Posted On: July 24th 2026, 05:40 pm
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara na kuacha utupaji wa taka hovyo.
Akizungumza wakati wa kampeni ya kuhamasisha usafi wa mazingira katika maeneo ya biashara na makazi Magogoni, Kata ya Tungi, Dalmia amepiga marufuku ujenzi holela wa maeneo ya kutupia taka na biashara katika maeneo yasiyo rasmi.
Amesema wananchi wanapaswa kuhakikisha mifereji inasafishwa kwa wakati na wakandarasi wanakusanya taka kwa wakati, ili kuweka Kigamboni katika mazingira safi na yenye mpangilio.