Posted On: October 28th 2021, 06:43 am
#TuzoNo1Leo nimetunukiwa tuzo yangu ya kwanza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Zainab Chaula kama Mwanafunzi bora wa kike mbunifu katika sekta ya Habari Mawasiliano na tecknilojia ( Best Innovative female Student in ICT).
Tuzo hizi ziligaiwa Katika mkutano mkubwa wa tano wa kitaifa wa mwaka 2021 ( 5th TAIC 2021) ulioandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano na Tecknolojia ya habari jijini Arusha Ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Waziri Mkuu wa nchi Mhe. kassim Majaliwa Majaliwa.
Ni furaha kubwa sana kwangu pamoja na team yangu nzima ya
#SarataniAI .Tuzo hii inazidi kunipa nguvu na Chachu ya kuongeza jitigada za kuendelea kutoa elimu ya afya kwa vijana hasa katika kutumia technologia katika sekta ya Afya.
Nipende kuishukuru wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari kwa kuandaa tuzo hizi na kutambua uwepo wa vijana wanaopaza sauti na kuunda mifumo ya kitechnologia itakayosaidia katika kutoa huduma za afya na kujenga Taifa la kidigitali.🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Tuijenge Tanzania ya Kidigitali 💪
.
.
.
#ict2021 #ictawards2021#sisiniwaletunaosaidiwanabwana🙏
Load More