Posted On: July 24th 2026, 05:00 pm
Makamu wa Rais wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema endapo angepata nafasi ya kutoa ujumbe mmoja wa mwisho kwa Watanzania, angewataka wapambane ili kupata Katiba Mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Nchimbi amesema mjadala wa Katiba Mpya umedumu kwa zaidi ya miaka 40.
Amesema Katiba Mpya inayopatikana inapaswa kuwa ya mwafaka na kudumu kwa muda mrefu, huku akisisitiza kuwa mchakato huo unapaswa kulenga kuijenga Tanzania na kuipeleka mbele.
“Pambaneni mpate Katiba Mpya itakayodumu miaka 50, yenye mwafaka katika Taifa, itakayotupeleka mbele miaka 50,” amesema Nchimbi.