Posted On: May 18th 2026, 07:38 pm
TRA imeeleza kuwa inaendelea kulinda viwanda vya ndani ili kuongeza wigo wa kodi kwa kupambana na uingizaji holela wa bidhaa nchini. Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Mkuu wa TRA alipokutana na uongozi wa Mount Meru Group, kampuni inayozalisha mafuta ya kupikia ya alizeti na pamba.
TRA imesisitiza kuwa inathamini mchango wa viwanda vya ndani katika mapato ya taifa na itaendelea kuvihamasisha pamoja na wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari. Kampuni ya Mount Meru Group imepongeza juhudi za TRA katika kudhibiti magendo ya mafuta ya kupikia yanayodhoofisha viwanda vya ndani na kupunguza ushindani wa soko.
Pia, Mount Meru Group imesema udhibiti wa magendo umeongeza nguvu kwa viwanda vya ndani na kuhakikisha usalama wa afya za wananchi, huku ikiipongeza TRA kwa mfumo wake wa kodi unaotabirika unaomwezesha mlipakodi kupanga malipo yake kwa ufanisi.
#digitalnewstzupdate