*ODERO AMVAA LEMA, WANAHARAKATI: “MSIHUJUMU MARIDHIANO YA TAIFA”*
- Asema mashambulizi kwa wakili wa Tundu Lissu na kupinga mazungumzo ni dalili ya siasa za migawanyiko
Na Mwandishi Wetu
Mwanachama wa CHADEMA Odero Charles Odero ameibuka na kuwakosoa vikali Godbless Lema pamoja na baadhi ya wanaharakati akiwatuhumu kuhujumu juhudi za maridhiano ya kitaifa yanayolenga kurejesha amani, haki na mshikamano nchini.
Odero ambaye aliwahi kugombea uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi uliowashindanisha na Tundu Lissu na Freeman Mbowe, alisema kinachoendelea ndani na nje ya chama kinaashiria mgawanyiko unaoweza kudhoofisha juhudi za kisiasa na mustakabali wa taifa.
*AKEMEA MASHAMBULIZI KWA WAKILI WA LISSU*
Katika tamko lake, Odero alilaani mashambulizi dhidi ya Wakili Paul Kisabo, akidai baadhi ya makada wa CHADEMA na wanaharakati wamekuwa wakimshambulia kutokana na msimamo wake katika mchakato wa mazungumzo.
Alisema hatua hiyo si tu haikubaliki bali inaonesha ukosefu wa nidhamu ya kisiasa na kuhatarisha mafanikio ya maridhiano.
*“MAZUNGUMZO SI YA MTU MMOJA”*
Odero alisisitiza kuwa mazungumzo ya maridhiano hayawezi kuangaliwa kwa jicho la mtu au kundi fulani, bali ni mchakato mpana wa kitaifa unaohitaji uvumilivu na mshikamano.
“Haya si mazungumzo ya mtu mmoja au chama kimoja, ni kwa mustakabali wa nchi nzima,” alieleza.
Aliongeza kuwa Tundu Lissu ameonesha ujasiri wa kisiasa kwa kuweka mbele maslahi ya taifa kuliko misimamo mikali ya kisiasa.
*AONYA SIASA ZA HOFU NA MIGAWANYIKO*
Kwa mujibu wa Odero, wanaopinga juhudi za maridhiano bila hoja za msingi wanachochea siasa za hofu na mivutano badala ya kujenga matumaini kwa wananchi.
Alisema mwenendo huo unaweza kuendeleza machafuko ya kisiasa na kuchelewesha kupatikana kwa suluhisho la kudumu la kitaifa.
*AITAKA CHADEMA IJITENGA NA WANAHARAKATI*
Katika hatua nyingine, Odero alipendekeza CHADEMA ijitenganishe wazi na wanaharakati wa nje, akisema kuna hatari ya taasisi ya kisiasa kupoteza mwelekeo wake inapovamiwa na ajenda za activism.
“Si sahihi activists kuingia kwenye taasisi ya kisiasa na kuiteka, chama lazima kijikite kwenye siasa zake,” alisisitiza.
*KIPAUMBELE: UHURU WA LISSU*
Odero alielekeza