Instagram story viewer> @katibanasheria_> Post
6 months ago
Co Creator: zainabkatimba
3
Posted On: April 27th 2026, 02:02 pm
Tagged Users:
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. @zainabkatimba, leo Aprili 27, 2026 Mkoani Morogoro amefungua kikao kazi cha uhakiki na uthibitishaji wa rasimu ya taarifa ya hali ya haki za binadamu kwa mzunguko wa nne wa Mfumo wa Mapitio ya Kipindi Maalum (UPR)

Mhe. Katimba amesema kuwa Tanzania imeendelea kupiga hatua katika kukuza, kulinda na kuendeleza haki za binadamu kupitia utekelezaji wa mapendekezo ya kimataifa pamoja na juhudi za ndani za serikali.

Ameeleza kuwa mafanikio hayo yamechangia kuimarisha amani, mshikamano na utulivu nchini, huku akisisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda haki za msingi kwa kuzingatia sheria, sera na mikakati mbalimbali bila ubaguzi.

Aidha, amebainisha kuwa Tanzania imekubali kutekeleza mapendekezo 187 yaliyotokana na ahadi ya kitaifa mbele ya jumuiya ya kimataifa, hatua inayolenga kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya taifa.
Katimba amewahimiza wataalamu kuhakikisha wanaandaa taarifa yenye ubora na takwimu sahihi zinazoakisi hali halisi ya utekelezaji wa haki za binadamu.
Comments (3)
sunday.godfrey 6 months ago

sunday.godfrey

❤️❤️❤️

cars_u_deserve 6 months ago

cars_u_deserve

Get the perfect car service from us

More posts

back to up