Instagram story viewer> @tzrailways> Post
2 months ago
Photo by Tanzania Railways Corporation on August 23, 2026. May be an image of poster, calendar and text.
Photo by Tanzania Railways Corporation on August 23, 2026. May be an image of train, poster, calendar, terminal and text.
153
Posted On: August 24th 2026, 04:39 am
ONGEZEKO LA SAFARI ZA SGR KUANZIA SEPTEMBA 01, 2026!

Tumeongeza idadi ya safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma ili kukupa urahisi zaidi wa kupanga Safari zako kila siku.

Sasa una fursa ya kuchagua muda unaokufaa zaidi, kagua ratiba hapo juu kuona muda wa kuondoka na kuwasili wa treni za Express, Royal Express, na Ordinary.

Kata Tiketi kupitia sgrticket.trc.co.tz au pakua SGR App.

Tupigie simu ya Bure 0800 110 042 au Chati nasi Whatsapp 0738 594 962
Comments (153)
yahyagonga 4 hours ago

yahyagonga

Booking zinaonekana kujaa lkn ukifika ndan ya treni nyeupeeee vp hapo?

kelvinkagoro 15 days ago

kelvinkagoro

Ndugu nashindwa kujiunga na app yetu pia page yenu inasumbua

dullahsuma1977 16 days ago

dullahsuma1977

MKURUGENZI @tzrailways tangu mwaka wa jana treni ya sgr hapa Ruvu station haishushi wala kupandisha abiria tangu itokee Ile ajali mpaka leo mnashindwa kurekebisha kwani tunashida gani watanzania?

wteeshaban40 16 days ago

wteeshaban40

ZERO BRAIN NAULI YA WENGI MNAPUNGUZA ROUTE NA KUWEKA ZA BEI JUU ILI BEHEWA ZITEMBEE TUPU

fredy_21_s 16 days ago

fredy_21_s

TUNAOMBA MRUDISHIE TRENI YA KAWAIDA KWENYE SAFARI YA ASUBUI KUTOKA MORO KWENDA DAR. WENGI WETU TUNAITUMIA NDIO MAANA KILA WAKATI INAJAA.

mwabuselectors 16 days ago

mwabuselectors

Route ya moro dar, saa tatu hii kuiondoa ile ya elf 13500 na kuweka ya 50k ni shida sana ilikua rout msaada sana kwa watu kwenda dar na kurudi same day saiz inabid wakapand ma basi

mcharo_homes_changombe_temeke 17 days ago
msafa_store 17 days ago

msafa_store

TRC tupeni majibu kwann mmebadilisha bei ya sa3 ikiw sio kila mtu ana uwezo wa 50k bas wekeni hata ya 22k iyo sa3

msafa_store 17 days ago

msafa_store

Naomba kuuliza ni kwann treni ya saa3 mmepandisha kutoka tsh 13,500 mpka Tsh 50,500?

kazala_tza 2 months ago

kazala_tza

Ratiba ya sasa bado sio rafiki sana kwetu wasakatonge napendekeza route ya Dodoma Moro Dar iwe hivi saa 11 asbh itoke treni ya ordinary saa 2 asbh itoke treni ya royal express au mchongoko ,saa 8 mchana itoke treni ya ordinary na saa 11 jioni itoke ya express then kwa route Moro Dar zianze saa 6 mchana na saa 1 usiku nafikiria ratiba itakaa vzr sana @tzrailways

rodgersasu 2 months ago

rodgersasu

hayo ma route ya mchana mmeyajaza kama nini, mabasi yanatembea usiku kucha, kwanini kusiwe na SGR inayo fika Dar au Dom saa 1/2 kamili asubuhi??

paschal_vfx 2 months ago

paschal_vfx

Kunatakiwa kuwa na at least train moja ya ordinary asubuhi, mchana na jioni kutoka na kwenda pande zote mbili. Mlichofanya siyo fair

mwl.neema_maisha 2 months ago

mwl.neema_maisha

Sasa hapa wameongeza nini!?kwan kila mwananchi anauwezo wa mchongoko

bafuba.updates 2 months ago

bafuba.updates

🔥🙌

beka_king 2 months ago

beka_king

Hello TRC, Leo nimehudhunishwa sana na huduma yenu, Jana saa 11 na dk 57 jioni nilikata ticket ya MGR kupitia tovuti toka MAKINYUMBI to DAR ES SALAAM kwenye mtandao, baada ya kukata nikapga simu ile Toll free 0800110042 , kwa ajili ya confirmation ya muda, kwenye mtandao waliandika saa 11:40 asubuh, so nikapga simu namba hzo ili kuhakiki muda , akapokea dada sikumbuki jina ila kwa kuwa najua simu zinarekodiwa ni rahis kwa ninyi kumfahamu, akasema muda ndo huo huo ulioandokwa kwenye mtandao. Nafika station Train limeondoka saa 8 usiku. Ntaambatanisha screenshot za ticket, na muda niliopga kwa ajili ya confirmation. Sasa nasaidiwaje...?? Mambo kama haya ndo yanafanya wananchi kuichukua serikali kwa makosa mtu mmoja ambaye hajui wajibu wake, hajui hata ratba ya ktu anachokifanyia kazi.

Load More

More posts

back to up