Instagram story viewer> @cce9840> Post
11 days ago
0
Posted On: October 9th 2026, 08:19 am
😂 Hapa si Bonde la Ngorongoro! Ni Kijiji cha Yaeda Chini katika Bonde la Yaeda, Mbulu, kaskazini mwa Tanzania, wakati wa kiangazi katika misitu ya savana za kitropiki.

🌿 Jamii za asili na za kitamaduni zikiwezeshwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi, ushirikishwaji wa wananchi na ushirikiano wa serikali na wataalamu, zinaweza kuendeleza maisha yao huku zikihifadhi mazingira na viumbe hai.

🐝 Ujasiriamali wa kiuchumi unaoendana na utamaduni na uhifadhi kama ufugaji nyuki, biashara endelevu za mifugo , utalii wa urithi wa kitamaduni, biashara ya kaboni nakadhalika unaweza kuongeza kipato bila kuharibu mazingira.

🌍 Uhifadhi wa maeneo haya ni muhimu kwa kulinda viumbe hai, kupunguza mabadiliko ya tabianchi kwa kufyonza hewa chafu na kudumisha maisha ya jamii zinazotegemea asili.

💚 Vijiji 12 vya Yaeda–Eyasi, katika eneo lenye zaidi ya hekta 200,000, vinaonesha mfano unaoweza kuigwa na jamii nyingine katika maeneo yanayofaa.

More posts

back to up