Instagram story viewer> @azamtvtz> Posts
POSTS STORIES REELS TAGGED
Download All
Heeeeeelloooooo Tanzania 🇹🇿 💃🏻 

@missuniversetanzania imefungua ukurasa mwingine kwa kushirikiana na #AzamTV kupitia #SinemaZetuHD, ambapo fursa kwa wanafunzi wa vyuo ndio hii hapa, jisajili sasa kabla ya Agosti pili mwaka huu.

Burudani ya vipindi vya #MissUniverseTanzania2026 utaanza kuipata kuanzia Agosti 8 saa 2:00 usiku ndani ya @sinemazetuhd chaneli namba 106.

#HelloTanzania #MissUniverseTanzania by @azamtvtz
7
5 hours ago
Download
#JakamoyoSeries | Chuma kinaanza Ijumaa hii Julai 24, 2026 kuanzia saa 1:30 usiku kupitia #SinemaZetuHD chaneli namba 106 #AzamTV inayopatikana pia ndani ya @azamtvmaxapp by @azamtvtz
76
2 days ago
Download
#4Utaweza? 😊 by @azamtvtz
45
8 days ago
Download
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Ussi Salum Pondeza amewashauri viongozi wa siasa na kada nyingine kujitolea kuchangia ukuaji wa elimu kwa namna wanayoweza ili kulisaidia taifa.

Pondeza amesema hayo wakati akikabidhi gari aina ya Toyota Alphard kwa uongozi wa Chuo cha Kiislamu Mazizini akisema anachangia kurahisisha utekelezaji wa shughuli za chuo hicho.

Mhariri @moseskwindi

#AzamTVUpdates by @azamtvtz
4
an hour ago
Download
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema serikali chini ya uongozi wa Rais wa Samia Suluhu Hassan  imedhamiria kutawanya miradi mingi ya maendeleo ili kupeleka huduma za msingi na manufaa kwa wananchi wote.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bukombe baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa stendi kuu ya kisasa ya mabasi katika Kata ya Katente wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 22 Mavunde amesema: “Dkt. Samia amedhamiria kuwafanya wananchi kunufaika na rasilimali za Taifa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa naye inaendelea kuweka mazingira bora ya kunufaika kwa kila mwananchi popote alipo na katika sekta zote kuhakikisha wanapata huduma stahiki kwa ubora ili kufurahia maendeleo yao.”

��Mbali ya ukaguzi wa stendi hiyo pia Mavunde amefanya ukaguzi wa miradi mingine ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami nyepesi yenye urefu wa kilomita 1.2 kutoka Uyovu hadi Namonge unaogharimu zaidi ya Shilingi milioni 917.6, mradi wa maji katika Kijiji cha Businda, Kata ya Bulangwa, wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 963.7 unaotarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 9,949 na kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama katika eneo hilo.

Mavunde pia amempongeza Mbunge wa Bukombe, Dkt. Doto Biteko kwa kusaidia upatikanaji wa miradi hiyo na kutoa rai kwa mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji ili mradi ukamilike kwa wakati na kuwawezesha wananchi hususan waliopisha ujenzi wa mradi huo kurejea katika shughuli zao za kiuchumi.�

�Katika hatua nyingine Waziri Mavunde ametoa katazo kwa  wachimbaji wadogo kuvamia maeneo yenye leseni za utafiti na kuagiza kufuatwa kwa sheria na taratibu zilizowekwa ili kuepusha migogoro na ugumu wa usimamizi wa leseni za madini,kwa kuwa serikali sasa inaweka mpango mzuri wa ugawaji wa leseni kwa wananchi wake.

Mhariri @moseskwindi by @azamtvtz
5
2 hours ago
Download
Wakulima wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wanatarajiwa kuongeza matumizi ya teknolojia ili kupata mavuno makubwa ikiwemo kuwa na maarifa ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika shughuli zao.

Hayo yamebainishwa baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya kilimo bora kilichombatana na ufundishwaji wa mbinu za kuongeza masoko ya bidhaa wanazolima.��Kasisi Kosta amezungumza nao.

Mhariri @moseskwindi by @azamtvtz
1
3 hours ago
Download
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikisha upandikizaji wa vifaranga vya samaki sato milioni 1.5 katika Ziwa Rwakajunju wilayani Karagwe.����

Akitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa Wilaya ya Karagwe, Mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa amesema wanaiomba Serikali iwasaidie kupata nyongeza ya vifaranga vya samaki kufikia milioni 5 sambamba na kupatiwa boti ya doria kwa lego la kuongeza ulinzi na usalama wa Mradi huo.

����Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Nazael Madalla ameeleza kuwa Serikali itaongeza vifaranga katika Ziwa Rwakajunju pamoja na kufanya upimaji wa ziwa hilo ili kubaini kama linafaa kwa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.��

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Zaituni Msofe akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ameishukuru Serikali kwa kuleta vifaranga milioni 1.5 vyenye thamani ya shilingi milioni 450.����

Mhariri @moseskwindi by @azamtvtz
5
5 hours ago
Download
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amekagua mradi wa soko la kisasa linalojengwa wilayani Bukombe mkoani Geita sambamba na mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi katika hatua inayolenga kuboresha huduma na kuchochea maendeleo ya kiuchumi wilayani humo.

Miradi hiyo kwa pamoja inatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi laki mbili na kuongeza mapato ya halmashauri kupitia ongezeko la fursa za ajira na uwekezaji.

Taarifa ya Ester Sumira.

Mhariri @moseskwindi by @azamtvtz
4
6 hours ago
Download
Ulipo Tupo! Dodoma Marathon tuko tayari kuwaokoa dhidi ya makato makubwa.

Popote utuonapo usisite kuuliza kuhusu Azampesa.

#azampesa by @azamtvtz
2
6 hours ago
Download
Kamishna Jenerali wa Mmalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amesema wamefanikiwa kudhibiti kwa kiwango kikubwa kilimo cha dawa za kulevya aina ya bangi hali inayoashiria mafanikio ya kijamii.

Msikilize hapa.

Mhariri @moseskwindi by @azamtvtz
15
20 hours ago
Download
Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu (TAREA) imezindua mradi maalumu wa kuwasaidia wajasiriamali wanaofanya biashara ya nishati safi ya kupikia ili kuwaondolea vikwazo mbalimbali vinavyokwamisha shughuli zao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TAREA, Prosper Magali amesema wajasiriamali hao wanakabiliwa na vikwazo vingi ikiwemo ukosefu wa mitaji, kufikia masoko na ugumu wa kurasimisha biashara zao.

Mhariri @moseskwindi by @azamtvtz
5
20 hours ago
Download
Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndio amesema Serikali imeendelea kuimarisha mikakati ya usalama ya uhifadhi na usafirishaji wa kemikali ya 'sulphur' ili kuongeza usalama wa udhibiti wa athari ya kemikali hiyo. 

Hayo ameyabainisha katika kikao kazi na wasimamizi wa kemikali hiyo katika ngazi mbalimbali za utendaji tangu kupokelewa bandarini hadi kusafirishwa nje ya nchi.

Mhariri @moseskwindi by @azamtvtz
5
20 hours ago
Download
×

Download all media on this page

Photos Videos
back to up