Instagram story viewer> @digitalnewstz_> Posts
31.7K
followers
70
following
| Ukurasa rasmi wa Instagram wa Digital News | The Official Instagram account of Digital News | #NewsWithUs🌍 | #SisiNaHabari |
Time: 24hrs🎙️
POSTS STORIES REELS TAGGED
 by @digitalnewstz_
0
16 days ago
Download
 by @digitalnewstz_
0
16 days ago
Download
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeelekeza kuwepo kwa mpango madhubuti wa kudhibiti na kusimamia Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam, ili kupunguza athari za kimazingira na kulinda afya za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Maelekezo hayo yametolewa leo, Oktoba 17, 2026, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Pius Zebhe Yanda (Mb), wakati wa ziara ya kukagua hali ya mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi na Mto Ng’ombe, iliyolenga kutathmini utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, Septemba 18, 2026.

Prof. Yanda amesisitiza umuhimu wa kutathmini afya za wananchi wanaoishi karibu na dampo hilo, pamoja na kuweka uzio utakaosaidia kudhibiti upanuzi wa makazi kuelekea eneo la dampo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Reuben Kwagilwa, amesema Serikali inapaswa kupata mwekezaji atakayeshughulikia uchakataji wa taka katika Dampo la Pugu ili kuboresha usimamizi wake na kupunguza athari za kimazingira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Aidha, ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushirikiana kwa karibu na taasisi zote zinazohusika, ikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kuhakikisha mradi wa dampo hilo unatekelezwa bila kukwama.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya mazingira mkoani humo, amesema Dar es Salaam ina eneo la takribani kilomita za mraba 1,300 na wakazi zaidi ya milioni 5.3 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Amesema ongezeko la watu na uzalishaji mkubwa wa taka kwa siku, pamoja na changamoto za miundombinu, vimechangia kiasi kidogo cha taka kufikishwa dampo, hali inayohitaji kuimarishwa kwa mifumo ya ukusanyaji, usafirishaji na uchakataji wa taka. by @digitalnewstz_
0
a day ago
Download
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinatarajia kufanya Kongamano la Saba la Biashara na Maendeleo ya Uchumi jijini Mwanza, likilenga kujadili matokeo ya tafiti, ubunifu, teknolojia na fursa za kukuza biashara na uchumi.

Kongamano hilo linatarajiwa kushirikisha wadau takribani 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania, kwa lengo la kubadilishana maarifa na kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili wafanyabiashara, hususan wajasiriamali wadogo na wa kati.#digitalnewstzupdate by @digitalnewstz_
0
a day ago
Download
SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limesema limeongeza mapato yake kutoka Sh bilioni 1.3 kwa mwaka 2018/19 hadi Sh bilioni 147.8 katika mwaka 2025/26, likieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na mageuzi ya kiutendaji, uwekezaji katika miradi ya kimkakati na kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika sekta ya madini.

Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. CPA Venance Mwasse, amesema hayo wakati akizungumza katika kikao kazi kati ya shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari, ambapo alieleza mikakati na mafanikio ya shirika pamoja na mipango ya kuongeza mchango wake katika uchumi wa taifa.

“Wakati tunaingia, mapato ya ndani ya shirika yalikuwa Sh bilioni 1.3 kwa mwaka mzima. Leo hii tunapozungumza, kwa hesabu zinazomalizika mwaka 2025/26, mapato yote ni Sh bilioni 147.8,” amesema Mwasse.

Amesema shirika hilo ambalo awali lilikuwa likitegemea fedha za Serikali kwa asilimia 89, sasa limeweza kujitegemea katika kulipa mishahara ya wafanyakazi wake, huku likiendelea kuchangia mapato ya Serikali kupitia gawio.

“Kwa sasa huu ni mwaka wa nne tangu tuache kutegemea Serikali, na huu ni mwaka wa tatu tunajilipa wenyewe mishahara. Tangu shirika lianzishwe mwaka 1972, tumekuwa na faida na kutoa gawio kwa Serikali, ambapo hadi sasa tumeshatoa Sh bilioni 11,” amesema.

Mwasse amesema STAMICO pia imewekeza katika miradi ya kimkakati ikiwemo uchorongaji wa miamba kwa ajili ya utafiti wa madini, ambapo idadi ya mitambo imeongezeka kutoka mitatu hadi 18 ya kisasa, huku shirika likihudumia wateja mbalimbali katika sekta hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amelitaka shirika hilo kuendelea kuwekeza katika utafiti, ubunifu na matumizi ya takwimu za kisasa ili kuongeza tija na kuimarisha mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa.

Balile amesema mafanikio ya STAMICO yanapaswa kuambatana na utafiti endelevu unaozingatia mabadiliko ya teknolojia na mazingira ya biashara, badala ya kutegemea takwimu za miaka iliyopita wakati sekta inaendelea kubadilika. by @digitalnewstz_
0
2 days ago
Download
Wananchi mkoani Tabora wamehimizwa kujiunga na huduma ya umeme na kutumia nishati safi ya kupikia, ikiwemo majiko ya umeme, kwa lengo la kuboresha afya, kutunza mazingira na kuinua maisha yao ya kila siku. Rai hiyo imetolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia ziara ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu miradi ya nishati vijijini.

Kupitia ziara hiyo, wananchi wanapatiwa elimu kuhusu taratibu za kuomba kuunganishiwa umeme, matumizi sahihi na yenye tija ya nishati, pamoja na tahadhari za kiusalama wanazopaswa kuzingatia wanapotumia umeme majumbani na katika shughuli za kiuchumi. Aidha, wanahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kupunguza athari za kiafya zinazotokana na moshi na uchafuzi wa mazingira.

Vilevile, wananchi wametakiwa kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa kwa kukumbatia nishati safi ya kupikia, pamoja na kushiriki katika kutunza miundombinu ya umeme. Juhudi hizo za REA zinalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za nishati vijijini na kuhakikisha nishati inatumika kwa usalama, ufanisi na kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira.
#DigitalnewstzUPDATES by @digitalnewstz_
0
4 days ago
Download
Wananchi mkoani Tabora wamehimizwa kujiunga na huduma ya umeme na kutumia nishati safi ya kupikia, ikiwemo majiko ya umeme, kwa lengo la kuboresha afya, kutunza mazingira na kuinua maisha yao ya kila siku. Rai hiyo imetolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia ziara ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu miradi ya nishati vijijini.

Kupitia ziara hiyo, wananchi wanapatiwa elimu kuhusu taratibu za kuomba kuunganishiwa umeme, matumizi sahihi na yenye tija ya nishati, pamoja na tahadhari za kiusalama wanazopaswa kuzingatia wanapotumia umeme majumbani na katika shughuli za kiuchumi. Aidha, wanahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kupunguza athari za kiafya zinazotokana na moshi na uchafuzi wa mazingira.

Vilevile, wananchi wametakiwa kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa kwa kukumbatia nishati safi ya kupikia, pamoja na kushiriki katika kutunza miundombinu ya umeme. Juhudi hizo za REA zinalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za nishati vijijini na kuhakikisha nishati inatumika kwa usalama, ufanisi na kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira.
#DigitalnewstzUPDATES by @digitalnewstz_
0
4 days ago
Download
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, amewapongeza wanachama wa Umoja wa Maendeleo ya Kiluvya (KIUMA) kwa kudumisha umoja na mshikamano unaowawezesha kusaidiana katika changamoto za kijamii.

Magoti ametoa pongezi hizo leo Oktoba 14, 2026 wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya KIUMA yaliyofanyika Kiluvya, ambapo amewashauri wanakikundi kuanzisha akaunti maalumu ya kuweka akiba kwa ajili ya kutekeleza mipango yao ya maendeleo.

Amesema umoja huo ni mfano wa ushirikiano katika jamii na kusisitiza umuhimu wa wanachama kuendelea kulinda mshikamano wao ili uweze kuzaa matunda zaidi katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

“Mkifungua akaunti hata kesho, nitachangia Sh. 500,000 kuwaunga mkono ili muendelee na mshikamano mlionao,” amesema Magoti.

Aidha, amesema ziara ya Waziri wa Ujenzi imezaa matunda kwa kuwa eneo hilo limehakikishiwa kuanzishwa kwa huduma za daladala katika njia ya Kisarawe–Kiluvya, sambamba na mpango wa kukarabati na kuboresha barabara hiyo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutafuta eneo la kujenga kituo cha huduma za pamoja (One Stop Centre) kitakachowezesha wananchi kupata huduma mbalimbali za Serikali karibu na makazi yao, badala ya kusafiri hadi Kisarawe mjini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa KIUMA, Mathew Msami, amesema umoja huo ulianzishwa kwa lengo la kuwakutanisha watu wenye dhamira ya kusaidiana, kushirikiana na kujenga maendeleo ya pamoja, hasa wakati wa misiba na changamoto nyingine za kijamii.

Amesema kaulimbiu ya umoja huo, “Jirani Yako ni Ndugu Yako,” inaakisi falsafa ya upendo, mshikamano, uaminifu na kujitolea kwa wanachama katika kuhakikisha hakuna mwanachama anayekabiliwa na changamoto peke yake.

Msami amesema katika kipindi cha miaka mitatu, KIUMA imepata mafanikio mbalimbali, yakiwemo kuimarika kwa uwezo wa kuchangia, uwazi katika usimamizi wa fedha na kujenga mahusiano mazuri miongoni mwa wanachama. by @digitalnewstz_
0
4 days ago
Download
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewahimiza vijana wajasiriamali nchini kuzingatia viwango na ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuongeza ushindani katika soko na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana nchini na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa na Afisa Masoko Mwandamizi wa TBS, Deborah Haule, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua mkoani Rukwa, ambapo TBS inashiriki kutoa elimu kuhusu viwango, ubora na usalama wa bidhaa.

Bi. Haule amesema maadhimisho hayo yamekuwa fursa muhimu kwa TBS kukutana na vijana, hususan wajasiriamali, kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kuzingatia viwango katika uzalishaji na kuwafahamisha huduma zinazotolewa na Shirika ili kuwawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko.

Ameeleza kuwa Serikali imeweka utaratibu wa kuwawezesha vijana wajasiriamali wanaostahili kupata huduma ya upimaji wa sampuli za bidhaa bila malipo, kwa lengo la kuwasaidia kutambua ubora wa bidhaa zao na kuboresha uzalishaji.

“Tunawahimiza vijana wajasiriamali wenye bidhaa wanazozalisha kutumia fursa hii kwa kufika katika ofisi za TBS ili kupata maelekezo na huduma zinazowawezesha kuthibitisha ubora wa bidhaa zao,” amesema Bi. Haule.

Aidha, amesema maabara za TBS zinafanya kazi kwa kuzingatia mahitaji ya umahiri wa kimataifa, jambo linalosaidia kuhakikisha matokeo ya vipimo yanaaminika na kukubalika kulingana na taratibu na makubaliano husika.

Ameongeza kuwa TBS ina ofisi katika kanda mbalimbali nchini zinazotoa huduma na elimu kuhusu viwango, hivyo kuwataka vijana kuendelea kutembelea ofisi hizo hata baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo ili kupata ushauri na mwongozo kuhusu ubora wa bidhaa na huduma za Shirika.

Akizungumzia kaulimbiu ya maadhimisho hayo, “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana,” Bi. Haule amesema TBS inaendelea kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha vijana wanapata elimu inayowawezesha kuzingatia viwango, ubora na usalama wa bidhaa wanapochangamkia fursa za biashara na ujasiriamali. by @digitalnewstz_
0
5 days ago
Download
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, ametoa wito kwa Viongozi wakiwemo wa Halmashauri na NEMC kushirikisha wananchi kikamilifu katika kupanga na kusimamia mifumo ya ukusanyaji taka, elimu ya usafi wa mazingira kuimarishwa na Sheria  kusimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha mazingira ya Mto Ng’ombe yanakuwa safi na salama.

Waziri Masauni ametoa maagizo hayo Oktoba 11, 2026, wakati wa ziara ya kikazi katika eneo la Mto Ng’ombe, Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kukagua hali ya mazingira na kuimarisha usimamizi wa taka.

Aidha, Mhe. Masauni amesisitiza umuhimu wa kuendeleza zoezi la usafi wa mazingira, ikiwemo kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, ili kujenga utamaduni wa usafi na uwajibikaji miongoni mwa wananchi.

Vilevile, ameelekeza hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya wanaokiuka Sheria na Kanuni za mazingira, wakiwemo wakandarasi wa ukusanyaji taka wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ili kuhakikisha huduma hiyo inatolewa kwa ufanisi.

Katika hatua nyingine, Waziri Masauni amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa juhudi zake za kulinda mazingira, huku akihimiza ushirikiano kati ya baraza hilo, wananchi, mamlaka za serikali za mitaa na wadau wengine katika kuboresha usimamizi wa taka kwa manufaa ya jamii na vizazi vijavyo. by @digitalnewstz_
0
6 days ago
Download
Tanzania 🔥🔥🔥🇹🇿 by @digitalnewstz_
0
8 days ago
Download
 by @digitalnewstz_
0
8 days ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up