Instagram story viewer> @aboodmediatz> Posts
14697
posts
80.2K
followers
35
following
Abood Media Official instagram Account
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Mvutano wa kifamilia umeibuka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, baada ya ndugu wa marehemu Wambura Mambiya (54) na mke wake kutofautiana kuhusu mahali ambapo mwili wa marehemu unapaswa kuzikwa.

Marehemu ambaye amefariki baada ya kuugua kwa muda, amezua mzozo baada ya mke wake mkubwa, Elizabeth Nyakao, kudai kuwa ndugu wa marehemu walikuwa wamepanga kuuchukua mwili huo na kuuzika kwa mke mdogo bila yeye kushirikishwa.

Akizungumza nje ya hospitali hiyo, Elizabeth amesema ameishi na marehemu kwa zaidi ya miaka 32 na wana watoto watano, huku akidai kuwa anapaswa kushirikishwa katika maamuzi ya mazishi ya mume wake.

Kwa upande wake, kaka wa marehemu na msemaji wa familia, Gradson Mambiya, amesema marehemu aliwahi kutoa maelekezo kwa ndugu zake kuwa angependa kuzikwa nyumbani kwa mke mdogo.

Hata hivyo, amesema familia imependekeza mwili uzikwe nyumbani kwao Musoma ili kumaliza mvutano huo na kuunganisha pande mbili za familia.

Akizungumzia suala hilo, Dativa Wenslaus kutoka Kitengo cha Utafiti wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza (SIMAUJATA), ametoa wito kwa wanandugu kutafuta suluhu kwa amani na kuzingatia taratibu za kisheria katika masuala ya mirathi na mazishi. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara na kuacha utupaji wa taka hovyo.

Akizungumza wakati wa kampeni ya kuhamasisha usafi wa mazingira katika maeneo ya biashara na makazi Magogoni, Kata ya Tungi, Dalmia amepiga marufuku ujenzi holela wa maeneo ya kutupia taka na biashara katika maeneo yasiyo rasmi.

Amesema wananchi wanapaswa kuhakikisha mifereji inasafishwa kwa wakati na wakandarasi wanakusanya taka kwa wakati, ili kuweka Kigamboni katika mazingira safi na yenye mpangilio. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ametangaza vita dhidi ya madanguro na vitendo vya ukiukwaji wa maadili, akisema Serikali haitamvumilia mtu yeyote anayewatumia watoto katika vitendo vya unyanyasaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mpogolo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwakamata watuhumiwa wa vitendo hivyo, akisema hatua hizo zimezuia madhara zaidi kwa jamii.

Amesema mtu mmoja anayedaiwa kuwatumia watoto wa kike katika vitendo vya udhalilishaji kwa malipo amekamatwa katika Kata ya Zingiziwa, huku uchunguzi ukiendelea.

Mpogolo amewataka viongozi wa mitaa na wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kutokomeza vitendo hivyo, akisisitiza kuwa umaskini si sababu ya kuwahusisha watoto au wanawake katika vitendo vinavyodhalilisha utu. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Wafanyabiashara wa Soko la Mawenzi mkoani Morogoro wamegoma kufungua biashara zao kwa saa kadhaa, wakipinga kodi ya pango la vizimba wanayodai ni kubwa.

Wafanyabiashara hao wanataka kodi hiyo ishushwe kutoka shilingi 10,000 hadi shilingi 8,000 kwa mwezi, huku wakilalamikia pia miundombinu mibovu na utitiri wa ushuru wa mizigo.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, amefika sokoni hapo na kuzungumza na wafanyabiashara hao, akiahidi kuyafanyia kazi malalamiko yao.

Baada ya ahadi hiyo, wafanyabiashara wamekubaliana kusitisha mgomo na kuendelea na shughuli zao huku wakisubiri majibu ya Serikali. by @aboodmediatz
2
a day ago
Download
Baraza la Vyama vya Siasa limeazimia kushirikiana na Serikali katika kuibua miradi ya maendeleo ya kiuchumi kwa lengo la kuongeza mapato na kuleta manufaa kwa jamii.

Azimio hilo limetolewa mkoani Morogoro wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika kwa ajili ya kuchagua viongozi wapya.

Juma Ali Khatibu amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, huku John Mongela, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichaguliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti.

Akizungumza baada ya uchaguzi, Juma Ali Khatibu amesema Baraza hilo halitajikita katika siasa pekee, bali litaendelea kujenga mahusiano kati ya Serikali na wadau wa demokrasia. Pia ameitaka Serikali kuangalia upya zuio la mikutano ya vyama vya siasa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa AAFP, Said Sudi Saidi, ametoa wito kwa Serikali na vyama vya siasa kutatua migogoro yao kwa njia ya mazungumzo, huku Katibu Mkuu wa UDP, Saumu Rashidi, akilipongeza Baraza hilo kwa kuwawezesha wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Makamu wa Rais wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema endapo angepata nafasi ya kutoa ujumbe mmoja wa mwisho kwa Watanzania, angewataka wapambane ili kupata Katiba Mpya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Nchimbi amesema mjadala wa Katiba Mpya umedumu kwa zaidi ya miaka 40.

Amesema Katiba Mpya inayopatikana inapaswa kuwa ya mwafaka na kudumu kwa muda mrefu, huku akisisitiza kuwa mchakato huo unapaswa kulenga kuijenga Tanzania na kuipeleka mbele.

“Pambaneni mpate Katiba Mpya itakayodumu miaka 50, yenye mwafaka katika Taifa, itakayotupeleka mbele miaka 50,” amesema Nchimbi. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Makamu wa Rais wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema Rais Samia Suluhu Hassan anataka mchakato wa kupata Katiba Mpya ukamilike kabla ya mwaka 2030.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, jijini Dar es Salaam, Nchimbi amesema Rais Samia analitaka suala hilo litekelezwe.

Amesema mjadala wa Katiba Mpya umedumu kwa zaidi ya miaka 40, huku akieleza kuwa Tume ya Haki Jinai pia ilishauri Katiba Mpya ipatikane kabla ya uchaguzi wa mwaka 2030. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kutokubaliana kati ya Serikali na Watetezi wa Haki za Binadamu katika baadhi ya masuala si ugomvi wala dhambi, bali ni sehemu ya jamii ya kidemokrasia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Nchimbi amesema mitazamo tofauti inasaidia kujenga mijadala na hoja zenye tija.

Amesema si lazima Serikali na Watetezi wa Haki za Binadamu wakubaliane kila jambo, akisisitiza kuwa jamii ambayo watu wake wanakubaliana kila kitu bila kuwa na mawazo tofauti hupoteza nafasi ya kujadiliana na kujenga hoja.

“Ikifika mahali mnakubaliana pamoja, mnakwenda pamoja, nyinyi si binadamu, mnakuwa roboti,” amesema Nchimbi. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema anatamani kuona Watanzania wenye mitazamo tofauti wakikaa pamoja na kujadili masuala ya kitaifa kwa amani bila uhasama wala uadui.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), jijini Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi amesema tofauti za mawazo zinapaswa kutumika kujenga taifa lenye kuheshimu haki, amani na demokrasia.

Amesisitiza umuhimu wa Watanzania kutumia nafasi walizonazo kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa, akisema kusimamia haki ni msingi wa kudumisha amani nchini. by @aboodmediatz
11
a day ago
Download
Benki ya CRDB imeanza mpango wa kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kutoa bajaji kwa mfumo wa mkopo mkoani Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ajira, kukuza kipato cha vijana na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Meneja wa Tawi la CRDB Mwanjelwa, Singwa Mwenemilao, amesema benki hiyo imejipanga kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia mikopo yenye masharti nafuu, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kuiamini CRDB kwa huduma zake za kifedha zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii.

Cc @tediusfeston
#MBEYA by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Ruvuma, Venance Msafiri, ameivunja Bodi ya Chama cha Msingi cha Ushirika Mwambesi, Wilaya ya Tunduru, baada ya kuwasilishwa taarifa  wanachama kuibua tuhuma za upotevu na ubadhilifu wa fedha za ushuru wa chama, zikiwamo madai ya kupotea kwa tani tisa za korosho, ununuzi wa ‘gari hewa’, uzito hewa wa tani 20 na hasara katika vituo vya ukusanyaji wa mazao.

Hatua hiyo imekuja baada ya wanachama wa chama hicho, kupitia mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini, Mhandisi Fadhili Chilombe,  ukiofanyika Julai 17, 2026 kushinikiza kupatiwa majibu kuhusu mwenendo wa uendeshaji wa chama na kutaka taarifa ya uchunguzi wa tuhuma walizoziibua.

Mrajis Msaidizi huyo, ambaye alifanya uamuzi huo baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya uchunguzi na maazimio kuhusu mwenendo wa matukio hayo, pia ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza tuhuma hizo na, endapo itabainika kuwa kuna ukiukaji wa sheria, hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.

Katika mkutano wa awali na Mbunge huyo, wanachama walieleza malalamiko mbalimbali kuhusu uendeshaji wa chama hicho, wakidai kuwa mali na fedha zao zimekuwa zikitumika bila uwazi na baadhi ya masuala hayajapatiwa majibu ya kuridhisha.

Miongoni mwa tuhuma zilizowasilishwa ni madai ya kupotea kwa tani tisa za korosho, huku wanachama wakitaka kufahamu zilipo na namna zilivyopotea.

Aidha, wanachama walidai zaidi ya Sh milioni 50 zilizokopwa benki na chama zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa gari ambalo hawajawahi kuliona, huku pia wakieleza kuwepo kwa madai ya ‘ghala hewa’.

Madai mengine ni pamoja na uzito hewa wa tani 20 na hasara katika vituo vya ukusanyaji wa mazao, hali ambayo wanachama walidai imeathiri mali na maslahi yao kama wamiliki wa chama hicho.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhandisi Chilombe aliwataka wanachama kutokaa kimya wanapoona dalili za ubadhilifu, bali kutumia haki yao ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.

Alisema matatizo yanayohusu usimamizi wa mali za wanachama yanaweza kuendelea kwa muda mrefu iwapo taarifa hazitawafikia viongozi na mamlaka zinazohusika kwa wakati, akisisitiza umuhimu wa uwazi na uwajib by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, amezindua eneo la mapumziko maarufu kama Garden ya Kemondo lililopo katikati ya Jiji la Mwanza, kwa ajili ya kuwapa wananchi sehemu salama ya kupumzika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makilagi amesema eneo hilo litasaidia wananchi kupata sehemu ya kupumzika wakati wakisubiri kufanya shughuli mbalimbali za kibiashara na kijamii katika maeneo ya katikati ya jiji.

Aidha, amewataka wakazi wa Wilaya ya Nyamagana kutunza mazingira ya eneo hilo kwa kuepuka kutupa taka ovyo, na badala yake kutumia maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya utupaji taka.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nyamagana, Frank Nkola Chacha, amesema Garden ya Kemondo ina historia kubwa kwa wakazi wa Mwanza na imekuwa sehemu muhimu ya mapumziko kwa wananchi. by @aboodmediatz
0
a day ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up