Posted On: October 14th 2026, 11:20 am
Tunapoadhimisha Siku ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, tunatafakari msingi wa haki, umoja na utu aliyotuachia, na wajibu wetu wa kuhakikisha misingi hii inalinda haki na utu wa kila mtoto.
Ndoa za utotoni, ukatili dhidi ya watoto na kunyimwa fursa ya elimu ni changamoto zinazohitaji dhamira na nia ya pamoja kama taifa ili kuzitatua.
Kupitia Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN), tunaendelea kutetea haki za watoto na kuhimiza jamii kuchukua hatua kuhakikisha kila mtoto anakua salama, analindwa na anapata fursa ya kutimiza ndoto zake.
#HappyNyerereDay #NyerereDay #mwalimunyerere #BabaWaTaifa #TECMN #EndChildMarriage