Posted On: July 19th 2026, 03:36 am
SHUKRANI KWA WACHANGIAJI WOTE WA PROUD FOUNDATION🙏.
Kwa niaba ya Proud Foundation, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kila mmoja wenu aliyechangia kwa moyo wa upendo katika jitihada zetu za kuwasaidia watoto wa mitaani.
Tukio letu la Kujitolea lililofanyika tarehe 18/07/2025, eneo la Magufuli, Kijazi - Ubungo, Dar es Salaam, limekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano wenu.
Mchango wenu wa mavazi na vitu vingine umeleta faraja kubwa kwa watoto hawa, na umeonesha jinsi ubinadamu unavyoweza kubadilisha maisha ya wengine hata kwa hatua ndogo.
Hatuwezi kufanya haya bila ninyi. Asanteni kwa kuwa sehemu ya safari hii ya kuwapa matumaini watoto wetu.
Mungu awabariki sana!.
@proudfoundationtz#ProudFoundationTZ #TuwasaidieWatotoWaMtaani
#UbungoDarEsSalaam #TogetherWeCare