Instagram story viewer> @ngome_media> Posts
44
posts
8.1K
followers
0
following
Ukurasa rasmi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Official Tanzania Peoples’ Defence Forces Page(TPDF)
Kikombo
P.O.Box 194,Dodoma
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Simulizi hii ya Mashujaa wa Vita ya Kagera ipo kwenye ukurasa wetu wa Youtube by @ngome_media
0
33 minutes ago
Download
Brigedia Jenerali Wilfred Kabunda(Mstaafu) akisimulia jinsi alivyoshiriki katika Vita ya Kagera, simulizi kamili inapatikana kwenye ukurasa wetu wa Youtube. by @ngome_media
0
7 hours ago
Download
Matukio katika Picha katika kumbukumbu ya Mashujaa by @ngome_media
7
13 hours ago
Download
Matukio mbalimbali katika picha kwenye maadhimisho ya siku ya Mashujaa by @ngome_media
5
13 hours ago
Download
Matukio mbalimbali katika picha kutoka viwanja vya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi, ambako yamefanyika Mahafali ya Kozi ya 14 ya chuo hicho.Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho.📸: @masimba_tz by @ngome_media
3
2 days ago
Download
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amewataka wahitimu wa Kozi ya 14 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutumia maarifa waliyoyapata kwa uzalendo, hususan katika usimamizi wa sera za nchi.Akizungumza leo Julai 23, 2026 wakati wa mahafali ya kozi hiyo yaliyofanyika Kunduchi, Dar es Salaam, Dkt. Nyansaho amesema bila kutekeleza wajibu huo, Taifa linaweza kuathirika.Amesema licha ya NDC kuwa na misingi ya kijeshi, chuo hicho huchukua wanafunzi wa aina zote wakiwemo wanajeshi, watumishi wa taasisi za Serikali, wizara na raia ambao wana wajibu wa kulilinda Taifa wakati mwingine bila hata ya kutumia silaha, kwa kuwa ulinzi wa Taifa ni jukumu la kila mmoja.Amesisitiza kuwa wahitimu hao wanapaswa kutumia maarifa waliyopata kuangazia masuala ya ulinzi wa Taifa katika sekta mbalimbali na kutekeleza wajibu wao kwa nia moja. by @ngome_media
8
2 days ago
Download
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka wahitimu wa Kozi ya Usalama na Stratejia wa Chuo Cha Ulinzi wa Taifa Tanzania kuitumia vizuri elimu waliyoipata ili ku dumisha usalama na kukuza uchumi wa Taifa. Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Rhimo Nyansaho(Mb) amesema kuwa nchi yoyote yenye uchumi unaokua kwa kasi huchangiwa na wasomi wa masuala ya Usalama na Stratejia.Aidha, Mkuu wa chuo hicho Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge amemuhakikishia Waziri wa Ulinzi kuwa wahitimu hao wamepatiwa elimu bora inayokubalika duniani kote. Kozi hiyo imejumuisha wahitimu 72 kutoka Mataifa 17 ambayo ni Bangladesh, Burundi, Botswana, Rwanda, Uganda, Kenya, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Nigeria, India, Ethiopia, Namibia, Afrika Kusini, Sierra Leone, Misri na mwenyeji Tanzania. by @ngome_media
0
2 days ago
Download
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda, akiwa katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Kunduchi, Dar es Salaam, ambako yanafanyika mahafali ya Kozi ya 14 leo Julai 23, 2026.Fuatilia matangazo haya pamoja na kurasa zetu za Instagram na Facebook za TBC Online kwa taarifa na matukio mbalimbali ya hafla hii.📸: @masimba_tz by @ngome_media
2
3 days ago
Download
“Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi(CDF CUP) yanaimarisha umoja”-Jenerali Jacob John Mkunda,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. by @ngome_media
4
3 days ago
Download
 by @ngome_media
1
3 days ago
Download
 by @ngome_media
1
3 days ago
Download
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi amewasihi watanzania kudumisha AmaniMkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Jacob John Mkunda amewasihu Wanajeshi na Wananchi kushirikiana katika kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa salama kwani ulinzi wa nchi ni jukumu la kila mtanzania.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga Michezo ya Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi 2026,Jenerali Mkunda amesisitiza kuwa Umoja na ushirikiano baina ya wanajeshi na raia ndiyo msingi wa utulivu nchini huku akiwashukuru watanzania kwa namna wanavyotoa ushirikiano kwa JWTZ wakati wote linapotekeleza majukumu yakeAidha, Jenerali Mkunda amesema kuwa ushirikiano huo unaweza kuimarishwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kushirikiana katika Michezo mbalimbali huku akiwataka makamanda vikosi kuhakikisha wanakuza vipaji vya wanamichezo vitakavyotoa mchango kwa timu za taifa. Mashindano hayo yalikuwa na michezo 13 ambapo JKT imeibuka kidedea kwa kuwa Mshindi wa jumla ikifuatiwa na Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu. Mashindano hayo ambayo yalikuwa na kauli mbiu ya Umoja,Amani na Mshikamano kwa Ujenzi wa Taifa imara yamehitimishwa Julai 22, katika viwanja vya Azam Complex Chamazi jijini Dar Es Salaam. by @ngome_media
1
3 days ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up