi Yangu Yatakubaliwa. Ahsante"

Una maoni gani juu ha barua hii ๐Ÿ˜๐Ÿ˜..?

#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
Kiungo na nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joshua Kimmich, amezua taharuki baada ya kufichua tukio la kushangaza na la hatari lililotokea kwenye kambi yao ya Kombe la Dunia nchini Marekani. Kimmich ameeleza kuwa kikosi cha Ujerumani kilikumbana na nyoka anayesadikiwa kuwa na sumu kali katika kituo chao cha mazoezi kilichopo Winston-Salem, North Carolina.

Tukio hili la nje ya uwanja limekuja wakati timu hiyo ikiwa kwenye morali ya juu baada ya kuanza michuano hiyo kibabe kwa kuinyuka Curacao mabao 7-1 chini ya kocha Julian Nagelsmann.
โ€‹Akizungumza kuhusu tukio hilo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliliambia gazeti la Bild la Ujerumani kuwa walimuona nyoka huyo jana yake na kupewa tahadhari kubwa na wenyeji. Kimmich alinukuliwa akisema: "Tulimwona nyoka jana, lakini tukaambiwa ana sumu. Ukiumwa, inabidi uende hospitali haraka sana. Sidhani kama utakufa, lakini kwa hakika ni hatari... nina hofu na heshima nao hapa. Kule Ujerumani, nina hisia kwamba hakuna wanyama wengi hatari kama hawa."

โ€‹Habari hii imepokelewa kwa mshtuko mkubwa na mashabiki wa soka mtandaoni, huku wengi wakitoa maoni ya ucheshi na wengine wakitaka usalama wa wachezaji uimarishwe zaidi kwenye hoteli na viwanja vya mazoezi. Pamoja na changamoto hiyo ya "mgeni asiyealikwa" kambini, Ujerumani inatarajiwa kuendelea na ratiba yake ya mechi za makundi ikitolewa macho kama moja ya timu hatari zaidi kwenye safu ya ushambuliaji baada ya onyesho lao la kwanza la mabao saba. 

#nyombejrsportnews@01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
Fainali za Kombe la Dunia za FIFA 2026 zimezidi kuchafua hali ya hewa sokoni baada ya miamba ya soka, Argentina na Norway, kusajili ushindi mnono wa mabao katika michezo yao ya hatua ya makundi iliyopigwa usiku wa kuamkia leo. Mfalme wa soka duniani, Lionel Messi, ameiongoza Argentina kuichakaza Algeria kwa jumla ya mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi J. Messi aliondoka na mpira wa mchezo huo baada ya kupiga hat-trick ya kibabe, akifunga mabao yake mapema mnamo dakika ya 17, kabla ya kurejea tena wavuni dakika ya 60 na kuhitimisha karamu hiyo dakika ya 76 ya mchezo.

โ€‹Wakati huo huo, mashine ya mabao ya Norway, Erling Haaland, naye amewasha moto mkali baada ya kuiongoza timu yake ya taifa kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Iraq katika mchezo wa Kundi I. Haaland alitawala kipindi cha kwanza kwa kupachika mabao mawili ya haraka mnamo dakika ya 29 na ya 43, huku Iraq wakipata bao lao la kufutia machozi dakika ya 39 kupitia kwa mshambuliaji wao Hussein. Kipindi cha pili kilikuwa kigumu zaidi kwa Iraq kwani waliruhusu bao la tatu dakika ya 76 lililowekwa kimiani na Ostgard, kabla ya Hussein kujifunga mwenyewe (og) katika dakika za majeruhi (90+6) na kuwazawadia Norway bao la nne la ushindi.

โ€‹Matokeo haya yanazidi kuongeza presha na msisimko mkubwa kwenye fainali hizi za kihistoria, huku fomu ya ufungaji ya Lionel Messi na Erling Haaland ikituma salamu za wazi kwa wapinzani wao kuelekea hatua ya mtoano. Ushindani huu wa mastaa hawa wawili wakubwa duniani umezua mijadala mizito mitandaoni kuhusu nani atakayeibuka mfungaji bora wa mashindano haya mwaka huu. 

#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡น Ureno ya Cristiano Ronaldo inakutana na ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ Chui wa DR Congo katika pambano kubwa la Kombe la Dunia 2026! Je, Afrika inaweza kuandika historia kwa kuangusha moja ya vigogo wa soka duniani? โšฝ๐Ÿ†

Mchezo huu wa Kundi K unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi huku Portugal wakianza kampeni yao ya kutafuta ubingwa wa dunia, wakati DR Congo wakirejea kwenye jukwaa la Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 50.

๐Ÿ“… Tarehe: Jumatano, 17 Juni 2026 โฐ Saa: 20:00 EAT / 19:00 CAT

๐Ÿ”ฅ Ronaldo dhidi ya Wissa, Fernandes dhidi ya Sadiki โ€“ nani ataondoka na pointi tatu muhimu?

#AzamTV #FIFAWorldCup2026 #MatchDay #PortugalDRCongo #EveryGameLive #WorldCup2026
#nyombejrsportnews 01ๅฅณ็”Ÿ by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
Ligi Kuu ya NBC inaendelea kushika kasi leo hii, Juni 17, 2026, ambapo miamba ya soka kutoka jijini Dar es Salaam, Simba SC, itashuka uwanjani kukabiliana na wenyeji wao, Mbeya City FC. Mchezo huo unatarajiwa kuanza mapema saa 8:00 mchana (14:00 HRS), huku mashabiki wa timu zote mbili wakisubiri kwa hamu kuona jinsi dakika 90 zitakavyoamua hatuzi wa pointi tatu muhimu katika mzunguko huu wa ligi.

โ€‹Pambano hili la kukata na shoka linatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, uwanja ambao unajulikana kwa kuwa na presha kubwa na mashabiki wenye mzuka wa hali ya juu. Simba SC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na dhamira ya kusaka ushindi ugenini ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi, wakati Mbeya City nao wamejipanga vilivyo kutumia vyema faida ya uwanja wa nyumbani na sapoti ya mashabiki wao ili kupindua meza kibabe.

#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
Lionel Messi anafunga hat-trick ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Bao la 16 kwenye michuano ya Kombe la Dunia akifikia rekodi ya Miroslav Klose wa Ujerumani ambaye alikuwa kinara wa magoli kihistoria kwenye michuano hiyo.

Messi ameiandikia Argentina bao la tatu dhidi ya Algeria kwenye mchezo wa Kundi J wa kombe la Dunia la FIFA 2026

Argentina ๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ท 3-0 ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ฟ Algeria 
โšฝ 17โ€™ Messi 
โšฝ 60โ€™ Messi 
โšฝ 76โ€™ Messi

#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
KONE ANAITAKA YANGA

Baada ya mazungumzo ya awali, jana mazungumzo yameendelea tena  kati ya klabu ya Young Africans na kambi ya mlinzi wa kushoto wa Mouna FC raia wa Ivory Coast ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ, Samba Koneฬ (23) 

Samba Kone anaknekana sana kuitaka Young Africans na matarajio ni kusaini miaka miwili kwa wananchi kama kila kitu kitakamilika.

Klabu ya Young Africans Sc wanamuona Kone kama mbadala sahihi wa Boka ambaye hatokuwa sehemu ya kikosi cha Young Africans Sc kuelekea msimu ujao wa 2026/27.

Kone anamaliza mkataba wake na Mouna FC, june 30 mwaka huu.

Mchezaji huyo amewahi kupita Paradou FC ya Algeria ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ฟ.

Msimu huu Kone katoa assist (4) huku akitajwa kama beki bora wa kushoto kwenye ligi ya Ivory Coast.

#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
๐Ÿšจ ๐—˜๐—ซ๐—–๐—Ÿ๐—จ๐—ฆ๐—œ๐—ฉ๐—˜: 

Mshambuliaji wa DR Congo, Fiston Mayele, Amesaini rasmi Mkataba na Klabu ya Al-Fateh ya Saudi Arabia.

Baada ya kuachana na Pyramids FC kisha kuingia kwenye mazungumzo na Klabu nyingi ikiwemo Al Ahly Tripoli ya Libya hatimae sasa Mayele anajiunga na Al-Fateh.

Rasmi sasa Mayele atacheza Ligi ya Saudi Arabia Msimu Ujao. ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉโœ…

#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
Naibu Waziri wa Habari Sanaa utamaduni na Michezo Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA' Amejibu swali la Mbunge wa Jimbo la Bumbwini, Unguja Zanzibar Aliyehoji ni kwanini

"Nchi yetu ni Tanzania, Spain Kuna Ligi ya Spain, England kuna Ligi ya England, South Africa Kuna Ligi ya South Africa, Tanzania Kama Nchi Ligi yake ni ipi? Zanzibar Kuna Ligi ya PBZ, Tanzania Bara Kuna Ligi ya NBC, ipi Ligi ya Taifa kama Nchi?" 

Majibu ya Waziri MWANA FA ๐Ÿ—ฃ

"Ligi ya Muungano inayofanyika sasa hivi ni tofauti na ligi ya Muungano iliyokuwa ikifanyika miaka ya nyuma na sababu ya utofafuti huo ni kwa sababu ligi ya Muungano ya miaka ya nyuma ilikuwa inafanyika ili kupata mwakilishi wa Nchi nzima kama Tanzania ili kupata kwenda katika mashindano Barani Afrika. 

Baadaye baada ya Zanzibar kupata 'Association Membership ya CAF' Iliruhusiwa kutoa timu zake ili kuiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya CAF Kwahiyo hakukuwa tena na ule mshiko wa ligi moja ya Muungano iliyokuwepo mwanzoni kwa sababu ligi hiyo haikutoa tena timu kuwakilisha Barani Afrika.

Tunashindwa kuwa na Ligi moja ya Tanzania ambayo ni hii tunayoiona inafanyika sasa inayoshirikisha vilabu vya Tanzania Bara na Zanzibar kwa sababu Nafasi tulizokuwa tunapata zimegawanywa katika pande mbili Tumeanza mazungumzo ili kuziunganisha Ligi hizo badala ya kutoa washindi kutoka Zanzibar na washindi kutoka Bara wawe washindi wataokwenda kuiwakilisha nchi bila kujali upande walipotokea"Amejibu Naibu Waziri Mwana FA

#nyombejrsportnews @01 by @japhethnyombe
0
a month ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up