Instagram story viewer> @cce9840> Posts
48
followers
167
following
POSTS STORIES REELS TAGGED
🌿 Asili ni msingi wa maisha, utamaduni na kipato chetu. Jamii hutegemea asili kwa chakula, maji, malisho ya mifugo, kipato na urithi wa utamaduni. Kuitunza ni kulinda bayoanuai, tabianchi na maisha ya vizazi vijavyo.

🤝 Ushirikishwaji wa jamii kupitia vikao vya hadhara huwezesha wananchi kutoa maoni, kufanya maamuzi ya pamoja kuhusu matumizi bora ya ardhi, kuweka kanuni zao zinazokubalika na wote kwa uhifadhi na kusimamia rasilimali zao kwa uwazi na uwajibikaji.

🌍 Ushirikiano wa kweli ni muhimu kati ya jamii, serikali na wadau wengine kwa kusaidia kuimarisha haki za ardhi, rasilimali, utaalamu na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uhifadhi,maendeleo endelevu kwa kupambana na hali ya umaskini inayowakumba hasa jamii za asili kwa muda mrefu hadi sasa.

🌱 Vijiji 12 vya Yaeda–Eyasi, kaskazini mwa Tanzania, vinaendelea na jitihada za kuonesha umuhimu wa mbinu hizi katika mandhari yenye zaidi ya hekta 200,000. Fedha za tabianchi kupitia mradi wa kaboni uliothibitishwa kwa zaidi ya miaka 15 zimesaidia kwenye kuimarisha uhifadhi wa misitu,nafuu kwa maisha ya jamii na usalama wa urithi wa mababu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. 🤝🌳 taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
3 days ago
Download
🌿 Asili ni msingi wa maisha yetu.

Jamii nyingi za asili huishi kwa ukaribu na mazingira na hutumia rasilimali zake kwa njia zinazosaidia kulinda uhai wa asili.

🌱 Asili hutupatia mahitaji muhimu ya maisha. Wawindaji-wakusanyaji hupata matunda, asali na mizizi porini; wafugaji hutegemea maji na malisho; wakulima hutegemea ardhi yenye rutuba na mvua; huku wavuvi wakitegemea samaki na rasilimali za baharini.

🪶 Asili hulinda utamaduni wetu. Hutupatia chakula na kipato, huku ikitusaidia kuendeleza mila, desturi na maarifa ya mababu zetu kwa vizazi vijavyo.

🌍 Kulinda asili ni kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Misitu, ardhi na vyanzo vya maji hutusaidia kuhifadhi mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

🤝 Ushirikiano ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Jamii, serikali na wadau wenye uwezo wa kifedha wanapaswa kushirikiana, kuthamini maarifa ya wenyeji na kuhakikisha wanaolinda asili wanapata msaada na manufaa yanayostahili.

🌿 Ndiyo maana eneo la Yaeda–Eyasi, kaskazini mwa Tanzania, ni mfano muhimu wa juhudi za kulinda asili. Jamii zinaendeleza urithi wa mababu zao ili kuhakikisha asili inalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Kulinda asili ni kulinda maisha, utamaduni, mustakabali wa watoto wetu na vizazi vijavyo.

"Happy indigenous Day" taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
7 days ago
Download
🌿 Moja ya vikumbusho kuhusu haki za jamii katika ardhi na mbinu bora za kuboresha maisha, kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 🌍🤝 taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
8 days ago
Download
😂 Hapa si Bonde la Ngorongoro! Ni Kijiji cha Yaeda Chini katika Bonde la Yaeda, Mbulu, kaskazini mwa Tanzania, wakati wa kiangazi katika misitu ya savana za kitropiki.

🌿 Jamii za asili na za kitamaduni zikiwezeshwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi, ushirikishwaji wa wananchi na ushirikiano wa serikali na wataalamu, zinaweza kuendeleza maisha yao huku zikihifadhi mazingira na viumbe hai.

🐝 Ujasiriamali wa kiuchumi unaoendana na utamaduni na uhifadhi kama ufugaji nyuki, biashara endelevu za mifugo , utalii wa urithi wa kitamaduni, biashara ya kaboni nakadhalika unaweza kuongeza kipato bila kuharibu mazingira.

🌍 Uhifadhi wa maeneo haya ni muhimu kwa kulinda viumbe hai, kupunguza mabadiliko ya tabianchi kwa kufyonza hewa chafu na kudumisha maisha ya jamii zinazotegemea asili.

💚 Vijiji 12 vya Yaeda–Eyasi, katika eneo lenye zaidi ya hekta 200,000, vinaonesha mfano unaoweza kuigwa na jamii nyingine katika maeneo yanayofaa. taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
11 days ago
Download
🐝" Kumlinda nyuki ni kulinda maisha yetu". 

Ufugaji wa nyuki ni mojawapo ya njia kuu katika kulinda asili ikiambatana na kuleta kipato, kuongeza uzalishaji wa chakula hasa kupia uchamvushaji, hulinda misitu na bioanuwai zingine kwa ujumla na kuchangia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 🌳🌍

Hivyo ni vyema Tuwalinde nyuki, tuhifadhi mazingira na tujenge uchumi endelevu. 🤝🐝 taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
13 days ago
Download
Kitu cha thamani zaidi tunachoweza kuwaachia vizazi vijavyo si kile tunachochukua kutoka kwenye Sayari, bali ni kile tunachochagua kukilinda,kukitumia kwa njia endelevu na kukirejesha inapobidi.

Tunapoacha alama zetu duniani, tujiulize: Tunajenga urithi wa kuharibu, au wa kurejesha na kutunza mazingira? by @cce9840
0
20 days ago
Download
Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bioanuwai na umaskini, ni muhimu kuimarisha mbinu zinazolingana na maisha chanya ya jadi ya jamii. Kila suala muhimu linapaswa kupewa nafasi.

Msingi wa jamii kuwa walinzi wa asili ni kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi ya vijiji pamoja na Hati za Kimila za Kumiliki Ardhi (CCROs), zinazopatikana kupitia makubaliano shirikishi ya jamii kwa usaidizi wa Serikali na wadau wenye nia njema.

Mipango hii kwa njia shirikishi kwa wananchi huainisha maeneo ya misitu ya ulinzi, uwindaji na ukusanyaji, malisho, makazi ya kudumu na kilimo, huku kanuni za pamoja zikisaidia kulinda asili na utamaduni na hata kupelekea kuanzisha fursa za kipato kama ufugaji nyuki, utalii wa kitamaduni, ufundi wa jadi, bidhaa za asili na ufugaji endelevu.

Katika Dunia ya sasa kadiri watu na shughuli za kibinadamu zinavyoongezeka, kupanga matumizi ya ardhi mapema husaidia kuzuia migogoro, uharibifu wa mazingira na kupoteza uwiano muhimu wa maisha.

Yaeda–Eyasi Kaskazini mwa Tanzania, kupitia vijiji 12 vyenye zaidi ya hekta 200,000 za mipango ya matumizi ya ardhi, ni mfano wa vitendo unaoendelea kusaidia maisha ya zaidi ya IPLCs 100,000 kupitia manufaa ya kiuchumi na yasiyo ya fedha. Mfano huu wa thamani kubwa unaweza kuigwa kwa maeneo mengine yenye mazingira na jamii mabingwa wa asili. taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
22 days ago
Download
🌿 Asili ndiyo msingi wa maisha bora, uchumi wa jamii, ustawi wa kijamii na hali ya hewa salama. 

Enzi za mababu, ujuzi wa jadi uliendana zaidi na mazingira na uliwezesha matumizi yenye uwiano; leo hali imebadilika kutokana na ongezeko kubwa la watu, mahitaji yanayoongezeka na utumiaji uliopitiliza wa rasilimali, huku jamii maskini zikibeba athari kubwa za uharibifu na mabadiliko ya tabianchi bila kuwa chanzo kikuu.

🌍 Leo, mchanganyiko wa maarifa ya jadi na mbinu rahisi za kisasa—ikiwemo ukusanyaji wa taarifa kwa maandishi au kidijitali—husaidia kufanya maamuzi yanayopimika, kuthibitisha matokeo na kushirikisha wataalamu pamoja na jamii. 

Maeneo mengi ya IPLCs bado yamehifadhi bioanuwai muhimu; hivyo ni muhimu kutambua, kulinda na kuwalipa kwa uwazi kwa kazi zao zinazoweza kuthibitishwa katika kulinda mazingira.

💚 Msaada unaweza kupitia mifuko ya kijani, ruzuku na uwekezaji wa mazingira, huku soko la kaboni lenye uadilifu wa hali ya juu likiwezesha kazi za uhifadhi zenye matokeo yanayopimika kugeuzwa kuwa mapato yanayorudi moja kwa moja katika ulinzi wa ardhi na ustawi wa jamii.

🇹🇿 Yaeda–Eyasi, kaskazini mwa Tanzania, ni mfano wa zaidi ya miaka 15 wa mfumo huu: mapato ya mradi wa kaboni yameendelea kuimarisha haki za ardhi na usalama wa rasilimali, huku ikidaiwa kuzuia zaidi ya tani 160,000 za hewa chafu kwa mwaka. 

Zaidi ya vijana 150 wa jadi wameajiriwa na jamii kama walinzi wa mazingira, huku mapato yakisaidia elimu, afya, chakula na maendeleo ya jamii.

🌱 Mfumo huu unaweza kuigwa katika maeneo mengine, huku mipango mizuri ya matumizi ya ardhi ikiwa msingi wa mafanikio ya muda mrefu. taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
a month ago
Download
Asili si kitu kilichotenganishwa na uchumi; ndiyo msingi wa kila uchumi.

Kwa ajili ya kuboresha maisha, kukuza maendeleo endelevu, na kuhakikisha tabianchi inayofaa kwa viumbe wote duniani, ni muhimu kutambua na kuthamini mchango wa asili.

Tunapoendelea kupata mafanikio hasa kupitia fursa rafiki kwa utamaduni na mazingira, ni lazima iambatane sambamba na kushirikiana kikamilifu kwa namna yoyote iwezekaanvyo katika kuendeleza na kulinda uhifadhi wa asili kwa sababu ndilo suluhisho muhimu dhidi ya changamoto za sayari mfano wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi nakadhalika,kwa kutumia njia bora, endelevu na zenye matokeo chanya kotekote 🤝. taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
a month ago
Download
Enzi za mababu, ardhi na rasilimali asilia zilikuwa nyingi, idadi ya watu na ushindani wa mahitaji ukiwa mdogo, hivyo gharama za maisha zilikuwa nafuu kuliko leo. Sasa ongezeko la watu, mahitaji ya huduma muhimu na shinikizo la kiuchumi vimeongeza uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi na migogoro.

Hata hivyo, maeneo mengi ya Jamii za asili na kitamaduni bado yana mazingira yenye afya. 

Katika maeneo haya Mipango shirikishi na jumuishi ya matumizi ya ardhi, inayoheshimu haki na maarifa ya jamii, ni msingi wa kulinda bayoanuai, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha usalama wa ardhi na kujenga maendeleo endelevu.

Mipango hiyo huamuliwa na wahusika kwa njia shirikishi kwa kutambua misitu ya kijamii na maisha yanayohusiana moja kwa moja na asili ya sehemu husika kama uwindaji na ukusanyaji, ufugaji, kilimo hai cha jadi, uvuvi, ufugaji nyuki ,utalii wa kiutamaduni nakadhalika.

Mipango bora ya ardhi za jamii au vijiji ni chachu ya kusababisha kuanzishwa kwa fursa mbalimbali za uchumi/Ujasiriamali jumuishi wa kijani kama ufundi wa jadi, bidhaa za asili, biashara endelevu n.k.

Maeneo ya asili ya Jamii yana bayoanuai kubwa kama misitu na ni muhimu yakisaidiwa vizuri katika usimamizi wal wa kisawasawa kwani ni MAGHALA makubwa ya kufyonza hewa chafu za kaboni(hewa ukaa), ambapo kazi hii huweza kuthibitishwa kwa vipimo halali na jamii kulipwa moja kwa moja kwa uwazi katika kuchangia kudhibiti mabadiliko tabianchi, licha ya kuwa miongoni mwa wachangiaji wadogo zaidi wa uchafuzi wa dunia.

Kaskazini mwa Tanzania, mandhari ya vijiji 12 vya Yaeda–Eyasi yenye eneo rejea la takriban hekta 208,000 imeendelea kunufaika na hekta 110,000 za misitu ya asili pekee inayolindwa kwa pamoja, ikiunga mkono wawindaji-wakusanyaji, wafugaji, wakulima wadogo ,utalii wa kiutamaduni kama DOROBO, tafiti na mradi wa kaboni unaohakikiwa kuondoa zaidi ya tani 170,000 za CO₂e (hewa ukaa) kila mwaka.

Kwa zaidi ya miaka 15 ,Yaeda-Eyasi imekuwa ni mojawapo ya mifano inayoendelea kuigwa na vijiji vya jirani pamoja na sehemu nyingine nchini taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
a month ago
Download
Kwa ujumla jamii za Asili na wenyeji zina urithi mkubwa wa kiutamaduni unaoishi kwa mshikamano wa karibu na mazingira, ikiwemo uwindaji na ukusanyaji endelevu, ufugaji wa asili, kilimo rafiki kwa ikolojia,uvuvi unaozingatia uhifadhi wa bahari na mikoko,nakadhalika.

Maeneo yao bado hayajaathiriwa sana na yana misitu, bioanuwai kubwa, vyanzo vya maji, maeneo ya kihistoria, maarifa ya jadi na mazingira yenye afya.

Pia maeneo haya ya Jamii hizi ni muhimu katika kuhifadhi kaboni (Hewa chafu za ukaa zinazozalishwa hasa baada ya mfumuko mkubwa wa mapinduzi ya viwanda), hivyo kusaidia kupambana dhidi ya mabadiliko mabaya ya tabianchi.

Hata hivyo, pamoja na utajiri huu, jamii nyingi bado zinakabiliwa na umaskini na ugumu wa maisha,zaidi katika Dunia ya leo iliyojaa ushindani kwa kutumia maarifa ya kitaalamu na ongezeko la gharama za kila siku.

Huu ni wakati sahihi wa kutambua utajiri wa urithi na mchango wao katika ajenda shirikishi za majukwaa mbalimbali Duniani kwa kuwezesha na kuendeleza fursa zinazoendana na tamaduni zao katika kuongeza kipato na kuchochea ubingwa wao wa kulinda ASILI

Ujasiriamalikijani kama ufugaji nyuki, biashara endelevu ya mifugo, mazao ya asili yenye bei nzuri, bidhaa za misitu zisizo za mbao, utalii wa kiutamaduni,uthibitishaji salama wa maarifa ya dawa za jadi n.k. ni mifano ya miradi inayoweza kuanzishwa na kikundi au mtu binafsi kwa urahisi hata kwa mtaji mdogo kabisa.

Mafanikio endelevu yatawezekana kupitia ushirikiano imara na wa kweli kati ya jamii, serikali, wataalamu, sekta binafsi, taasisi za kiraia na wadau wa kimataifa, huku sauti na vipaumbele vya jamii vikipewa nafasi ya msingi. taken in Yaeda Valley by @cce9840
0
a month ago
Download
Katika dunia ya sasa, programu yoyote yenye manufaa huhitaji taarifa sahihi, za msingi na zinazoweza kuthibitishwa.

Maarifa ya jadi ya jamii yawekwe katikati ya maamuzi, hasa katika miradi ya maeneo yao, kwa kuwa jamii huzifahamu vyema ardhi, misitu, maji, wanyama na mabadiliko ya mazingira.

Maarifa hayo yakichanganywa kwa ushirikiano na mbinu rahisi za kisayansi—kama kuweka kumbukumbu kwenye karatasi au vifaa vya kidijitali, ukusanyaji wa takwimu na ufuatiliaji—husaidia kuthibitisha taarifa, kupanga hatua sahihi na kurahisisha ushirikiano na serikali, wataalamu, wafadhili na wadau wengine.

Kwa zaidi ya miaka 15 hadi leo, jamii za Yaeda–Eyasi kaskazini mwa Tanzania zimeonyesha mafanikio ya mfumo unaoheshimu utamaduni wao kupitia uchumi wa kijani wa biashara ya kaboni na ulinzi wa misitu yao, ukileta manufaa ya kifedha na yasiyo ya kifedha.

Mfumo huu unaweza kupanuliwa katika maeneo mengine yenye jamii zinazolinda asili, pamoja na programu nyingine zenye malengo yanayofanana. taken in Yaeda Valley by @cce9840
1
2 months ago
Download

Download All

Save the photos and videos currently loaded on this page.

0Photos
0Videos
Ready to download 0 / 0

Keep this tab open until your download is ready.

back to up