Instagram story viewer> @tzrailways> Posts
141.8K
followers
217
following
Official account for Tanzania Railways Corporation |
Ukurasa rasmi wa Shirika la Reli Tanzania
Toll Free 0800110042
Bofya kukata Tiketi za SGR👇
POSTS STORIES REELS TAGGED
ONGEZEKO LA SAFARI ZA SGR KUANZIA SEPTEMBA 01, 2026! 

Tumeongeza idadi ya safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma ili kukupa urahisi zaidi wa kupanga Safari zako kila siku.

Sasa una fursa ya kuchagua muda unaokufaa zaidi, kagua ratiba hapo juu kuona muda wa kuondoka na kuwasili wa treni za Express, Royal Express, na Ordinary. 

Kata Tiketi kupitia sgrticket.trc.co.tz au pakua SGR App.

Tupigie simu ya Bure 0800 110 042 au Chati nasi Whatsapp 0738 594 962 by @tzrailways
152
2 months ago
Download
Why pay more when you can travel better?
SGR offers comfort, speed, and affordable fares.
 Choose smart. Choose SGR
______________________________________________________________
Kwa nini ulipe zaidi wakati unaweza kusafiri kwa ubora zaidi?
SGR inakupa safari yenye faraja, kasi na nauli nafuu.
Chagua kwa busara. Chagua SGR. by @tzrailways
47
9 months ago
Download
Ukiona ujumbe kama "Scan to share for feedback" katika kituo cha SGR au ndani ya treni ya SGR, unamaanisha:
Changanua (scan) msimbo wa QR kwa kutumia kamera ya simu yako.
Msimbo huo utakuelekeza kwenye fomu ya maoni inayosimamiwa na TRC (Shirika la Reli Tanzania).
Unaweza kutoa maoni yako, kutathmini huduma uliyoipata wakati wa safari, au kuripoti changamoto ili kusaidia kuboresha huduma za SGR.

@gersonmsigwa @david_kihenzile
------------------------------------------------------------------------
If you saw a message like "Scan to share for feedback" at an SGR station or on an SGR train, it usually means:
Scan the QR code with your phone's camera.

It will open a feedback form managed by TRC.
You can submit comments, rate your travel experience, or report issues to help improve the service. In kiswahili please. by @tzrailways
8
3 months ago
Download
Wiki njema kwako..! by @tzrailways
2
18 hours ago
Download
Shirika la reli Tanzania (TRC) na kampuni ya Arab contractors ya nchini Misri, zimetia saini hati ya makubaliano kuhusu mradi wa reli ya Mtwara–Songea–Mbamba bay, yenye matawi ya Mchuchuma na liganga, hafla iliyofanyika Oktoba 16, 2026 Jijini Dar EsS alaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Akizungumza muda mchache baada ya tukio la utaiji Prof. Mbarawa, alisema, mradi wa Reli ya Kusini una umuhimu wa kipekee katika kufungua fursa za kiuchumi katika Ukanda wa Kusini aidha aliongeza kusema kuwa Reli hiyo  inatarajiwa kuunganisha Bandari ya Mtwara na maeneo ya uzalishaji wa kilimo, madini na viwanda, hususan miradi ya Mchuchuma na Liganga. 

Akitolea ufafanuzi utiwaji Saini huo, Prof. Mbarawa, alisema, ‘’makubaliano yanayosainiwa leo ni hatua ya maandalizi ya mradi huu muhimu.Kupitia ushirikiano huu, tunatarajia kufanyika kwa tafiti za kina zitakazobainisha mahitaji ya usafirishaji, gharama za mradi, manufaa yake ya kiuchumi na njia zinazowezekana za kupata fedha za utekelezaji.

Waziri huyo wa Uchukuzi, Pamoja na mambo mengine, alisisitiza mambo matatu ambayo ni, 

‘’Kwanza, TRC na Arab Contractors waandae mpango wa kazi wenye majukumu, na matokeo yanayotarajiwa na muda maalumu wa utekelezaji. Pili, tafiti zizingatie uhalisia wa kiuchumi, mahitaji ya mizigo na uwezekano wa kupata fedha za ujenzi na uendeshaji wa reli. Tatu, ushirikiano huu uhakikishe ushirikishwaji wa taasisi muhimu, ujenzi wa uwezo wa wataalamu wa Tanzania na uzingatiaji wa maslahi ya Taifa’’, alimalizia Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Shiwa, amesema hati hiyo ya Makubaliano iliyosainiwa inaweka msingi wa ushirikiano katika kufanya tafiti na kuandaa mapendekezo ya kitaalamu na kifedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Mha. Machibya,  ameeleza kuwa, kwa mujibu wa makubaliano hayo, Arab Contractors itafanya tafiti za awali na upembuzi yakinifu kwa gharama zake, ikitarajiwa kuwasilisha taarifa ya awali ndani ya miezi mitatu tangu kusainiwa kwa hati hiyo.

#manaratvupdate by @tzrailways
4
3 days ago
Download
Shirika la reli Tanzania (TRC) na kampuni ya Arab contractors ya nchini Misri, zimetia saini hati ya makubaliano kuhusu mradi wa reli ya Mtwara–Songea–Mbamba bay, yenye matawi ya Mchuchuma na liganga, hafla iliyofanyika Oktoba 16, 2026 Jijini Dar EsS alaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Akizungumza muda mchache baada ya tukio la utaiji Prof. Mbarawa, alisema, mradi wa Reli ya Kusini una umuhimu wa kipekee katika kufungua fursa za kiuchumi katika Ukanda wa Kusini aidha aliongeza kusema kuwa Reli hiyo  inatarajiwa kuunganisha Bandari ya Mtwara na maeneo ya uzalishaji wa kilimo, madini na viwanda, hususan miradi ya Mchuchuma na Liganga. 

Akitolea ufafanuzi utiwaji Saini huo, Prof. Mbarawa, alisema, ‘’makubaliano yanayosainiwa leo ni hatua ya maandalizi ya mradi huu muhimu.Kupitia ushirikiano huu, tunatarajia kufanyika kwa tafiti za kina zitakazobainisha mahitaji ya usafirishaji, gharama za mradi, manufaa yake ya kiuchumi na njia zinazowezekana za kupata fedha za utekelezaji. by @tzrailways
6
3 days ago
Download
Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri zimetia saini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika maandalizi ya mradi wa Reli ya Kusini, utakaounganisha Mtwara–Songea–Mbamba Bay pamoja na matawi ya Mchuchuma na Liganga.

Hafla ya utiaji saini imefanyika Oktoba 16, 2026, jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mbarawa amesema mradi huo una umuhimu mkubwa katika kufungua fursa za kiuchumi katika Ukanda wa Kusini kwa kuunganisha Bandari ya Mtwara na maeneo ya uzalishaji wa kilimo, madini na viwanda, hususan miradi ya Mchuchuma na Liganga.

Amesema makubaliano hayo ni hatua ya maandalizi ya mradi, ambapo kampuni ya Arab Contractors itafanya tafiti za awali, upembuzi yakinifu na kuandaa mapendekezo ya kitaalamu na kifedha yatakayosaidia Serikali kufanya maamuzi kuhusu utekelezaji wake.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa, kampuni hiyo inatarajiwa kuwasilisha taarifa ya awali ndani ya miezi mitatu tangu kusainiwa kwa makubaliano. Baada ya taarifa hiyo kuidhinishwa, upembuzi yakinifu wa kina utafanyika ndani ya miezi tisa, ukifuatiwa na maandalizi ya pendekezo la mradi kwa ajili ya kutafuta ufadhili katika kipindi kingine cha miezi tisa.

Mradi wa Reli ya Kusini unalenga kuimarisha usafirishaji wa mizigo na bidhaa, kuchochea uwekezaji katika sekta ya kilimo, madini na viwanda, pamoja na kufungua fursa mpya za biashara na ajira kwa wananchi wa Ukanda wa Kusini na Tanzania kwa ujumla.

________________________ 

Tufuatilie STBongo TV kwenye:
⭐ StarTimes → CH 161 & 401
▶️ YouTube → BONGO MAX TV

#STBongoTV #STBongoUPDATES #nyumbanikwanza BongoMaxTv by @tzrailways
0
3 days ago
Download
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa, wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano (MoU) kati ya TRC na kampuni ya Arab Contractors ya Misri...kwa maelezo zaidi endelea kufuatulia mitandao yetu ya jamii. by @tzrailways
8
4 days ago
Download
Usikose by @tzrailways
3
4 days ago
Download
Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la reli Tanzania (TRC) Bw. Athumani Janguo, katika sehemu ya simulizi yake kuhusu nini baba wa Taifa alifanya kwenye sekta ndoho ya reli kufuatia kuvunjika kwa Jumuia ya Afrika Mashariki....simullizi nzima unaipata you yube @relitv

@david_kihenzile @gersonmsigwa @ikulu_mawasiliano @prof.mbarawa by @tzrailways
1
6 days ago
Download
Sehemu ya Simulizi ya Mkurugenzi Mkuu wa  TRC 1996-2007, Linford Mboma, wakati huu Taifa linaadhimisha miaka 27 ya kumbukizi ya kifo cha baba wa Taifa...Simulizi yote utaipa you tube @relitv

@gersonmsigwa @david_kihenzile @prof.mbarawa @ikulu_mawasiliano by @tzrailways
2
6 days ago
Download
Ni miaka 27 hatuko na wewe baba wa Taifa, lakini umeacha alama katika sekta ndogo ya reli nchini, hata sasa tunapojivunia mageuzi katika usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo, hakika ni maono yako. Endelea kupumzika kwa amani baba.

@david_kihenzile
@gersonmsigwa
@ikulu_mawasiliano by @tzrailways
18
6 days ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up