Posted On: July 23rd 2026, 07:55 pm
📢 TAARIFA RASMI – VIJANA MARATHON RUANGWA 2026
Tunawashukuru wanachama wote kwa ushiriki wao katika kikao cha maandalizi. Baada ya kikao hicho, viongozi wa muda waliopatikana ni:
• Mwenyekiti: Sadal
• Katibu: Maulale
• Afisa Habari: Shadah Amepiga Tena
Aidha, kutaundwa Kamati Maalumu ya Maandalizi na Usimamizi wa shughuli zote za Vijana Marathon Ruangwa 2026.
Lengo letu ni kuunganisha vijana kupitia michezo, burudani na shughuli za kijamii, pamoja na kufikisha msaada kwa jamii yenye uhitaji.
Siku ya tamasha kutakuwa na:
⚽ Mechi ya kirafiki:
Team Hussein Stationery 🆚 Team Rama Katara
🎶 Burudani kutoka kwa wasanii, ma-DJ, wachekeshaji na vipaji mbalimbali.
🏃 Vijana Marathon pamoja na michezo mbalimbali ya ushindani kama vile:
• Kukimbia na gunia
• Kukimbiza kuku
• Michezo mingine ya burudani
🏆 Washindi wa mashindano mbalimbali watapata zawadi.
Tarehe, ratiba kamili na taarifa nyingine zitatolewa baada ya kikao kijacho.
Pamoja tunaweza kuleta mabadiliko chanya kwa jamii yetu.
Imetolewa na:
Shadah Amepiga Tena
Afisa Habari – Vijana Marathon Ruangwa 2026