Posted On: September 7th 2026, 09:22 am
Siku ya Ijumaa,
#ArudiShuleChampions wetu
@eda_mathias_ alipata fursa ya kushiriki uzinduzi wa jukwaa la “One Girl Plus”, lililozinduliwa na Msichana Initiative likiwa na lengo la kufikia wasichana wengi zaidi na kuwapa fursa ya kujiendeleza. Jukwaa hili sasa linapatikana rasmi katika tovuti ya Msichana Initiative.
Tunaipongeza
@msichanainitiative kwa hatua hii muhimu ya kuongeza wigo wa huduma kwa wasichana, na tunafuraha kuona Champion wetu kuwa sehemu ya matukio kama haya yanayolenga kuinua sauti na fursa za wasichana nchini.
#OneGirlPlus