Instagram story viewer> @ngbfadventist> Posts
4.5K
followers
5
following
The Official Page of Nyanza Gold Belt Field Of Seventh-Day Adventist Church.
_____
Grounded in the Bible and Focused on The Mission.
Onevoice27!
_____
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Mambo yote mapya, tumaini linaanzia hapa!

“Tazama, nayafanya yote kuwa mapya.” — Ufunuo 21:5 by @ngbfadventist
0
13 days ago
Download
Mambo yote mapya, tumaini linaanzia hapa!

“Tazama, nayafanya yote kuwa mapya.” — Ufunuo 21:5 by @ngbfadventist
0
13 days ago
Download
Mambo yote mapya, tumaini linaanzia hapa!

“Tazama, nayafanya yote kuwa mapya.” — Ufunuo 21:5 by @ngbfadventist
0
13 days ago
Download
Kumbuka, kile Mungu alichokubariki nacho hakikupi sababu ya kujiona bora kuliko wengine. Kipaji, cheo, mali au mafanikio ni dhamana kutoka kwa Mungu, si kipimo cha thamani yako kuliko watu wengine. Endelea kuwa mnyenyekevu, maana baraka zako zinapaswa kuwagusa wengine, si kukufanya ujione zaidi yao.

Ujumbe huu umetolewa hii leo na @peter_msechu ambaye ametembelea Kanisa la Waadventista wa Sabato Chuo Kikuu

#mamboyotemapya #tumainilinaanziahapa by @ngbfadventist
22
a day ago
Download
USIKATE TAMAA, MUNGU BADO ANATAWALA! 

Hata safari ikiwa ngumu na majibu yakichelewa, usikate tamaa. Mungu hajakusahau; bado ana mpango na maisha yako. Endelea kumtumaini! 

📖 “Mkabidhi Bwana njia yako, pia umtumaini, naye atafanya.” — Zaburi 37:5

#MamboYoteMapya #TumainiLinaanziaHapa by @ngbfadventist
0
2 days ago
Download
Je, vyombo vya habari vinawezaje kusaidia Kanisa la Waadventista kuwafikia watu wengi zaidi kwa Injili?

Tarehe 8 Oktoba, mkutano wa LEAD uliwakutanisha viongozi wa kanisa na washiriki wa kawaida wakati wa Baraza la Mwaka la 2026, ili kujadili nafasi ya mawasiliano ya kidijitali katika kuendeleza utume wa Kanisa.

Chini ya kaulimbiu “Vyombo vya Habari kwa Ajili ya Utume” (Media for Mission), mada mbalimbali, mifano ya vitendo na mijadala shirikishi vilisisitiza umuhimu wa mawasiliano yanayozingatia mahitaji ya hadhira, uinjilisti wa kidijitali, usimulizi wa hadithi na mikakati ya kuwaunganisha watu wanaofikiwa mtandaoni na makanisa ya mahali husika.

Mkutano huo pia ulisisitiza ushirikiano wa kimataifa kupitia SautiMoja27, ukiwahimiza viongozi kutumia vyombo vya habari si kwa ajili ya kuongeza ushiriki pekee, bali pia kujenga mahusiano yenye maana na kueneza ujumbe wa Yesu.

#CalledForMission #AnnualCouncil2026 #adventistchurch #mamboyotemapya by @ngbfadventist
0
2 days ago
Download
Mungu hakuweka Sabato kwa sababu amechoka, bali kama zawadi ya kutupumzisha na kutukaribisha zaidi katika uwepo wake. 
Sabato inapoingia, weka simu yako pembeni, tuliza mawazo yako, jifunze Neno la Mungu na tafakari uzuri wa uumbaji wake.

Pumzika kutoka katika shughuli za dunia, ili upate muda zaidi wa kuwa karibu na Muumba wako.

#mamboyotemapya #tumainilinaanziahapa #allthingsnew by @ngbfadventist
0
2 days ago
Download
Pumzika. Omba. Mwamini Mungu. Hupaswi kubeba kila kitu peke yako, maana Yesu anakualika: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” — Mathayo 11:28.

🌅 Sabato Njema!
Mungu akupe amani moyoni, pumziko la kweli na nguvu mpya kwa ajili ya safari iliyo mbele yako. by @ngbfadventist
0
2 days ago
Download
Kuna mizigo ya maisha ambayo huwezi kuibeba peke yako. Usikate tamaa, wala usikubali uchovu wa moyo ukuondoe kwa Yesu. Mkabidhi yeye mizigo yako, maana kwake utapata pumziko, faraja na tumaini jipya.

Pumziko linaanzia hapa, kwa Yesu Kristo

#MamboYoteMapya #tumainilinaanziahapa by @ngbfadventist
2
3 days ago
Download
Zaidi ya viongozi 440 wa Kanisa la Waadventista wa Sabato kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekusanyika katika Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato, Silver Spring, Maryland, Marekani, kwa ajili mkutano wa Mkatano wa meisho wa mwaka-Annual Council 2026 ulioanza tarehe 7 Oktoba.

Chini ya kaulimbiu “Called for Mission” — “Tumeitwa kwa Utume,”** hafla hiyo imeangazia umoja wa kanisa la kimataifa, utamaduni na dhamira ya pamoja ya kutimiza utume wa Mungu. Hafla hiyo pia ilishuhudia mavazi ya kitamaduni na bendera kutoka zaidi ya nchi 200.

Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji. Erton Köhler, aliwakaribisha wajumbe, huku viongozi wa kanisa wakisisitiza umuhimu wa uaminifu, maombi na kujitoa katika utume wa kanisa.

Mkutano huo wa siku nane utahusisha taarifa, majadiliano na masasisho kuhusu kazi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato ulimwenguni kote.

📲 Fuata mikutano mubashara kupitia YouTube: @gcadventistchurch

#CalledForMission #AnnualCouncil2026 #AdventistChurch #TumeitwaKwaUtume

AdventistChurch by @ngbfadventist
6
3 days ago
Download
“Kwa Mungu yote yawezekana.” — Mathayo 19:26

Leo, kwa nini unaogopa kile unachopitia? 
Mkabidhi Mungu kila kitu.

Mambo yote mapya—Tumaini linaanzia hapa. by @ngbfadventist
1
4 days ago
Download
MWILI UMEFUNGAMANISHWA NA HALI YA DHAMBI…

Tangu anguko la mwanadamu, asili ya mwanadamu imeathiriwa na dhambi. Ndiyo maana tunajikuta tukitamani mema, lakini wakati mwingine tunafanya yale tusiyoyataka.

Lakini habari njema ni kwamba dhambi si mwisho wa mwanadamu.
Katika Kristo, kuna msamaha, mabadiliko, na tumaini la maisha mapya.

Hatuwezi kuushinda mwili kwa nguvu zetu wenyewe; tunamhitaji Kristo kila siku.

“Kwa maana katika mwili wangu halikai neno jema…” — Warumi 7:18 by @ngbfadventist
4
4 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up