Posted On: July 25th 2026, 04:41 pm
Majeruhi wa ajali mbalimbali jijini Mwanza waliolazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa matibabu, wameiomba serikali kufunga kamera za ulinzi (CCTV) kwenye baadhi ya maeneo muhimu ya barabara, vikiwepo vivuko vya watembea kwa miguu ili iwe rahisi kubaini vyanzo vya ajali na kuharakisha uchunguzi.
Wakizungumza wakati wakipokea misaada ya kiutu kutoka kwa askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo, wagonjwa hao wamemuambia Kamanda wa Polisi, DCP Wilbroad Mutafungwa kuwa, waathirika wengi wa ajali za barabarani hupoteza haki zao kutokana na kukosekana kwa ushahidi, huku wanaosababisha ajali hizo wakikwepa mkono wa sheria.
✍Innocent Aloyce
Mhariri |
@abuuyusuftz #AzamTVUpdates