Instagram story viewer> @localtourtz> Posts
3.2K
followers
2095
following
Ukurasa kwa ajili kuhamasisha watanzania kufanya utalii wa ndani kupitia vivutio vyetu
Twenzetu Kutalii Tanzania
Hapa ni nyumbani
#Localtourtz
POSTS STORIES REELS TAGGED
Yes Mambo ya Pugu Hills Nature Forest Reserve sio poa usifikirie utaenda kula Good time wapi, ni muda mchache tu kutoka Dar es Salaam. 

#localtourtz by @localtourtz
0
5 months ago
Download
Ebwanee….. #LocalTourTz tulipata nafasi ya kupiga kambi ndani ya Pugu Hills Forest Reserve iliyochini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) lengo likiwa ni moja tu kuhakikisha watalii wanaotembelea eneo lile kuhakikisha wanapiga kura na tunashinda katika kipengele cha African’s Leading Tourist Attractions, sio poa watu kibao walipiga kura na hapa ni kwa uchache tu wa Vaibu baada ya kupiga kura.

Usisahau ku Share, Repost, Comment na Like, pia kuhimiza watu kibao wapige kura. Kumbuka kura yako moja tu ndiyo itapelekea ushindi wetu. VOTE NOW tushinde 

NAMNA YA KUPIGA KURA PUGU HILLS FOREST RESERVE, TANZANIA UTAKUWA UMEPIGA KURA 
1.	bofya hiyo Link ya https://www.worldtravelawards.com/vote
2.	Kama una akaunti log in kama hauna akaunti basi bofya ‘register’  fuata hatua chache itakuelekeza 
3.	Ukisha login utaenda sehemu imeandikwa ‘Select Region’ Chagua Africa 
4.	Katika orodha chagua African’s Leading Tourist Attractions kisha kwenye kiduara bonyeza Pugu Hills Forest Reserve, Tanzania utakuwa umepiga Kura 
5.	Ukifanikiwa kupiga kura waweza kuweka comment yako hapo chini ili tuhamasishe zaidi watu kupiga kura, kura yako ushindi wetu by @localtourtz
2
5 months ago
Download
Moja ya maeneo muhimu sana unayotakiwa kuyatembelea ukiwa Iringa ni pamoja na Iringa Boma Regional Museum and Cultural Center hapa ni sehemu muhimu sana ya kuanzia utalii wako wa ndani ya Mkoa wa Iringa kwa kuwa utapata kuvifahamu vivutio vyote vya Mkoa huo kabla haujaanza ziara yako ya kitalii na eneo hili lenyewe tu ni kivutio.

Hii ni sehemu moja ya vivutio vya kihistoria na kitamaduni Iringa ambapo kuna historia na vitu vingi vya makumbusho vimehifadhiwa katika sehemu hii. Jengo hili lilijengwa enzi za ukoloni wa Wajerumani mwaka 1914 ambao lilikuwa hivyo mpaka mnamo mwaka 2016 ambapo palibadilishwa kuwa kituo cha makumbusho na utamaduni.

Karibu katika video hii fupi ambayo niliifanya nilipotembelea eneo hilo

Mtanzania Mwenzangu hakikisha unapofika Iringa unakuja na hapa, kuna mengi.

#localtourtz by @localtourtz
4
5 months ago
Download
Kwa mara ya kwanza katika Historia ndani ya Magofu ya Kaole pameanzishwa 'camping site' ambapo wewe raia mtanzania au wakigeni pamoja na Familia yako mnaweza kuja na kufurahia hii si ya kukosa, ukiwa hapo utapata viburudisho vya kutosha mpaka ushangae, usingoje niendelee kukusimlia tazama picha ili uone kulivyonoga.

Na hapa ilikuwa uzinduzi rasmi wa Kaole Ruins Campsite. by @localtourtz
0
6 months ago
Download
Na huu ni muendelezo hapa ni @chomawaterfalls milima ya uluguru Morogoro sehemu ambayo kuna mambo meengi sana ambayo kimsingi hautojutia kufika hapo, lengo la kufika hapo ilikuwa kukuletea vivutio kupitia matukio ambayo yatakuvuta ufike hapo

Huyu ni mdau wa utalii baada ya kusikia habari za Choma waterfalls nae akatia timu na hapa anatueleza kwa ufupi. Usingoje kusimuliwa fika mwenyewe

Endelea kufuatilia hapa 

#localtourtz by @localtourtz
0
6 months ago
Download
Hii inaitwa jipange mwenyewe kila kitu unapokwenda Tour, nilichofanya katika safari hii katika milima ya Uluguru nilibeba stand,mic na kamera. So nilianza kwa kupiga cuts kila hatua baadaye nikajirekodi na mwisho nikafinalize, endelea kufuatilia kuona tour hii. 

Mwisho nimemtaja Sam Paul insta yake hii @nsyukaphotographer huyu jamaa ndiye aliyenisihi nipite maeneo yote mtayaona katika clip zangu zijazo. Kuwa hapa

Sema neno kama ulisha wahi fika mto wa mawe, Peponi,Choma,Morning Sight na Kinsamvili Culture camp 

#localtourtz by @localtourtz
2
6 months ago
Download
Huyu Mwamba ni Boda Boda lakini kutokana na kwamba amekuwa akipeleka sana wageni huko milimani Moro sasa amekuwa ni mzuri sana katika kuwapa dondoo wageni wake za kitalii, nilimchukua clip hii nikiwa huko, hawa ni wadau muhimu wa utalii
#localtourtz by @localtourtz
1
6 months ago
Download
Nikiwa Iringa pamoja na wadau wengine wa utalii tulifanikiwa kufika Boma eneo ambalo ni la kihistoria na linalotoa fursa mbalimbali kushiriki urithi wa utamaduni wa Iringa.

 Ni mojawapo ya majengo ya zamani zaidi Iringa. Ilijengwa mwaka 1914 na Wajerumani kama hospitali ya kijeshi, kwa kutumia mtindo wa usanifu wa Kijerumani uliochanganya vipengele vya Kiafrika, Kiswahili na Ulaya.

 Baadaye Waingereza waliifanya kuwa kituo cha utawala hadi baada ya uhuru. Hii ni sehemu muhimu sana hasa utakapofika katika mkoa wa Iringa, kazi yangu ni moja tu kupiga picha na kukusogezea tukio ili na wewe upate hamasa ya kutembelea huko. Karibu Iringa Karibu Ufurahie Boma utapumzika na kujifunza mengi.

#localtourtz by @localtourtz
0
6 months ago
Download
Wadau Mbalimbali wametembelea Hifadhi ya Msitu wa Asili Pugu Kazimzumbwi ambao upo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) uliopo Kisarawe.

Wakiwa ndani ya Msitu huo ambao una Mazingira ya kuvutia, watalii hao wa ndani waliweza kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya matembezi ndani ya msitu #hiking ambapo waliweza kupata maelezo juu ya mimea mbalimbali na sifa zake yaani utalii wa Ikolojia, walifurahi kuiona Dar es Salaam na Mkoa Pwani walipofika View Point na pia waliweza kufurahia katika Bwawa la Minaki ambapo waliweza kupiga picha mbalimbali. 

Watalii hao wa ndani kwa nyakati tofauti walieleza kufurahishwa kwao na safari hiyo na kuahidi kuwa watakuwa mabalozi wa wengine kuhakikisha wanatembelea katika hifadhi hiyo by @localtourtz
2
2 years ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up